JE RONALDO NI MFUNGAJI BORA 2023?.
Cristiano Ronaldo anatazamiwa kumaliza mwaka akiwa mfungaji bora wa soka duniani kwa 2023 baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa 4-1 wa Al-Nassr dhidi ya Al-Taawoun Jumamosi.
Fowadi huyo amefurahia kipindi cha mafanikio nchini Saudi Arabia baada ya kujiunga na ligi hiyo akitokea Manchester United mwezi Januari, na kuisaidia timu yake kuendeleza harakati za kuwania ubingwa dhidi ya Al-Hilal.
Magoli yake mawili dhidi ya Al-Taawoun yalimfanya afikishe mabao 54 kwa mwaka, likiwemo soka la kimataifa, huku zikiwa zimesalia timu chache tu kucheza kabla ya mwaka wa kalenda kuisha.
Ronaldo alikuwa akiwafuata Kylian Mbappe na Harry Kane kabla ya kufikia december 26,2023 ambapo Mbappe anacheza, na Bundesliga.
Wote Kane na Mbappe watamaliza mwaka wakiwa na mabao 52, huku mabao ya hivi karibuni ya Ronaldo yakimfanya aonekane mbele akiwa na mabao 54.