Muigizaji wa Bongo Movie Irene Paul amewaasa Mastaa wenzake kuacha kujichumbua na wabaki
katika uhalisia wake kwani licha ya kupata madhara makubwa baadaye pia hugharimu gharama kubwa ambapo matokea
yake ni hatari kiafya.
Msanii huyo alijitolea mfano kwake yeye kwa
kuonekana na rangi yake kuwa asili na yakuvutia na kusema kuwa ni gharama ndogo
sana ambayo anatumia kwa kununua vitu vya kawaida ambavyo vinaonesha ngozi yake
kuwa asili kila siku.
Ukitaka kuniangalia kuanzia kichwani hadi ngozi
yangu situmii gharama hata kidogo, naamini mastaa wengine wakiamua kuwa jinsi
walivyo watapendeza na wataepuka gharama ambazo si za muhimu“ alisema Irene
Paulo
Hata hivyo msanii huyo anasema kuwa mastaa hao wamekuwa
wakijichubua kwa kutafuta kuoneka kuwa na mvuto na kupendeza lakini wengi wao hawako hivyo licha yakutaka
kuonekana hivyo kunamadhara makubwa sana
Wakati msanii huyo akiwataka mastaa kutojichumbua
msanii wa muziki
Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ alikaliliwa na
wanazengo kuwa anajichumbua kitendo ambacho amekanusha na kusema siyo kweli.
“Jamani mimi hizo
tabia nimezianza lini tena? Yaani walimwengu hawakosagi cha kusema, unajua kuna
picha ambazo zikitupiwa mtandaoni naonekana mweupe sana na nyingine zinakuwa zimetoka
vibaya, hapo watu ndiyo huanza kusema nimejichibua, kitu ambacho siyo kweli,”
alisema Rayvanny.
LAJIJI halikuishia
hapo lilifanya utafiti zaidi ili kujua madhara makubwa yatokanayo na
kujichumbua kwa kutumia vipondozi ambavyo ni hatali kwa afya .
Katika bidhaa zinazotumika kujichubua, kuna kemikali za aina
mbili. Ambayo ni ‘Hydroquinone’ na ‘Mercury’
Hydroquinone kemikali hii ni sumu kali, ambayo hutumika kwa ajili ya kuchapisha
picha na kutengeneza bidhaa za mpira. pia kama kisaidizi katika kutengeneza
rangi za nywele. Mercury nayo ni kemikali ya sumu inayoweza kuuzwa katika
maduka ya madawa
Dkt. Elizabeth Kilili, ni mtaalamu na
Mkurugenzi Mtendaji wa Grace Product Limited ambaye ameainisha madhara
yatokanayo na matumizi ya vipodozi maarufu kama kujichumbua kitendo ambacho ni
hatali sana.
“Kujijumbua kunahatali kubwa sana ikiwa
ni pamoja na kupata kansa ya ngozi, kuzeeka mapema,kupata watoto wenye
kasoro, mishipa ya fahamu,figo, kupungua kwa uzito na kupelekea athari za
kuvunjika mifupa.Madhara haya huoneka mara moja na kadri mtu anavyozidi kutumia
mkorogo kung'arisha ngozi yake.
Dkt Kilili anaendelea kwa kutoa
ushauri wa kuepukana na madhara ya kujichubua huku akishauri matumizi ya bidhaa
za asili zisizokuwa na madhara, ikiwemo kutumia vipodozi vilivyopitishwa na
Mamalaka ya Chakula na Dawa (TFDA) pamoja na kupata ushauri kwa wataalamu juu
ya afya na magonjwa ya vipodozi ikiwemo kujikinga na madhara yanayoweza
kusambabisha athari katika mwili wako.
Ukweli ni kwamba wapo mastaa wengi
ambao wanajichumbua kitendeo ambacho kinasababisha baadhi ya jamii kuiga kwa
kuona muonekano ambao si halisi hivyo kuna hitaji kwa namna moja au nyingine
kila mmoja kujitasumini na kuacha kabsa kwani ni hatali sana
Lady Gaga aweka histori kushinda tuzo
za Oscar 2109
Kupitia tuzo kubwa duniani za Filamu
za Oscar 2019 ambazo zilifanyika Los Angeles Marekani, ambapo ilihusihwa na utowaji wa tuzo
kwa washindi mbalimbali mwanamuziki nchini humo Lady Gaga ameweka historia ya
kipekee katika maisha yake.
Gaga ameibukuka
kidedea na kujinyakulia ushindi ambao umempa tuzo ya kipekee kuwa msanii bora
kupitia wimbo wake uitwao ‘Shallow’ na hii ikiwa ni mara ya kwanza kwake tangu
tuzo hizo zianzishwe.
Lady Gaga anaingia
kwenye orodha ya wasanii wa muziki ambao walishawahi kushinda tuzo hizo, kama
Cher, Jennifer Hudson, The Beatles, Prince, Elton John, Adele na wengine
kitendo ambacho kinaleta hamasa kubwa ya kuzidi kufanya vizuri katika muziki
Utoaji wa tuzo kwa
washindi ambao kwa namna moja au nyingine wanafanya vizuri katika kazi yao ya
kimuziki ni moja ya msanii husika kumpa uwezo wa kufikilia zaidi kwa kufanya
muziki ambao ni bora na wenye kufuata taratibu husika
Hata hivyo kupitia
tuzo hizo kwa upande mwingine Washirika wawili katika filamu ya ‘Black Panther’
ambao ni Ruth Carter na Hannah Beachler alishinda tuzo ya ubunifu wa
filamu kwa pamoja na mshindi mwingine Jay Hart.
wameweka historia katika tuzo hizo kwa kuibuka washindi wa kwanza weusi
katika vitengo walivyoshinda.
“Huenda Marvel
imeunda shujaa wa kwanza mtu mweusi lakini kwa kutumia mavazi ya ubunifu
tulimgeuza kuwa mfalme wa Afrika.” Alisema Hannah Beachler
Tukiachilia mbali na
tuzo hizo zilizotolewa nchini humo Tanzania kupitia Bodi ya Filamu na Sinema Zetu
International Film Festival Award (SZIFF) 2019 ilitoa tuzo kwa washindi
mbalimbali kama vile mwanamuziki bora, muingizaji bora, mchekeshaji bora, na nyingine ambapo wahusika walipewa tuzo
maalumu ambazo ni moja ya historia katika maisha yao.