IKIWA ni takribani muhongo mmoja tokea msanii wa Bongo Fleva
Rasheed Makwiro, Chiddy Benz kutambulika katika tasnia ya muziki wa Bongo
Fleva, staa huyo amefunguka kujaribu kete yake katika biashara ikiwa alikuwa
akifanya muziki kama biashara japo si biashara rasmi.
Akipiga stori na LAJIJI kwa njia ya simu Chiddy amesema kwa
sasa anajikita katika baishara ya uuzaji wa mkaa. Yawezekana Chidd amefanya
tafiti ya kutosha na kuja na biashara hiyo kwani mjini zipo fursa nyingi lakini
yeye amechangua kuja na aina hiyo ya biashara.
“Mimi ni mwana Dar es
Salaam, najua wana Dar es salaam wanahitaji nini, nimekulia Ilala pale najua
jambo linalohitajika kwa kiasi kikubwa kwa matumizi, wasanii wengi wanafungua
maduka ya nguo. Kuvaa siku hizi ni chaguo tu wala sio lazima. Kwanza wajanja
wote wanatafuta hela wala sio ishu za kuvaa vaa” alisema Chiddy
Watanzania wanampuuzia msanii huyo kwa kudhani huwenda ni
athari za matumizi ya dawa za kulevya ndiyo
yanamuendesha kiasi cha kuwa hivyo, LAJIJI limezungumza naye na kubaini kuwa
jamaa anajielewa na anaelewa nini anafanya.
Ikumbukwe Chiddy Benzy amewahi kutiwa nguvuni mara kadhaa jijini
Dra es Salaam na mikoa ya jirani kwa
makosa mbalimbali ikiwemo kudaiwa kukutwa na dawa za kulevya.