Mwanamuziki wa Bongo Fleva Ay anasema kuwa licha ya
kuwa na majukumu mengi ya kimaisha lakini suala la kimuziki na taratibu zote za kuhakikisha unasongo mbele
kwa kiasi kikubwa kwa sababu ni moja ya kazi ambayo muda wote anaifikilia
kichwani kwaajili ya kufikia lengo kubwa zaidi la maisha kupitiia kazi hiyo.
Aidha msanii huyo alienda mbali zaidi kwa kueleza
jinsi anavyotekeleza majukumu yake ya kimuziki licha yakuwepo na changamoto kwa
maana kazi yeyote haiwezi kukosa
vizingiti ambavyo ni chazo cha kukushusha kuelekea mafanikio.
“Mara nyigi katika utaratibu wangu ni lazima nifanye
kitu baada ya wiki moja au mbili kwa sababu naamini muziki ni kama
mpira,riadha, kitu ambacho kinahitaji mazoezi ya kila wakati sababu ukikaa bila
kufanya chochote unaweza kudumaa kimuziki” alisema Ay.
Kuachilia na hilo Alisema kuwa anafurahi kuona kuwa baadhi ya wafanya
biashara kuwekeza katika muziki kitu ambacho ni faida kubwa sana kwa msanii sababu inaongeza zaidi thamani ya
kubwa katika kuufikisha muziki huo mbali
“Hata hivyo napenda
baadhi ya wafanyabiashara wameanza kugudua kuwa wanaweza kuwekeza kwa
msanii kama sehemu ya kuinua biashara katika hatua nyingine vilevile nachoamini
ni kitu kimoja kuwa msanii siyo mfanya biashara ila msanii ni biashara” aliongeza
Kwahiyo ni wakati sasa ambapo msanii kusimama katika
kazi yake kwa ajili ya kuutunza utamaduni wake na nchi kiujumla.