Baraza la
Sanaa Tanzania (BASATA), wametoa shukrani za dhati kwa Rais Magufuli kwa
kurejesha shughuli za kisanaa kama ilivyokuwa awali, baada ya kuzuiliwa kwa
muda kutokana na janga la Corona.
Godfrey
Mngereza alisema kuwa, walikuwa wamekaa vikao na wadau wote wa sanaa ili
kujadili jinsi gani watafanya shughuli hizo licha ya uwepo wa ugonjwa wa
Corona.
"Tayari
tulikuwa tumekaa vikao na wadau wote wa sanaa siku ya Mei 28 ili kuangalia ni
namna gani ambavyo tunaweza kufanya kazi zetu huku tunaishi na Corona,
tulichukua
yale maoni na tukapeleka Wizarani, ndiyo maana Rais mwenyewe alitoa tamko ili
kurejesha shughuli za michezo, sanaa na burudani, na sisi kama BASATA tumetoa
ruksa, lakini haina maana wasanii wavunje sheria na kanuni" Katibu
Mtendaji wa Basata Godfrey Mngereza.
Ikumbukwe kwamba
hii imekuja mara baada ya Rais Magufuli kutoa tamko la kuruhusu shughuli zote
ziendelee kama kawaida wakati alipokuwa anavunja Bunge la 11 jijini Dodoma june
16.
YOUNG DEE
AFUNGUKA KUHUSU DAWA ZA KULEVYA
Msanii wa
Bongo Fleva, David Ganzi
‘Young Dee’ amefunguka namna ambavyo alipitia wakati mgumu wa kutumia dawa za
kulevya.
Akiweka wazi
jambo hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram Young Dee aliandika kuwa haikuwa
rahisi kwa yeye kuondokana na tatizo hilo kwani madaktari walifanya kazi ya
ziada sana.
“Kuna muda
nikikumbuka baadhi ya mapito yangu huwa naishia kucheka tu (Swipe Left ucheke).
Mwaka 2016 nilipambana sana kuachana na hili swala, kwa msaada wa watu wengi.
Haikuwa rahisi washkaji zangu, ila Mungu yu nami na alinipigania sana.
Kuna sababu
kadhaa zilizopelekea kunisaidia kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya (Hivi
karibuni Documentary yangu ikitoka, mtajua namna nilivyoingia kwenye hilo
swala). Sababu ya kwanza ilikuwa ni team yangu ya kipindi kile ya MDB. Kusema
ukweli hawa watu walipambana sana na jambo langu, nadhani sikupigwa makofi tu ila
niliwakwaza sana. Walipambana sana kunitoa huko.
Japo haikuwa
rahisi hata kidogo, Sababu ya Pili ni Mh. Baba Keagan na kampeni ya kuzuia
madawa. Ile ilikuwa na matokeo chanya sana kwa jamii hasa kwangu mimi. Najua
Mh. Makonda alipigwa vita sana kwenye swala lile, na najua wapo ambao hadi leo
wanaliona jambo lile lilikaa kisiasa, lakini mimi nina ushuhuda wa namna
kampeni ile ilivyonisaidia mimi binafsi, na baadhi ya vijana ninaowafahamu,
ambao leo hii tunaendesha maisha yetu na familia zetu baada ya kulazimika
kuacha kabisa
matumizi ya madawa ya kulevya kutokana na shinikizo la serikali.
Wazee,
msichokijua ni kwamba kuna siku nilizidisha dozi, nikajiona kabisa nakufa. Siku
hiyo nilisali sala mbili, ya kwanza ni ya mwisho, na ya pili ilikuwa ya
kumuomba Mungu anivushe ule usiku tu, nami nilimuahidi kuto kurudia tena na
shughuli hizo. (Story nyingi mtazipata kwenye Documentary yangu); Baba Keagan
kwa namna moja au nyingine najua ulikutana na changamoto kubwa sana wakati wa
kampeni ile,
kwasababu ulipigana vita kubwa sana.
Mimi na
familia yangu tuchukue fursa hii kwanza kukupa pole kwa kadhia zote ulizokutana
nazo, na pia naomba niseme asante sana kwa kuileta. Imenisaidia sana, huenda
leo hii ningekuwa teja kabisa nisiye na thamani machoni mwa watu, lakini kwa nguvu
za Mungu, leo naweza kuandika hapa na kushare a positive note kutoka kwenye
janga negative kwenye maisha yetu vijana” aliandika Young Dee.
Chidi Benzi,
Ray C na wengine ni moja ya mastaa ambao walipitia changamoto ya dawa za
kulevya.
HARMONIZE ATIMIZA
AHADI YAKE KWA
LADY JAY DEE
Nyimbo hiyo
ambayo inaitwa ‘wife’ video yake imeachiwa juzi mashabiki wameifurahia kuwa kali
pamoja na mazingira yake ni mazuri.
jana
Harmonize ameuposti wimbo huo katika ukurasa wake wa ‘Twitter’ huku akielezea
jinsi alivyokuwa na ndoto ya muda mrefu ya kuimba na Lady Jaydee.
“Ilikuwa
ndoto yangu ya siku nyingi kufanya kazi na dada yangu kipenzi Jidejaydee trust
me i'm big fan of her! nimeanza kumsikia na kumuona tangu nikiwa mtoto finally
dream come true brand new clapper boardclapper board wife elephant ft Jidejaydee”
aliandika Lady Jaydee.