Mwanamume
aliweka maiti ya mama yake ndani ya chumba cha chini kwa zaidi ya mwaka mmoja
wakati akiendelea kupokea malipo yake ya pensheni, polisi wa Austria wanasema.
Mwanamke
huyo wa miaka 89, ambaye inasemekana alikuwa na ugonjwa wa shida ya
akili-dementia anadhaniwa kufa kwa sababu za kawaida mnamo Juni mwaka jana.
Mwanawe,
mwenye umri wa miaka 66, anasemekana kuweka mwili wake ndani ya sanduku na
kutumia vifurushi vya barafu na bandeji kuzuia harufu hiyo.
Polisi
wanaamini anaweza kuwa amepokea malipo kinyume cha sheria ya karibu € 50,000 (£
42,000).
Ulaghai wake
uligunduliwa tu baada ya tarishi mpya aliyekuwa amewasilisha mafao ya mwanamke
huyo katika mkoa wa magharibi wa Tyrol kuzuiwa kumwona, polisi ilisema katika
taarifa.
Hilo
lilisababisha uchunguzi, na kupelekea ugunduzi wa kilichofanyika baadaye .
Polisi
wanasema kuwa mtu huyo hakuwa na mapato mengine, na alikuwa amewaambia kuwa
malipo yangekoma mara moja ikiwa angetoa habari za kifo cha mamake
Mshukiwa pia
alisema alikuwa amemwambia kaka yake kwamba mama yao alikuwa akipatiwa huduma
hospitalini, na kwamba haikustahili kumtembelea kwani hali yake ilimaanisha
haingewezekana kumtambua, iliripoti ORF.
Mapenzi
ni moja ya mahitaji muhimu ya wanadamu, kila mmoja wetu ahahitaji kupenda na
kupendwa, hapo hamna majadiliano ndio jinsi tulivyoumbwa. Katika enzi za mababu
zetu, watu walikuwa wanaishi kwa raha, amani na upendo japokuwa walikuwa
wanachagulia wake au waume wa kuishi pamoja kama mke na mume, enzi hizo
zimepitwa na wakati siku hizi watu wanajitafutia wenza wao wenyewe, ila siku
hizi watu ndio hawana amani, ndoa zinavunjika kila siku na wanaobakia kuteseka
zaidi ni watoto ambao wanaishia kuishi bila mama na baba.
Ukweli
ni kwamba inachukua muda mrefu kumfahamu mtu vizuri, kikubwa zaidi watu
wanabadilika jinsi wanavyokuwa, hela zinaongezeka au kupungua na wanajikuta
wanavutiwa na watu wa aina tofauti. Kwa wale ambao hawajabahatika kupata wenza
wao kuna mambo ya msingi ya kuzingatia kabla hujajizamisha katika dimbwi la
mapenzi, ukizingatia mambo haya, hata kama mtu uliyenaye atabadilika ,
uwezekano wa kuvumiliana na kuweza kuishi pamoja ni mkubwa zaidi.
1.ni
lengo (ambition),
kama
mmoja kati wa wapenzi (nazungumzia wapenzi ambao wanampango wa kuishi pamoja
kama mke na mume) ni mtu wa kuwa na malengo na anataka kufanya kitu fulani au
kuwa mtu fulani katika maisha yake na mwenzake anachukulia siku kama inavyokuja
(laid back), huyu ambaye ana malengo atamchukulia ambaye ni “laid back” kama ni
mvivu. Wapenzi wanatakiwa wasipishane sana katika malengo yao hata kama wana
kazi mbali mbali.
2.ni
uwazi (openness),
kama
mpenzi wako ni “open minded” anapenda kujifunza vitu tofauti, kujaribu vyakula
tofauti, kusafiri n.k. Yule ambaye anapenda kujifunza mambo mapya kila siku
atamuona mwenzake anaboa.
3.wapenzi
wanaweza kuwa tofauti katika ujuzi wa hisia (emotional intelligence).
Hapa
kama tofauti sio kubwa, watu wanaweza kuvumiliana na kuishi pamoja, ila kama
tofauti ni kubwa sana, yule ambaye hana ujuzi wa hisia, atakuwa anamburuza na
kumharibia mudi yule ambaye amesimama imara kwenye mambo ya hisia. Onyo kwa
wanaume ambao wana ujuzi au utaalam wa kusoma hisia za wanawake, wanawake ambao
wana F katika ujuzi wa hisia huwa wanavutiwa sana na watu kama ninyi.
4.ni
usosho,
kama
mmoja wenu ni mtu wa watu anapenda kuongea na watu na anamarafiki kibao,
utamkwaza ambae ni mtu ambaye anapenda maisha “private” na ya utulivu. Mwenzako
atakuwa bize anaweka picha zenu na status zinazowahusu facebook wakati wewe
unataka mambo ya ndani yawe ya ndani tu. Kama tofauti si kubwa sana mnaweza
vumiliana kama tofauti ni kubwa, muda si mrefu mtashindwana
5.ni
wivu.
Wivu
ni kitu kibaya sana, kama mpenzi mmoja ana wivu ni ngumu kuekewana na ambaye
hana wivu. Kama wote mna wivu, sawa kwani kila mmoja ataepuka kufanya mambo
ambayo yanamuumiza mwenzake, ila kama mmoja ndio ana wivu ataona mwenzake
hajali, basi ukimuona mwenzako anaongea na classmate wake wa zamani au ukiona
mtu amepiga picha na mpenzi wako ameshikwa bega basi inakuwa fujo tupu. Kama
upo tayari kwenye uhusiano, na mwenzako ana wivu, jaribu kumuelewesha kwamba
kum-kumbatia rafiki yako sio kwamba ndio una mipango mingine ya siri.
Kikubwa
katika yote ni uaminifu, kama hamna uaminifu katika mapenzi au ndoa. Usipasue
kichwa, ondoka na tafuta mtu ambaye anakuamini au kama haupo tayari kuwa
mwaminifu usijiingize katika mahusiano, utajiumiza mwenyewe na mwenzako. Msome
mwenzako kabla ya kuanza kuitana wachumba, kama tangu siku ya kwanza mwenzako
ana wasiwasi na wewe ukikaribia simu yake, ni afadhali umuulize mapema,
kulikoni? Kama umepoteza uaminifu katika mahusiano yako, usihofu, muonyeshe
mweza wako kwamba umebadilika na jinsi muda unavyoenda atajifunza kukuamini
tena.
Hizi
sifa zilizotajwa hapo juu sio za kina sana, lakini ni moja wapo ya mambo ya
kuzingatia katika kuchagua mwenza wako wa maisha(kama basi mapenzi yana macho)
kabla ya kujizamisha katika mapenzi. Je wewe unaona ni mambo gani ya kuzingatia
katika mahusiano na ni mambo gani yanasababisha ndoa kuvunjika? Usisite
kuandika maoni yako.
Alana Nesbitt anahisi kama ni kisu kilichomo ndani yake, lakini kifaa hiki kiliwekwa na daktari. Alana ni mmoja wa wanawake kadhaa ambao maisha yao yamegeuka na kuwa magumu baada ya kupandikiziwa kifaa cha Coil ndani ya mirija ya inayokutanisha mbegu ya kiume na yai la uzazi kwa ajili ya utungwaji wa mimba.
Kifaa hicho kinachofahamika kwa lugha ya kitalaamu kama Essure coil implant kimetengenezwa mahsusi kwa ajili ya kuzuwia mayai ya uzazi kuingia katika mfuko wa uzazi.
Kifaa hicho kiliondolewa kwenye soko la Uingereza mnamo mwaka 2017. Watengenezaji wa kifaa hiki , Bayer Healthcare Pharmaceuticals, walisema kuwa uamuzi wa kukiondoa kwenye maduka ya dawa na hospitali ulikuwa ni ”wa kibiashara”
Kufikia mwezi Januari mwaka huu ,uuzaji na usamabazaji wa kifaa cha Essure ulipigwa marufuku nchini Marekani, baada ya masharti makali ya matumizi yake kuwekwa na taasisi ya Marekani ya Chakula na utoaji wa dawa (FDA).
Hata hihvyo , watoaji w ahuduma za afya bado wanaweza kupandikiza kifaa cha Essure Coil kwa kipindi cha hadi mwaka mmoja tangu kiliponunuliwa.
Awali zilizuwiwa kutumiwa, kwani wanawake wengi walipata maumivu makali na wengi hadi sasa bado wanaumia kutokana na Coil.
Alana Nesbitt, mwenye umri wa miaka 39, kutoka magharibi wa Belfast, anasema unapowekewa kifaa hicho cha kupandikizwa “unahisi kama una kisu ndani yako -ni kibaya sana”.
Bi Nesbitt ambaye ni mama wa watoto wawili anasema kuwa ,maumivu yalianza miezi michache baada ya kupandikiziwa coil mnamo mwaka 2012.
Mwanzo alikwenda kwa daktari akiwa anashuku maumivu ya kidole tumbo(appendix), lakini baadae ilibidi aagizwe kumuona daktari bingwa wa magonjwa ya uzazi kwa ajili ya matibabu.
Kwa sasa anasubiri kufanyiwa upasuaji wa kuondoa kifaa hicho.
“Kusema ukweli ni vigumu kuishi nacho ,”aliiambia BBC.
” Unakua ukifikiri kuwa hatimae utafikia umri wa ukomo wa uzazi, lakini hujui utakayoyapitia kabla ya muda huo.
“Nilifahamu kuwa ninataka kupewa kinga ya ujauzito, lakini sikufahamu nitapata maumivu ya kiasi gani. Natamani kungekuwa na taarifa na utafiti unaotolewa wakati mtu anapotaka kupata huduma hii
“Badala yake nilishauliwa niamini kuwa ni upasuaji wa haraka utakaochukua dakika 10 tu ninaoweza kufanyiwa wakati wa chakula cha mchana, na kukamilika na hiyo ndiyo taarifa tu niliyopata .”
Amy Speers, mama wa watoto wanne kutoka eneo la Bangor, County Down,pia anasubiri upasuaji wa kuondolewa kwa Assure Coil mwilini mwake.
Alipandikiziwa Essure imwaka 2014, baada ya kuamua kuwa familia yake imekamilika.
“Ni sawa na uchungu wa kujifungua, mara nne zaidi, wote kwa wakati mmoja ,” alisema mama wa miaka 33.
“Maumivu huwa yanaongezeka unapoinama chini, wakati mwingine ukitembea unachechemea kutokana na maumivu makali .”
Vifaa vidogo huingizwa katika mirija ya fallopian ambamo husababisha majeraha, kusababisha kovu ambalo baadaye huvimba na kuziba mirija ya fallopian hali ambayo hujulikana kama hysteroscopic sterilisation.
“Maumivu unayoyapata ni kama unadungwa kisu kwa ndani, kupigwa na umeme, au kama una ujauzito usio na mimba – Nisingependa mtu yeyote apitie” Bi Speers aliiambia BBC News.
“Linakuwa ni jambo la siri, na kufunikwa chini ya zulia, lakini kupandikiziwa kifaa cha kuzuwia ujauzito – sterilisation ni kitu kibaya nilichowahi kukifanya . Afya yangu ya akili ni kama ilishuka chooni .”
Kumekuwa na matukio machache ya ripoti za wagonjwa wa Ireland kaskazini , kulingana na msemaji wa Wizara ya Afya ya Irleand Kaskazini.
Wizara ya Afya nchini humo inasema iliwashauri maafisa wa afya na huduma za kijamii kuwa Essure hilipoteza kibali cha matumizi yake mwaka 2017 na kuomba vifaa vilivyobakia visitumiwe.
Lakini Bayer Healthcare Pharmaceuticals, kampuni inayohtengeneza vifaa hivyo, imeiambia BBC News kwamba wanawake ambao bado wanavifaa hivyo mwilini mwao wanaweza kuendelea kuvitegemea kwa kuzuwia ujauzito.
Kelly George, kutoka eneo la County Down, aliwekewa kifaa cha Essure mwaka 2014, baada ya kuzaliwa kwa mtoto wake mdogo wa kiume. Kuanzia wakati huo alianza kupata upele anaposhika vifaa vilivyotengenezwa kwa madini ya aina ya Nikel ambayo hutumika kutengeneza kifaa cha Essure
“Nilikuwa sawa mwanzo, lakini baadae nikaanza kutokwa na jasho usiku na baada ya wiki chache ngozi yangu ikaanza kubabuka ,” aliiambia BBC News NI.
“Pia nimekuwa sijisikii vizuri tu – Niko katika sayari nyingine na kabla sikuwa hivi . Ni moja ya dalili ambazo watu wengi wamekuwa wakilalamikia kuhusu kifaa hiki .”
Bi George alifanyiwa upasuaji wa kuondoa mirija ya fallopian tubes mwezi wa Novemba na akafanyiwa upasuaji wa kuondoa kifaa Ijumaa iliyopita. “Kimeathiri vibaya maisha yangu .”