Na kalebo mussa, Dar Es
Salaam
Tangawizi ni mmea kati
ya mimea mingi yenye maajabu ,mmea huu unaweza kutumika kama dawa na kutibu magonjwa
mengi tu zaidi ya 72 yaliyo ndani ya miili yetu na kutuacha tukiwa wazima na
kutekeleza majukumu yetu ya kila siku
Mmea huu unaweza
kuonekanika kama mmea wa kawaida na watu kutumia kama mazoea lakini kiungo hiki
kinaweza kutumiwa kama dawa , kiungo hiki huweza kutumika kikiwa kibichi au kikavu kimekaushwa na kutengenezwa unga,
Vilevile tangawizi maranyingi hutumika katika nyanja mbalimbali , kiungo katika
mboga, dawa ya kutibu kikohozi, na matumizi
mengine vilevile unashauriwa ili kuwa na afya bora kila wakati tumia chai ya tangawizi kwa wingi ili uweze
kujikinga na kutibu magojwa mabalimbali.
a zakeFaida
Huondoa harufu mbaya ya
kinywa,
Tofauti na vyakula
vingine kama kitunguu swaumu, tangawizi husaidia uwe na harufu nzuri pale
unapopumua na kufanya maeneo ya kinywa chako kuwa safi
Tangawizi husaidia
msukumo wa damu kuwa mzuri,
Tangawizi husaidia
msukumo wa damu mwili kuwa vivzuri hii ni kwa sababu huupa mwili joto la
kutosha pindi unapokunywa chai ya tangawizi ambapo mwili huhitaji wakati wa
usukumaji wa damu mwilini
Huondoa magonjwa ya
asubuhi,
Tanagawizi licha ya
kuwa ni tiba ya magonjwa kama kikohozi na mafuta mwilini, tangawizi pia
husaidia kupunguza magonjwa ya asubuhi kama uchovu na mninginio, kwa akina mama
hasa wajawazito tangawizi huwapunguzia homa za asubuhi pindi wanapoamka , pia
hutumika kama kichocheo cha utulivu.
Tangawizi husaidia
mfumo wa chakula mwilini
Tangawizi husaidia
mwili kunyonya virutubisho kwenye chakula hii husaidiana sana pale unapoamua
kupunguza uzito wa mwili na kupata virutubisho vilivyo muhimu tu.
Tangawizi hurekebisha
sukari ya mwlii
Husaidia katika kuweka
sawa kiwango cha sukari kwenye damu, hapa wagonjwa wa kisukari wanashauriwa
kutumia tangawizi badala ya chai,
Tangawizi huongeza hamu
ya kula
Huongeza hamu ya kula
chakula kwa wale wenye mfumo mbaya wa umeng’enyaji wa chakula wanashauriwa
kutumia tangawizi ili kupata mfumo mzuri wa mmeng’enyo wa chakula
Tangawizi husaidia
kuyeyusha mafuta mwilini
Tangawizi husaidia
kupunguza kuganda kwa mafuta mwilini ambayo yana madhara makubwa mwilini hasa
magonjwa ya kiharusi na shinikizo la damu
Tangawizi husaidia
kuondoa sumu mwilini
Tangawizi husaidia
kuondoa kichefuchefu na kutapika pia huwasaidi sana wale watu waliotumia sana
madawa na kuwa sumu nyingi mwilini
Tangawuzi husaidia
kutibu vidonda vya tumbo
Tangawizi pia husaidia
mtu mwenye vidonda vya tumbo kwa kupunguza maumivu na hata kuponya vidonda
hivyo kama vitakuwa katika hatua ya awali.
Tanagawizi ina
kiinilishe muhimu sana ambacho huzuia kuongezeka kwa seli za kansa ya kongosho
kiitwacho kwa kitaalamu (gingerol) vilevile hutibu kansa zinazoweza
kusababishwa na kupata choo kigumu muda mrefu kwa kitaalamu (constipation
related cancer)
Huzuia kuzalishwa kwa
bacteria aitwaye (helicobacter pylori)
bacteria huyu ndiye anayesababisha vidonda vya tumbo mwilini pia hutibu
kiungulia na kaza mbali mbali za tumbo pia husaidia katika kutibu kansa ya
titi,
Pia tangawizi husaidia
kutibu kansa za kwenye kizazi na kansa za kwenye mirija ya uzazi, husaidia
kuzuia shambulio la moyo, huzuia damu kuganda, hushusha kiwango cha
kolesto,husafisha damu , husaidia watu wenye kukamaa mishipa , hutibu maumivu
ya tumbo hasa wakati wa hedhi, huimarisha afya ya figo
Ina madini ya manganese
ambayo ni muhimu kuongeza mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali,
hulinda kuta za moyo, hulinda mishipa ya damu na mishipa ambako mikojo hupita .
tangawizi inakitu kiitwacho (silicon) ambacho cheyewe kazi yake hasa ni
kuongeza afya ya ngozi, nywele,meno na kucha pia husaidia umengenyaji wa madini
ya calcium
Tangawizi ina vitamin
A, C, E, B complex, chuma,zinki, magnesium, phosphorus, sodium, calcium, na
beta carotene.
Unaweza kujitibu
magonjwa mbalimbali kwa kutumia zao hili la tangawizi kwa kufuata maelekezo
yafuatayo
Kwa wale wenye kuumwa
jino na maumivu ya kichwa, unashauriwa kuchukua tangawizi ya unga koroga na
maji kidogo iwe nzito kama tope kisha jipake na uchue kwenye paji lako la uso kabla ya kulala, kwa jino jipake na uchue
kwenye shavu
Kwa wenye maumivu makali ya tumbo unashauriwa kuwa
changanya kijiko kimoja au viwili vya tangawizi iliyosangwa na kijiko kimoja au
viwili vya mafuta ya kastoroli kisha kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku
Kujitibu tatizo la
kuvimbiwa nakukosa hamu ya kula, unashauriwa kuchangaya juice ya tangawizi ,
juice ya limao na chumvi mawe kwa vipimo vilivyo sawa hakikisha umechanganya
vizuri kunywa dawa hiyo kabla ya kula chakula au changanya vipimo vilivyo sawa
sawa vya juice ya tangawizi na sukari ya mawe , koroga vizuri kunywa kabala ya
kula chakula. Dawa hii husafisha ulumi na koo na hukuongezea hamu ya kula na
kukufanya mchangamfu.
Kujitibu maumivu ya
kukoo na kukauka sauti unashauriwa
kutafuana vipande vidogo vya tangawizi vilevile kujitibu tatizo la
kuharisha unashauriwa kuchua sehemu
zinazozunguka kitovu kwa juice ya tangawizi
Kwa wale wanaosumbuliwa
na kichefuchefu na kutapika kunywa mchanganyiko wa juice ya tangawizi na juice
ya kituguu.
Ukiwa na maumivu ya
kichwa cha wasiwasi , unashauriwa kuchanganya juice ya tangawizi na maziwa, kisha kausha nusa unga huo kama tumbaku.
Maumivu makali ya
tumbo, changanya kijiko kimoja cha au viwili vya tangawizi iliyosagwa na kijiko
kimoja au viwili vya mafuta ya kastoroli kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa
siku
Kwa wale wanaojisikia
baridi bisi sugu unashauriwa kuchanganya kijiko kimoja cha tangawizi ya unga na
vijiko 24 vya maji kunywa mchanganyiko huo ukiwa vuguvugu ,ulale na ujifunike
mpaka utoe jasho.
Mmea huu unafanan sana
na binzali ikiwa bado haijamenywa maganda yake na kwa hapa Tanzania tangawizi
hulimwa sana katika mikoa ya nyanda za juu kusini na baadhi ya mikoa ya kama
Kilimanjaro, manayara, morogoro na kwingineko nchini.