Msanii wa Bongo Fleva Zuchu kutoka katika lebo ya Wasafi WCB.
Na Kalebo Mussa.
Msanii wa Bongo Fleva
kutoka katika lebo ya Wasafi WCB Zuhura Othumani 'Zuchu' amevunja
uvumi wa kutoka kimapenz na bosi wake Naseeb Abdul maarufu kama Diamond
Platnumz.
Akizungumza leo katika mahojiano na Wasafi Fm alisema kuwa yeye na bosi wake Diamond
Platnumz hawapo katika mahusiano ya kimapenzi kama watu wanavyotofsiri.
Alisema huenda maneno
au uvumi huo unatoka na ukaribu alionao wa kikazi na bosi wake, kwani mara
nyingi amekuwa karibu naye kwaajili ya kumpa maelekezo ya kazi yake ya mziki.
"Mimi na Bosi
wangu hatopo kwenye mahusiano kama watu wanavyotofsiri yeye ni bosi ataendelea
kuwa bosi" alisema Zuchu.
Uvumi huu umekuja mara
baada ya taarifa kusambaa mitandaoni kuwa wawili hao wanamahusiano ya kimapenzi
na wameshavalishana Pete ya uchumba.