Mahakama ya kadhi ya Wilaya ya Mfenesini imemuamuru kwenda Rumande kwa muda wa wiki moja mtuhumiwa Makame Jumbe Makame mwenye umri wa miaka 22 mkaazi wa Bumbwini Kitoroni baada ya kushidwa kutekeleza amri halali aliyopewa na Mahakama hiyo kwa kosa la kushindwa kulipa mahari ya mkewe ya Sh/= 1,000,000.
Kwamujibu wa maelezo aliyoyatoa mtuhumiwa mahakamani hapo kwamba, mtuhumiwa huyo alikiri kosa hilo na hatimae Mahakama ilimuamuru aanze kulipa fedha hizo kidogo kidodo kwa muda wa miezi sita ziwe zimesha kamilika.
Siku yamwanzo aliyopangiwa kulipa pesa hizo mtuhumiwa huyo alifika Mahakamani hapo na kuanza kulipa elfu kumi na tano kitendo ambacho Mahakama haikuridhia na ndipo Mahakama ilipomuamuru mtuhumiwa kwenda rumande hadi tarehe 20 Septemba ili iwe fundisho kwake.