Familia ya marehemu Samson Petro ambaye anahusika na matukio ya kuteka watoto imesema haitofanya matanga wala kuufuata mwili wa marehemu kutokana na kitendo cha ukatili alichokifanya cha kuwateka watoto ovyo na kuwatumbukiza kwenye shimo la karo watoto wawili akidai apatiwe fedha.
Hayo yalizungumzwa na Petro Aaron, ambaye ni baba mzazi wa marehemu Samson mbele ya wanafamilia wengine akiwepo mama mzazi wa marehemu huyo, amesema kitendo kilichofanywa na marehemu si kitendo cha kusameheka wala kusahaulika katika jamii.
Aidha kamanda wa polisi mkoani Arusha , Charles Mkumbo ameeleza kuwa mtuhumiwa alikufa baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi mbili miguuni alipokuwa akijaribu kutoroka mikononi mwa polisi waliokuwa wamemshikilia kwa kosa la utekaji na mauaji ya watoto wawili ambaye ni Moureen Njau na Ikhram Salim aliokuwa amewatumbukiza kwenye karo baada ya wazazi wao kuto mlipa fedha ili kuwaachia huru watoto hao.
‘’ Mtuhumiwa alijaribu kutoroka, ndipo polisi walipolazimika kumjeruhi miguu yote miwili na kukimbizwa hopsitali ya Mkoa Mount Meru akibubujikwa na damu ndipo alipofariki dunia.