FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM
Showing posts with label burudani. Show all posts
Showing posts with label burudani. Show all posts

ZUCHU AVUNJA UKIMYA KUHUSU DIAMOND PLATNUMZ

 

                          Msanii wa Bongo Fleva Zuchu kutoka katika lebo ya Wasafi WCB.



Na Kalebo Mussa.


Msanii wa Bongo Fleva kutoka katika lebo ya Wasafi WCB  Zuhura  Othumani 'Zuchu' amevunja uvumi wa kutoka kimapenz na bosi wake Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platnumz. 

 Akizungumza leo katika mahojiano na Wasafi Fm alisema kuwa yeye na bosi wake  Diamond Platnumz hawapo katika mahusiano ya kimapenzi kama watu wanavyotofsiri.

 Alisema huenda maneno au uvumi huo unatoka na ukaribu alionao wa kikazi na bosi wake, kwani mara nyingi amekuwa karibu naye kwaajili ya kumpa maelekezo ya kazi yake ya mziki.

 "Mimi na Bosi wangu hatopo kwenye mahusiano kama watu wanavyotofsiri yeye ni bosi ataendelea kuwa bosi" alisema Zuchu.

 Uvumi huu umekuja mara baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kuwa wawili hao wanamahusiano ya kimapenzi na wameshavalishana Pete ya uchumba.

 


RIHANNA ATUPILIA MBALI KESI DHIDI YA BABA YAKE


 

 Na Mwandishi wetu.

Mwanamuziki Rihanna ametupilia mbali kesi dhidi ya baba yake, wiki chache kabla ya siku waliopaswa kukutana mahakamani.

Nyota huyo wa muziki aina ya pop alikuwa amemshtaki baba yake, Ronald Fenty, kwa kutumia jina lake vibaya kunufaisha kampuni yake ya burudani, na alimshtaki mnamo mwaka 2019 kwa matangazo ya uwongo na kuingilia maisha yake kwa hali iliyokiuka haki zake za kuwa na siri

Alisema pia kwamba alijaribu kumsajili katika safari yake ya nje ya nchi bila ruhusa.

Kesi hiyo ilitakiwa kuanza kusikilizwa mnamo Septemba 22, lakini Rihanna aliwasilisha ombi la kuitupilia mbali kesi hiyo Jumanne.

Hakuna sababu iliyotolewa, lakini ripoti za vyombo vya habari vya Marekani zinaonyesha kwamba walifikia makubaliano ya kutatua mzozo wao nje ya mahakama na baba yake na mwenza wake wa kibiashara.

Rihanna, ambaye jina lake kamili ni Robyn Rihanna Fenty, alifungua kesi miaka miwili iliyopita, akisema: "Ingawa Bwana Fenty ni baba wa Rihanna, hana, na hajawahi kuwa na mamlaka ya kuchukua hatua kwa niaba ya Rihanna."

Alidai kuwa mnamo mwaka 2017, baba yake na mtu mwingine, Moses Perkins, waliunda kampuni inayoitwa Fenty Entertainment, ambayo ilidai mara kwa mara kuwa inahusiana na Rihanna.

Katika nyaraka za mahakamani, mawakili wake walisema: "Bwana Fenty na Bwana Perkins wametumia uwongo huu katika juhudi za kulaghai mamilioni ya madola kutoka kwa watu wengine kwa mabadilishano ya ahadi za uwongo kwamba wameidhinishwa kuchukua hatua kwa niaba ya Rihanna."

Walidai kuwa kampuni ya Fenty Entertainment ilijaribu kusajili safari ya tarehe 15 Marekani Kusini yenye thamani ya $ 15m (£ 11m), na vile vile maonyesho huko Los Angeles na Las Vegas, bila Rihanna kujua.

Kwa kuongezea, walidai kwamba Ronald Fenty alikuwa akijaribu kufaidika na utambulisho wa nembo ya kibiashara ya "Fenty", ambayo Rihanna ameitumia kwa biashara zake kadhaa ikiwa ni pamoja na ile ya vipodozi ya mamilioni ya fedha, Fenty Beauty

Baba yake hapo awali alijaribu kuanzisha nembo yake ya kibiashara kwa kutumia jina Fenty, kama sehemu ya mpango wa kufungua msururu wa hoteli ambazo mtu pia anaweza kufanya manunuzi, alidai.

Hata hivyo, ofisi inayosimamia hataza na nembo za kibiashara Marekani ilikataa ombi hilo.

Akiomba kutolewa kwa agizo la kumzuia baba yake na mwenzi wake wa kibiashara kuchukua hatua hiyo, Rihanna alisema shughuli zake za biashara zilikiuka matangazo, ushindani na sheria za faragha na pia kulihatarisha "jeraha kubwa lisiloweza kutibiwa" kwa kmpuni ya Fenty ikiwa hatua hiyo haitasimamishwa.

Mwimbaji huyo, ambaye ni miongoni mwa wanamuziki tajiri duniani, kwa muda mrefu amekuwa na uhusiano mbaya na baba yake, ambaye awali, aliwahi kupambana na uraibu wa pombe na dawa za kulevya.

Hakuna kati ya wawili hao aliyepatikana mara moja kutoa maoni yake juu ya kutupiliwa mbali kwa kesi hiyo ya kisheria.

SAMAKIBA FOUNDATION WATAMBIANA KIBABE


Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ali Salehe ‘Alikiba’ amefunguka kuwa Team Kiba hawatakubali tena kufungwa na Team Samatta katika mechi ya hisani ya SamaKiba Foundation ambao unakwenda kupigwa Uwanja wa Taifa Dar, Agosti 8, mwaka huu.

King Kiba amesema walikuwa na bahati mbaya katika misimu miwili iliyopita na kujikuta wakifungwa katika mechi zote mbili, licha ya kuwa kikosi chao kilikuwa bora zaidi ya kile cha Team Samatta, hivyo awamu hii ni ni zamu yao kuwapa raha mashabiki wa TeamKiba.

Mchezo huo wa SamaKiba Foundation ulianzishwa kwa kuunganisha nguvu kati ya nahodha wa Taifa Stars na nyota wa Aston Villa ya England, Mbwana Samatta na msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Alikiba kwa lengo la kukusanya fedha na kuzisaidia jamii za watu wa hali ya chini.

Mbwana Samatta tayari ameshatangaza timu ya watu watano ambao ni Mohamed Samatta, Idd Seleman ‘Nado’, Farid Mussa na Juma Kaseja na msemaji wake ni Haji Manara, ambaye ni Ofi sa Habari wa klabu ya Simba.

Huku wasanii wake wawili wa Kings Music, K2ga na mdogo wake Abdu Kiba wakitajwa kuwa sehemu ya kikosi hicho.

Matokeo yaliyopita yalikuwa hivi, msimu wa kwanza ambao ulikuwa ni Juni Mosi, 2018, Team Samatta 3-1 TeamKiba, huku msimu wa pili uliofanyika Juni 11 mwaka jana, Team Kiba walifungwa 6-3.

Hivyo sasa wapenzi wa michezo wawe tayali kupata burudani ya kipekee katika siku hiyo maalumu.


ZUCHU AMKUNA LADY JAYDEE

Msanii wa Bongo Fleva, Judithi Wambura ‘Lady Jaydee’ amesema kuwa msanii mpya wa Lebo ya Wasafi Classic, Zuchu atafika mbali kutokana na juhudi zake.

Lady Jaydee amesema kuwa Zuchu amekuwa na juhudi ya kutaka kukutana na watu waliotangulia ili kujifunza na hicho ndicho kitamfikisha mbali.

“Zuchu ana juhudi za kuwa karibu na watu waliomtangulia kwenye gemu, hii itamfanya kufika mbali zaidi na anajitahidi hata kwenye kazi zake.

Pia amesema kuwa kama sisi zamani tulikuwa tunawaongelea wanamuziki kama mama yake mzazi (Malkia Khadija Kopa), hiyo ni nzuri sana,’’. alisema Lady Jaydee.


TAKEOFF AKABILIWA NA TUHUMA NZITO

Mwanamke mmoja huko Jijini Los Angels nchini Marekani amemshitaki Rapa anaeunda kundi la Migos , Kirshnik Khari Ball ‘Takeoff’ kuwa alimbaka walipokua kwenye Party mjini humo huku akisisitiza kuwa ana ushahidi kutoka Hospitali .

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ , mwanamke huyo amesema kuwa Takeoff alimlazimisha kuwa karibu nae Chumba cha mtu aliyemualika katika Party hiyo .



HUMPHREY POLEPOLE AMKINGIA KIFUA TID


Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM), Humphrey Polepole amemkingia kifua msanii wa Bongo Fleva, Khalid Salum Mohamed ‘TID’ mara baada ya

kutumia msemo wake wa ‘Ni Yeye’ na chama pinzani bila ruksa kutoka kwake.

Humphery amesema kuwa kwa kitendo kilichofanywa kwa msanii huyo siyo haki kabisa kwani walipaswa kukubaliana kabla ya kutumia msemo huo.  

“Nampa pole TID sababu hawa majamaa ni mazulumati wametudhulumu wimbo wa Taifa. TID anapambana mtu wa watu ametengeneza Ni Yeye na ile ilikuwa Magufuli, wale majamaa wameichomeka kule. Hawajamshirikisha hawajamuomba kwa kweli sisi kama Watanzania tutawachukulia hatua” Humphrey Polepole alisema.

Aidha Polepole ameshangazwa na waliobadilisha wimbo wa Taifa kwa kuogeza ubeti watatu kwa manufaa yao bila kujua kuwa ni kinyume na sheria

“Nchi hii inatambulishwa ulimwenguni kwa vitu vikubwa vitatu, Moja kwa jina lake ambayo inaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pili ni Bendera yetu, na kitu cha tatu kinachotutambulisha ni Wimbo wetu wa Taifa bila ya kujali tofauti zetu hapo juzi wenzetu wamebadilisha maneno ya wimbo wa taifa wameweka ya chama chao, najiuliza mbona sisi CCM tuna nyimbo nyingi nzuri lakini tunaheshimu huu mmoja hatuwezi kuunajisi kwa kuweka maneno binafsi."  Polepole alisema.


MADEE ATOA WAZO KWA WASANII WENZAKE


Mara baada ya msanii wa Bongo Fleva, Herry Samir ‘Mr Blue’ kuanguka jukwaani wakati anatumbuiza katika tamasha la nyama Choma, Madee ameibuka na wazo la kuwataka wasanii kukata bima za maisha.

Madee kupitia ukurasa wake wake wa Twitter aliandika ujumbe huo ambapo alimpa pole msanii huyo na kisha kutoa wazo la kukata bima za maisha na siyo kuishia kuwa na bima za magari kwa kuogopa matraffic

"Nimeona video Herry Samir Mr blue ameanguka jukwaani, natoa pole kwa niaba ya wanamuziki wote, Mungu akusimamie urudi tena kazini

"Ifike muda sasa wasanii mjikatie bima za maisha yenu, msikimbilie kukata bima za magari kisa unaogopa kukamatwa na traffic, hizi ajali za majukwaani zimekua nyingi siku hizi, hela uliolipwa unaenda kujitibia ni wazo tu" aliandika Madee Madee.

Suala la kuanguka kwa wasanii wakati wakitumbuiza katika majukwaa limekuwa likitokea sana madhara H. Baba, Gig Money ni moja ya wahanga na wengine.


Hata hivyo rapa huyo mpaka sasa anaendelea vizuri toka apate ajali hiyo Mungu aendelee kumlinda dhidi ya mjanga hayo.



MENINAH ACHAFUA HALI YA HEWA


Mashabiki wamechukizwa na tabia ya muigizaji wa filamu Bongo, Meninah Attick baada ya kuposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anafanyiwa masaji na mwanaume.




NYIMBO ZA DIAMOND, ALI KIBA ZINASAIDIA KUENEZA KISWAHILI, KAZI YA KULINDA AMANI DRC




Nchini ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC,  lugha ya Kiswahili imekuwa nyenzo muhimu katika kutekeleza majukumu ya ulinzi wa amani ya Umoja wa Mataifa, ikitumiwa na walinda amani wa chombo hicho hususan wale wanaotoka Tanzania,  sambamba na raia.

Mashuhuda wa Kiswahili na ulinzi wa amani ni walinda amani wa Tanzania wa kikundi cha 7, TANZBATT 7, cha kikosi cha kujibu mashambulizi, FIB cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO.

Meja Michael Kibira ni miongoni mwao mjini Beni jimboni la Kivu Kaskazini na anasema kuwa, "lugha ya kiswahili imekuwa ikiongelewa katika eneo hili la Kivu kaskazini na raia wengi kuanzia wadogo ni lugha yao ambayo wanakua nayo.

“Na sisi tunaitumia kama ni faida kwetu kwa sababu unapokuwa unakutana na raia wa DR Congo unakuwa uko huru kuongea naye, naye anakuamini.
“Unajua katika maeneo ya vita, yule ambaye ni mwaathirika wa vita anakuwa ni mtu ambaye anatilia shaka kila mtu ambaye ni mgeni kwake.

“Hapa DR Congo tumekuwa tukifanya kazi na mataifa mbalimbali kuna Malawi, Afrika Kusini na Indonesia."
Mlinda amani huyu kutoka Tanzania anatoa mfano zaidi akisema kuwa,  "kwa mfano hapa ninafanya kazi na mtu kutoka Indonesia,
“kwa hivyo wakikutana na mtu ambaye ni raia wa Indonesia  ni tofauti kabisa na wanavyokutana na sisi kwasababu wanapokutana na mimi wanakuta kwamba sihitaji kuwa na yule msaidizi wa lugha.

“Mimi, ana uwezo wa kunisongelea, akaongea na mimi ni kama ndugu moja na anatambua kabisa kwamba nyinyi Tanzania ni ndugu zetu tunaongea lugha moja,
“tunafahamiana hata kama lugha yangu mimi wa DRC haijanyooka kama Kiswahili chenu lakini  tunaelewana vizuri.

“Kwa hivyo mimi hapa Kamango nimeitumia kama silaha ambapo naweza nikaambiwa kitu kama akiona adui anakwambia kule rafiki usiende kuna hii na hii kwa hivyo mimi nasema hiyo ni silaha na msaaada mkubwa sana kwetu watanzania kufanya kazi hapa Congo!"
Kwa upande wake Kepteni Salum Lihega, lugha ya Kiswahili inafanikisha doria kama akifafanua kuwa, "lugha ya Kiswahili imetoa msaada mkubwa sana kwetu kwasababu imeleta urahisi sana katika kuwafikia raia na kufanya nao mazungumzo mbalimbali.

“Lugha ya Kiswahili imeenea na hii imepelekea kutuletea urahisi sana sisi katika kuwafikia raia kuzungumza nao kupata taarifa mbalimbali na pia sisi kujenga nao mahusiano yaliyo karibu.

“Kuna suala moja ambalo kwa kweli naomba nilizungumze nitoe pongezi zangu za dhati kwa wasanii wetu wa Tanzania waimbaji wa nyimbo za injili na vile vile hata waimbaji wa hizi nyimbo za kizazi kipya nao wamechangia sana katika kueneza hii lugha ya Kiswahili katika nchi hii.

“Utasikia nyimbo za  injili kama vile za Rose  Mhando, na  Christina Shusho na vile vile za kizazi kipya kama vile za Diamond Platnumz na Ali kiba. Sasa hivi nikipita huko mitaani huona sisi tunapita kuzungumza nao na hasa hasa wakizisikiliza zile nyimbo na kutuona sisi wanaona kwamba sisi ndio wale ambao tumekuwa tukiziimba zile nyimbo.
“Kwa kweli imeleta faraja sana kwa watanzania tujidai kuwa na kiswahili tujivunie, tukitetee Kiswahili tukilinde na tujitahidi kukikuza ili kiweze kuenea  sehemu mbalimbali ukiacha hapa DRC."

Kinasaidia kupata taarifa kutoka kwa  tunaowalinda
Walinda amani hao kutoka Tanzania wanaendelea kuelezea ni kwa vipi wakiwa wanasaka taarifa za ulinzi wa amani, lugha ya Kiswahili ni nyenzo muhimu ambapo Luteni Godfrey Mzungu anasema kuwa,
"Niko huku katika ulinzi wa amani katika kuongoza doria mbalimbali kwa maeneo ya DRC na nimekuwa katika hili jukumu kwa maeneo ya Beni, Mavivi lakini pia nimekuwepo katika majukumu katika sehemu moja inatwa Matombo.

“Mfano mzuri, mimi katika eneo la Sake katika doria zangu najitahidi kukutana na raia wengi tunaongea lugha vizuri ni tofauti kati ya majirani wenzetu ambao wapo katika hili jukumu inaleta shida sana katika kuwasiliana na raia, inafikia kipindi mpaka wawe na mtu anayetafsiri.

“Lakini sisi raia wanatueleza shida zao mbalimbali tunakutana na machifu wao wanatufikishia habari mbalimbali ambazo zinasaidia kabisaa katika utendaji kazi wetu."
Kwa upande wake Sajini Nassoro Mohammed anasema kuwa , "Kiswahili kimetusaidia sana kwa ndugu zetu wacongo kuleta umoja katika DR Congo, kwa hiyo tunasaidia sana na wanapenda sana tuongee Kiswahili na wanapenda sana lugha yetu ya Kiswahili kwamba kumbe lugha ya Kiswahili ni nzuri kuliko hata lugha yao, wanasema lugha yao ni ngumu kuliko kiswahili kwa vile ni rahisi sana.
“Sisi kimetusaidia kuliko mataifa mengine tuliyonayo kama Bangladesh, ndugu zetu wa Malawi au Afrika Kusini.

“Kwa hiyo sisi wanatupenda sana hata maeneo tuliyopo sasa tunafanya kazi kwa karibu hapa tulipo kwa vile tuko

karibu, tukitoka tu nje tunakutana nao kwa hiyo Kiswahili kinasaidia sana."
Je raia wanasemaje?  Augustine ni mkazi wa Goma jimboni Kivu Kaskazini na anakiri kuwa Kiswahili kinawaunganisha na Watanzania akisema, "Kiswahili kinatusaidia sisi wanacongo na Watanzania.
“Ni lugha ya dunia nzima na ndio maana nasema ni lugha ya amani Afrika Mashariki kwa vile sisi sote tunaongea lugha moja.

“Mimi nitachanganya na kifaransa watanzania wanasema wanaongea Kiswahili sanifu lakini sisi sote tunaelewana katika mazungumzo yetu na kutafuta amani nchini Congo.
“Kiswahili kinaleta mahusiano kama niko hapa na mtu wa Bangladesh hawezi kunielewa lakini mtu wa kutoka Afrika Mashariki tutaelewana kwa vile sote tunazungumza Kiswahili na pia inaleta amani."





BASATA YATOA RUKSA SHERIA IZINGATIWE



Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), wametoa shukrani za dhati kwa Rais Magufuli kwa kurejesha shughuli za kisanaa kama ilivyokuwa awali, baada ya kuzuiliwa kwa muda kutokana na janga la Corona.

Godfrey Mngereza alisema kuwa, walikuwa wamekaa vikao na wadau wote wa sanaa ili kujadili jinsi gani watafanya shughuli hizo licha ya uwepo wa ugonjwa wa Corona.

"Tayari tulikuwa tumekaa vikao na wadau wote wa sanaa siku ya Mei 28 ili kuangalia ni namna gani ambavyo tunaweza kufanya kazi zetu huku tunaishi na Corona,
tulichukua yale maoni na tukapeleka Wizarani, ndiyo maana Rais mwenyewe alitoa tamko ili kurejesha shughuli za michezo, sanaa na burudani, na sisi kama BASATA tumetoa ruksa, lakini haina maana wasanii wavunje sheria na kanuni" Katibu Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza.

Ikumbukwe kwamba hii imekuja mara baada ya Rais Magufuli kutoa tamko la kuruhusu shughuli zote ziendelee kama kawaida wakati alipokuwa anavunja Bunge la 11 jijini Dodoma june 16.  






YOUNG DEE AFUNGUKA KUHUSU DAWA ZA KULEVYA


Msanii wa Bongo Fleva, David Ganzi ‘Young Dee’ amefunguka namna ambavyo alipitia wakati mgumu wa kutumia dawa za kulevya.

Akiweka wazi jambo hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram Young Dee aliandika kuwa haikuwa rahisi kwa yeye kuondokana na tatizo hilo kwani madaktari walifanya kazi ya ziada sana.

“Kuna muda nikikumbuka baadhi ya mapito yangu huwa naishia kucheka tu (Swipe Left ucheke). Mwaka 2016 nilipambana sana kuachana na hili swala, kwa msaada wa watu wengi. Haikuwa rahisi washkaji zangu, ila Mungu yu nami na alinipigania sana.

Kuna sababu kadhaa zilizopelekea kunisaidia kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya (Hivi karibuni Documentary yangu ikitoka, mtajua namna nilivyoingia kwenye hilo swala). Sababu ya kwanza ilikuwa ni team yangu ya kipindi kile ya MDB. Kusema ukweli hawa watu walipambana sana na jambo langu, nadhani sikupigwa makofi tu ila niliwakwaza sana. Walipambana sana kunitoa huko.

Japo haikuwa rahisi hata kidogo, Sababu ya Pili ni Mh. Baba Keagan na kampeni ya kuzuia madawa. Ile ilikuwa na matokeo chanya sana kwa jamii hasa kwangu mimi. Najua Mh. Makonda alipigwa vita sana kwenye swala lile, na najua wapo ambao hadi leo wanaliona jambo lile lilikaa kisiasa, lakini mimi nina ushuhuda wa namna kampeni ile ilivyonisaidia mimi binafsi, na baadhi ya vijana ninaowafahamu, ambao leo hii tunaendesha maisha yetu na familia zetu baada ya kulazimika kuacha kabisa 

matumizi ya madawa ya kulevya kutokana na shinikizo la serikali.
Wazee, msichokijua ni kwamba kuna siku nilizidisha dozi, nikajiona kabisa nakufa. Siku hiyo nilisali sala mbili, ya kwanza ni ya mwisho, na ya pili ilikuwa ya kumuomba Mungu anivushe ule usiku tu, nami nilimuahidi kuto kurudia tena na shughuli hizo. (Story nyingi mtazipata kwenye Documentary yangu); Baba Keagan kwa namna moja au nyingine najua ulikutana na changamoto kubwa sana wakati wa kampeni ile, 

kwasababu ulipigana vita kubwa sana.
Mimi na familia yangu tuchukue fursa hii kwanza kukupa pole kwa kadhia zote ulizokutana nazo, na pia naomba niseme asante sana kwa kuileta. Imenisaidia sana, huenda leo hii ningekuwa teja kabisa nisiye na thamani machoni mwa watu, lakini kwa nguvu za Mungu, leo naweza kuandika hapa na kushare a positive note kutoka kwenye janga negative kwenye maisha yetu vijana” aliandika Young Dee.
Chidi Benzi, Ray C na wengine ni moja ya mastaa ambao walipitia changamoto ya dawa za kulevya.





HARMONIZE ATIMIZA AHADI YAKE KWA 
LADY JAY DEE


 Msanii wa  Bongo Flave, Abdul Rajabu ‘Harmonize’ baada ya kuitoa hivi karibuni na single aliyoshirikishwa na mwanadada Nandy, mara hii anakuja na  toleo jipya akiwa na msanii mkongwe Lady Jaydee.


Nyimbo hiyo ambayo inaitwa ‘wife’ video yake imeachiwa juzi mashabiki wameifurahia kuwa kali pamoja na mazingira yake ni mazuri.

jana Harmonize ameuposti wimbo huo katika ukurasa wake wa ‘Twitter’ huku akielezea jinsi alivyokuwa na ndoto ya muda mrefu ya kuimba na Lady Jaydee.

“Ilikuwa ndoto yangu ya siku nyingi kufanya kazi na dada yangu kipenzi Jidejaydee trust me i'm big fan of her! nimeanza kumsikia na kumuona tangu nikiwa mtoto finally dream come true brand new clapper boardclapper board wife elephant ft Jidejaydee” aliandika Lady Jaydee.










Kategori

Kategori