Arsenal watamlenga mshambuliaji mwingine watakapokamilisha
dili la kumsaini kiungo wa kati wa Uhispania Mikel Merino, 28, kutoka Real
Sociedad. (Mirror)
Leicester City wako kwenye mazungumzo ya kumsajili kiungo wa
kati wa Morocco Bilal El Khannouss, huku Genk ikitaka angalau pauni milioni 17
kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (HITC)
Kiungo wa kati wa Chelsea Tino Anjorin, 22, amekubali kwa
mdomo kujiunga na Empoli inayoshiriki Ligi ya Serie A, huku mchezaji huyo wa
zamani wa kimataifa wa Uingereza akihama kwa uhamisho wa bila malipo. (Fabrizio
Romano)
Kipa wa Brazil Alisson, 31, yuko tayari kusaini mkataba mpya
na Liverpool baada ya kukataa ofa kutoka Saudi Arabia, lakini Reds wamemtambua
mrithi wake wa muda mrefu, mlinda lango wa Georgia Giorgi Mamadashvili, 23.
(Telegraph - subscription required)
Mshambuliaji wa Brazil Vinicius Jr, 24, atasubiri hadi mwisho
wa msimu huu kabla ya kufanya uamuzi wa kuhamia Saudi Arabia. (ESPN)
Real Sociedad wako kwenye mazungumzo ya mwisho mwisho ya
kumsajili beki wa zamani wa Ujerumani Mats Hummels, 35, ambaye yuko kama
mchezaji huru baada ya kuondoka Borussia Dortmund mwishoni mwa msimu uliopita.
(Athletic - subscription required)
Mshambulizi wa Everton Neal Maupay, 28, anafuatilia kwa karibu kurejea nchini kwao Ufaransa na klabu ya Nice ya Ligue 1. (Nice-Matin - in French)