Mwanamuziki wa Bongo Fleva Nandy , ameeleza siri ya
ufanisi wake katika kazi ya kimuziki, ni kufanya kitu kwa kujitoa na kuelekeza
nguvu zote na kuhakikisha lengo linatimia.
Nandy anaamini kuwa kufanya muziki mzuri ambao unavutia
kwa namna moja au nyingine pia wenye maudhui mazuri ni moja ya kufika mbali
kimuziki
“kikubwa
ni kufanya muziki mzuri unajua wananchi nao saiviwanaelewa muziki kwahiyo
ukifanya kitu kizuri au kibaya lazima watakwambia kitu ambacho napenda sababu
ni moja ya kujifunza zaidi kwangu” alisema Nandy.
Aidha aliwataka mashabiki wake katika mwaka huu
kutalajia kupata mziki mzuri pia na kufanya korambo na wasanii wan je lengo
ikiwa nikupanua mbawa za kimuziki kuelekea kimataifa zaidi
“Najua watu wengi walikuwa wanatamni na kuona
nafanya kolabo na watu wa nje, niwahakikishie mwaka huu nimeamua kujipanga
kikamilifu kuanzia video, niko siliasi na muziki sababu nimeona unalipa sana
hivyo washabiki wangu wategemee muziki muzuri” aliongeza
Hata hivyo msanii huyo anampango wa kuanzisha
biashara ambayo ni moja ya ndoto katika maisha yake kuachilia mbali na muziki
ambao anafanya.
“Nampango
wa kuanzisha biashara nyingi nitafungua kampuni mbili tatu za kibiashara
nitaajiri watu wengi ili kuhakikisha tunafika mbali kimaendeleo” alisema Nandy
Nandy aliwahi kuwa na skendo za video zake ambazo
hazikuwa na maadili kusambaa mtandaoni kitende ambacho siyo heshima kama msanii
ambaye ni kioo cha jamii