Katibu wa
Itikadi na Uenezi (CCM), Humphrey Polepole amemkingia kifua msanii wa Bongo
Fleva, Khalid Salum
Mohamed ‘TID’ mara baada ya
kutumia msemo
wake wa ‘Ni Yeye’ na chama pinzani bila ruksa kutoka kwake.
Humphery
amesema kuwa kwa kitendo kilichofanywa kwa msanii huyo siyo haki kabisa kwani
walipaswa kukubaliana kabla ya kutumia msemo huo.
“Nampa pole
TID sababu hawa majamaa ni mazulumati wametudhulumu wimbo wa Taifa. TID
anapambana mtu wa watu ametengeneza Ni Yeye na ile ilikuwa Magufuli, wale
majamaa wameichomeka kule. Hawajamshirikisha hawajamuomba kwa kweli sisi kama
Watanzania tutawachukulia hatua” Humphrey Polepole alisema.
Aidha Polepole
ameshangazwa na waliobadilisha wimbo wa Taifa kwa kuogeza ubeti watatu kwa
manufaa yao bila kujua kuwa ni kinyume na sheria
“Nchi hii
inatambulishwa ulimwenguni kwa vitu vikubwa vitatu, Moja kwa jina lake ambayo
inaitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Pili ni Bendera yetu, na kitu cha tatu
kinachotutambulisha ni Wimbo wetu wa Taifa bila ya kujali tofauti zetu hapo
juzi wenzetu wamebadilisha maneno ya wimbo wa taifa wameweka ya chama chao,
najiuliza mbona sisi CCM tuna nyimbo nyingi nzuri lakini tunaheshimu huu mmoja
hatuwezi kuunajisi kwa kuweka maneno binafsi." Polepole alisema.
MADEE ATOA
WAZO KWA WASANII WENZAKE
Mara baada ya msanii wa Bongo Fleva, Herry Samir ‘Mr Blue’ kuanguka jukwaani wakati anatumbuiza katika tamasha la nyama Choma, Madee ameibuka na wazo la kuwataka wasanii kukata bima za maisha.
Madee kupitia ukurasa wake wake wa Twitter aliandika ujumbe huo ambapo alimpa pole msanii huyo na kisha kutoa wazo la kukata bima za maisha na siyo kuishia kuwa na bima za magari kwa kuogopa matraffic
"Nimeona
video Herry Samir Mr blue ameanguka jukwaani, natoa pole kwa niaba ya
wanamuziki wote, Mungu akusimamie urudi tena kazini
"Ifike
muda sasa wasanii mjikatie bima za maisha yenu, msikimbilie kukata bima za magari
kisa unaogopa kukamatwa na traffic, hizi ajali za majukwaani zimekua nyingi
siku hizi, hela uliolipwa unaenda kujitibia ni wazo tu" aliandika Madee Madee.
Suala la
kuanguka kwa wasanii wakati wakitumbuiza katika majukwaa limekuwa likitokea sana
madhara H. Baba, Gig Money ni moja ya wahanga na wengine.
Hata hivyo rapa huyo mpaka sasa anaendelea vizuri toka apate ajali hiyo Mungu aendelee kumlinda dhidi ya mjanga hayo.
MENINAH
ACHAFUA HALI YA HEWA
Mashabiki
wamechukizwa na tabia ya muigizaji wa filamu Bongo, Meninah Attick baada ya
kuposti video kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa anafanyiwa masaji na
mwanaume.
Meninah
aliposti video hiyo akifanyiwa masaji na mwanaume asiyejulikana, jambo ambalo
liliwakera wafuasi wake waliosema kwamba, anarudia yaleyale ya mwaka jana.
Baadhi ya
wafuasi hao walimshambulia kwa kusema kuwa mambo mengine anajitakia mwenyewe.
“Huyu
mwanamke sijui huwa hajielewi? Anajirekodi mwenyewe video zake halafu anakuwa
wa kwanza kukimbilia Polisi na kuwaletea shida watu wengine,” aliandika mmoja
wa wafuasi wake
Ikumbukwe kwamba
mwaka jana Meninah aliitwa na Baraza la Sanaa Taifa (Basata) kwa kuhusishwa na
kosa la kusambaza video chafu kwenye mitandao ya kijamii, jambo ambalo
lilimuingiza matatani mwigizaji Mwijaku ambaye mpaka sasa ana kesi ya Makosa ya
Mtandao.
SHAMSA FORD
ACHOKA UBACHELA
Msanii wa Bongo Movies na mjasiriamali, Shamsa Ford ameweka wazi mipango yake ya kufunga pingu za maisha na ampendaye kwa sasa.
"Tangu nilipotoka kwa ndoa nimekataa posa 3 kwasababu sikuwa teyali na pia sikutaka kukurupuka kuolewa kwa ajili ya kumfurahisha mtu yoyote au kumkomoa yoyote.ila kwa sasa nipo teyali huyu niliyenaye nahisi atakuwa baba bora kwa mwanangu coz nimeyaona mapenzi yake.2/12/2020 i can't wait " aliandika Shamsa Ford kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Ikumbukwe kwamba Shamsa alikuwa kwenye mahusiano na Chidi Mapenzi na baadae ndoa yao ikavunjika na sasa yupo tayari kuolewa kwa mara nyingine.