WATU 13 wameuwawa na wengine hawajulikani walipo kwenye jimbo la Maluku
Kaskazini mwa Indonesia baada ya mafuriko makubwa kulikumba eneo la mashariki
mwa visiwa hivyo.
Shirika la
utafutaji na uokoaji la Indonesia Basarnas lilisema kwamba mvua kubwa ilionyesha
tangu jana Jumamosi ilisababisha mafuriko makubwa katika kisiwa cha Ternate na
kwamba kikosi cha uokoaji bado kinaendeleza juhudi za kuwaondoa waathiriwa.
Vyombo vya habari nchini
humo viliripoti kwamba watu 11
wamefariki kufuatia mkasa huo lakini afisa wa shirika la
Basarnas hakuthibitisha idadi hiyo ya vifo.
Itakumbukwa kuwa mnamo
mwezi Mei takriban watu 60 waliuwawa kutokana na mafuriko na maporomoko ya
matope katika mkoa wa Sumatra magharibi mwa Indonesia.