FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM
Showing posts with label burudani. Show all posts
Showing posts with label burudani. Show all posts

ZUCHU AVUNJA UKIMYA KUHUSU DIAMOND PLATNUMZ

 

                          Msanii wa Bongo Fleva Zuchu kutoka katika lebo ya Wasafi WCB.



Na Kalebo Mussa.


Msanii wa Bongo Fleva kutoka katika lebo ya Wasafi WCB  Zuhura  Othumani 'Zuchu' amevunja uvumi wa kutoka kimapenz na bosi wake Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz. 

 Akizungumza leo katika mahojiano na Wasafi Fm alisema kuwa yeye na bosi wake  Diamond Platnumz hawapo katika mahusiano ya kimapenzi kama watu wanavyotofsiri.

 Alisema huenda maneno au uvumi huo unatoka na ukaribu alionao wa kikazi na bosi wake, kwani mara nyingi amekuwa karibu naye kwaajili ya kumpa maelekezo ya kazi yake ya mziki.

 "Mimi na Bosi wangu hatopo kwenye mahusiano kama watu wanavyotofsiri yeye ni bosi ataendelea kuwa bosi" alisema Zuchu.

 Uvumi huu umekuja mara baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kuwa wawili hao wanamahusiano ya kimapenzi na wameshavalishana Pete ya uchumba.

 


RIHANNA ATUPILIA MBALI KESI DHIDI YA BABA YAKE


 

 Na Mwandishi wetu.

Mwanamuziki Rihanna ametupilia mbali kesi dhidi ya baba yake, wiki chache kabla ya siku waliopaswa kukutana mahakamani.

Nyota huyo wa muziki aina ya pop alikuwa amemshtaki baba yake, Ronald Fenty, kwa kutumia jina lake vibaya kunufaisha kampuni yake ya burudani, na alimshtaki mnamo mwaka 2019 kwa matangazo ya uwongo na kuingilia maisha yake kwa hali iliyokiuka haki zake za kuwa na siri

Alisema pia kwamba alijaribu kumsajili katika safari yake ya nje ya nchi bila ruhusa.

Kesi hiyo ilitakiwa kuanza kusikilizwa mnamo Septemba 22, lakini Rihanna aliwasilisha ombi la kuitupilia mbali kesi hiyo Jumanne.

Hakuna sababu iliyotolewa, lakini ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zinaonyesha kwamba walifikia makubaliano ya kutatua mzozo wao nje ya mahakama na baba yake na mwenza wake wa kibiashara.

Rihanna, ambaye jina lake kamili ni Robyn Rihanna Fenty, alifungua kesi miaka miwili iliyopita, akisema: "Ingawa Bwana Fenty ni baba wa Rihanna, hana, na hajawahi kuwa na mamlaka ya kuchukua hatua kwa niaba ya Rihanna."

Alidai kuwa mnamo mwaka 2017, baba yake na mtu mwingine, Moses Perkins, waliunda kampuni inayoitwa Fenty Entertainment, ambayo ilidai mara kwa mara kuwa inahusiana na Rihanna.

Katika nyaraka za mahakamani, mawakili wake walisema: "Bwana Fenty na Bwana Perkins wametumia uwongo huu katika juhudi za kulaghai mamilioni ya madola kutoka kwa watu wengine kwa mabadilishano ya ahadi za uwongo kwamba wameidhinishwa kuchukua hatua kwa niaba ya Rihanna."

Walidai kuwa kampuni ya Fenty Entertainment ilijaribu kusajili safari ya tarehe 15 Marekani Kusini yenye thamani ya $ 15m (£ 11m), na vile vile maonyesho huko Los Angeles na Las Vegas, bila Rihanna kujua.

Kwa kuongezea, walidai kwamba Ronald Fenty alikuwa akijaribu kufaidika na utambulisho wa nembo ya kibiashara ya "Fenty", ambayo Rihanna ameitumia kwa biashara zake kadhaa ikiwa ni pamoja na ile ya vipodozi ya mamilioni ya fedha, Fenty Beauty

Baba yake hapo awali alijaribu kuanzisha nembo yake ya kibiashara kwa kutumia jina Fenty, kama sehemu ya mpango wa kufungua msururu wa hoteli ambazo mtu pia anaweza kufanya manunuzi, alidai.

Hata hivyo, ofisi inayosimamia hataza na nembo za kibiashara Marekani ilikataa ombi hilo.

Akiomba kutolewa kwa agizo la kumzuia baba yake na mwenzi wake wa kibiashara kuchukua hatua hiyo, Rihanna alisema shughuli zake za biashara zilikiuka matangazo, ushindani na sheria za faragha na pia kulihatarisha "jeraha kubwa lisiloweza kutibiwa" kwa kmpuni ya Fenty ikiwa hatua hiyo haitasimamishwa.

Mwimbaji huyo, ambaye ni miongoni mwa wanamuziki tajiri duniani, kwa muda mrefu amekuwa na uhusiano mbaya na baba yake, ambaye awali, aliwahi kupambana na uraibu wa pombe na dawa za kulevya.

Hakuna kati ya wawili hao aliyepatikana mara moja kutoa maoni yake juu ya kutupiliwa mbali kwa kesi hiyo ya kisheria.

SAMAKIBA FOUNDATION WATAMBIANA KIBABE


Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ali Salehe ‘Alikiba’ amefunguka kuwa Team Kiba hawatakubali tena kufungwa na Team Samatta katika mechi ya hisani ya SamaKiba Foundation ambao unakwenda kupigwa Uwanja wa Taifa Dar, Agosti 8, mwaka huu.

King Kiba amesema walikuwa na bahati mbaya katika misimu miwili iliyopita na kujikuta wakifungwa katika mechi zote mbili, licha ya kuwa kikosi chao kilikuwa bora zaidi ya kile cha Team Samatta, hivyo awamu hii ni ni zamu yao kuwapa raha mashabiki wa TeamKiba.

Mchezo huo wa SamaKiba Foundation ulianzishwa kwa kuunganisha nguvu kati ya nahodha wa Taifa Stars na nyota wa Aston Villa ya England, Mbwana Samatta na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba kwa lengo la kukusanya fedha na kuzisaidia jamii za watu wa hali ya chini.

Mbwana Samatta tayari ameshatangaza timu ya watu watano ambao ni Mohamed Samatta, Idd Seleman ‘Nado’, Farid Mussa na Juma Kaseja na msemaji wake ni Haji Manara, ambaye ni Ofi sa Habari wa klabu ya Simba.

Huku wasanii wake wawili wa Kings Music, K2ga na mdogo wake Abdu Kiba wakitajwa kuwa sehemu ya kikosi hicho.

Matokeo yaliyopita yalikuwa hivi, msimu wa kwanza ambao ulikuwa ni Juni Mosi, 2018, Team Samatta 3-1 TeamKiba, huku msimu wa pili uliofanyika Juni 11 mwaka jana, Team Kiba walifungwa 6-3.

Hivyo sasa wapenzi wa michezo wawe tayali kupata burudani ya kipekee katika siku hiyo maalumu.


ZUCHU AMKUNA LADY JAYDEE

Msanii wa Bongo Fleva, Judithi Wambura ‘Lady Jaydee’ amesema kuwa msanii mpya wa Lebo ya Wasafi Classic, Zuchu atafika mbali kutokana na juhudi zake.

Lady Jaydee amesema kuwa Zuchu amekuwa na juhudi ya kutaka kukutana na watu waliotangulia ili kujifunza na hicho ndicho kitamfikisha mbali.

“Zuchu ana juhudi za kuwa karibu na watu waliomtangulia kwenye gemu, hii itamfanya kufika mbali zaidi na anajitahidi hata kwenye kazi zake.

Pia amesema kuwa kama sisi zamani tulikuwa tunawaongelea wanamuziki kama mama yake mzazi (Malkia Khadija Kopa), hiyo ni nzuri sana,’’. alisema Lady Jaydee.


TAKEOFF AKABILIWA NA TUHUMA NZITO

Mwanamke mmoja huko Jijini Los Angels nchini Marekani amemshitaki Rapa anaeunda kundi la Migos , Kirshnik Khari Ball ‘Takeoff’ kuwa alimbaka walipokua kwenye Party mjini humo huku akisisitiza kuwa ana ushahidi kutoka Hospitali .

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ , mwanamke huyo amesema kuwa Takeoff alimlazimisha kuwa karibu nae Chumba cha mtu aliyemualika katika Party hiyo .



HUMPHREY POLEPOLE AMKINGIA KIFUA TID


Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM), Humphrey Polepole amemkingia kifua msanii wa Bongo Fleva, Khalid Salum Mohamed ‘TID’ mara baada ya

kutumia msemo wake wa ‘Ni Yeye’ na chama pinzani bila ruksa kutoka kwake.

Humphery amesema kuwa kwa kitendo kilichofanywa kwa msanii huyo siyo haki kabisa kwani walipaswa kukubaliana kabla ya kutumia msemo huo.  

“Nampa pole TID sababu hawa majamaa ni mazulumati wametudhulumu wimbo wa Taifa. TID anapambana mtu wa watu ametengeneza Ni Yeye na ile ilikuwa Magufuli, wale majamaa wameichomeka kule. Hawajamshirikisha hawajamuomba kwa kweli sisi kama Watanzania tutawachukulia hatua” Humphrey Polepole alisema.

Aidha Polepole ameshangazwa na waliobadilisha wimbo wa Taifa kwa kuogeza ubeti watatu kwa manufaa yao bila kujua kuwa ni kinyume na sheria

“Nchi hii inatambulishwa ulimwenguni kwa vitu vikubwa vitatu, Moja kwa jina lake ambayo inaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pili ni Bendera yetu, na kitu cha tatu kinachotutambulisha ni Wimbo wetu wa Taifa bila ya kujali tofauti zetu hapo juzi wenzetu wamebadilisha maneno ya wimbo wa taifa wameweka ya chama chao, najiuliza mbona sisi CCM tuna nyimbo nyingi nzuri lakini tunaheshimu huu mmoja hatuwezi kuunajisi kwa kuweka maneno binafsi."  Polepole alisema.


MADEE ATOA WAZO KWA WASANII WENZAKE


Mara baada ya msanii wa Bongo Fleva, Herry Samir ‘Mr Blue’ kuanguka jukwaani wakati anatumbuiza katika tamasha la nyama Choma, Madee ameibuka na wazo la kuwataka wasanii kukata bima za maisha.

Madee kupitia ukurasa wake wake wa Twitter aliandika ujumbe huo ambapo alimpa pole msanii huyo na kisha kutoa wazo la kukata bima za maisha na siyo kuishia kuwa na bima za magari kwa kuogopa matraffic

"Nimeona video Herry Samir Mr blue ameanguka jukwaani, natoa pole kwa niaba ya wanamuziki wote, Mungu akusimamie urudi tena kazini

"Ifike muda sasa wasanii mjikatie bima za maisha yenu, msikimbilie kukata bima za magari kisa unaogopa kukamatwa na traffic, hizi ajali za majukwaani zimekua nyingi siku hizi, hela uliolipwa unaenda kujitibia ni wazo tu" aliandika Madee Madee.

Suala la kuanguka kwa wasanii wakati wakitumbuiza katika majukwaa limekuwa likitokea sana madhara H. Baba, Gig Money ni moja ya wahanga na wengine.


Hata hivyo rapa huyo mpaka sasa anaendelea vizuri toka apate ajali hiyo Mungu aendelee kumlinda dhidi ya mjanga hayo.



MENINAH ACHAFUA HALI YA HEWA


Mashabiki wamechukizwa na tabia ya muigizaji wa filamu Bongo, Meninah Attick baada ya kuposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anafanyiwa masaji na mwanaume.




Kategori

Kategori