Na Mwandishi Wetu.
Kiungulia (kwa Kiingereza heartburn) ni hali ya kusikia maumivu makali katika koo la chakula.
Maumivu hayo yanatokana na kupanda kwa asidi iliyomo tumboni (asidi haidrokloriki = HCl) inayofanya kazi ya kuua vijidudu vinavyoingia tumboni kwa njia ya chakula na maji. Mara nyingi kiungulia hutokea baada ya tumbo kujaa gesi
Kiungulia kinaweza kuwa na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kula kwa pupa au kupita kiasi, matumizi ya dawa za kulevya, ujauzito, tumbo kujaa gesi, vidonda vya tumbo.
Namna ya kuzuia kiungulia
Kiungulia kinaweza kuzuiwa kwa namna mbalimbali. Zifuatazo ni baadhi ya njia za kuzuia kiungulia:
Epuka kulala mara tu badaa ya kula chakula.
Epuka kula kupita kiasi.
Epuka kula vitu kama maharagwe, mboga za sukuma n.k.
Epuka vinywaji vyenye asidi kwa wingi, mfano: soda n.k.
EEpuka matumizi ya dawa za kulevya.
Matibabu ya asili ya
kiungulia
1.Apple cider vinegar
Apple cider vinegar au siki ya matunda ya apple inasaidia kurekebisha utindikali kwenye tumbo na hivo kupunguza acid ya tumboni. Nenda supermaket au sokoni tafuta apple vinagar yenye sifa hiziOrganic
Unfiltered
With the mother
2.Baking soda
Baking soda ni moja ya bidhaa ingine inayopatikana kwa urahisi itakayokutibu kiungulia chako. Kumbuka tu kwamba kuna tofauti kati ya baking soda na baking powder. Ukienda dukani au supermaket ulizia baking soda.
3.Juisi ya Aloe vera
Aloe vera ni moja ya mimea adhimu sana kutokea kwani inatibu magonjwa mengi. Hakikisha unapata juisi salama ambayo haijawekwa kemikali mbaya. Mmea wa aloe vera ni mchungu sana, kabla hujaanza kutumia tafuta kwanza kwenye maduka ya tiba asili kama utapata juisi ya aloe vera iliyopunguzwa makali.
Matumizi ya aloe vera kutibu kiungulia
Kutibu kiungulia kunywa robo kikombe cha juisi ya aloe vera kila siku asubuhi kabla hujala chochote. Endapo utakosa juisi, unaweza pia kutafuta vidonge vya aloe vera vitakufaa sana kutibu kiungulia.
4.Tangawizi
Tangawizi moja ya dawa asili kabisa ya kutibu maumivu ya mwili. Pia tangawizi ni nzuri kwa kuuimarisha usagaji wa chakula tumboni na kuzuia asidi ya tumbo kupanda juu. Tangawizi pia inazuia athari ya bakteria wabaa tumboni.
Matumizi ya tangawizi kwa kiungulia
Kutibu kiungulia, tengeneza chai ta tangawizi na unywe baada tu ya kumaliza kula.
5.Binzari nyembamba(Cumin)
Moja ya tiba ingine makini sana ya kiungulia inayopatikana jikoni kwako ni binzari nyembamba ambayo hutumika sana kwenye kupika pilau. Gesi inapojaa tumboni inaweza kusababisha kiungulia pia. Kutumia binzari nyembamba itakusaidia kuondoa gesi tumboni a hivo kuepusha kiungulia.
Matumizi ya binzari nyembamba
Chukua kijiko kimoja cha bidhaa nyembamba chemsha pamoja na maji nusu lita kisha kunywa mara tatu kwa siku baada ya mlo wako.
6.Tui la nazi
Utashangaa kwamba kiungo hichi ambacho umekuwa ukitumia kila siku kupika wali na maharage, kinaweza kutibu changamoto yako ya kiungulia pasipo kumeza dawa.
Matumizi
Baada ya kukuna nazi yako, weka machicha ya nazi kwenye sufuria, sagia na tangawizi kidogo pamoja na maji lita moja kisha chemsha kwa dakika 5 epua. Chuja tui lako kisha kunywa glass moja asubuhi na jioni kabla ya kula.
NB: Kumbuka wataalamu wa Afya wanashauri kwamba wakati wa kulala ni vyema utumie mto.