FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

Alikiba: Sababu ya SEDUCE ME kugonga ngoma za viongozi wa kisiasa




Msanii wa muziki Bongo, Alikiba bila ya hofu aamuakufunguka na kuweka hadharani sababu iliyo pelekea ngoma yake ya ‘Seduce Me’ kupokelewa vizuri hadi kugusa viongozi mbali mbali wa kisiasa.
Alikiba wakati akiwa katika katika mahojiano ya kipindi cha Dj Show Radio One aslisema kuwa utakapo fanya muziki mzuri kilamtu ataukubali na kuupenda haijalishi ni mtu warika gani waa anacheo gani.
“Muziki mzuri ukitoa kila mtu anaukubali haijalishi kwamba huyo ni kiongozi au mheshimiwa watu wanasikiliza muziki kwa sababu ni sehemu ya maisha yao,” ameiambia Dj Show ya Radio One na kuongeza.
“Nimefurahi sana kwa kweli na jinsi muziki umetanuka na kufika mbali. Inaniongezea nguvu ya kufanya kazi nzuri ambayo nahisi itaizidi kuipeleka Tanzania yetu mbele kutangaza lugha ya Kiswahili,” amesisitiza.
Ngoma ya Seduce Me ilitoka August 25 mwaka huu na hadi sasa ina views milioni 4.6 katika mtandao wa YouTube.