Mwanamuziki
wa Bongo Fleva, Ali Salehe ‘Alikiba’ amefunguka kuwa Team Kiba hawatakubali
tena kufungwa na Team Samatta katika mechi ya hisani ya SamaKiba Foundation
ambao unakwenda kupigwa Uwanja wa Taifa Dar, Agosti 8, mwaka huu.
King Kiba
amesema walikuwa na bahati mbaya katika misimu miwili iliyopita na kujikuta
wakifungwa katika mechi zote mbili, licha ya kuwa kikosi chao kilikuwa bora
zaidi ya kile cha Team Samatta, hivyo awamu hii ni ni zamu yao kuwapa raha
mashabiki wa TeamKiba.
Mchezo huo
wa SamaKiba Foundation ulianzishwa kwa kuunganisha nguvu kati ya nahodha wa
Taifa Stars na nyota wa Aston Villa ya England, Mbwana Samatta na msanii wa
muziki wa Bongo Fleva, Alikiba kwa lengo la kukusanya fedha na kuzisaidia jamii
za watu wa hali ya chini.
Mbwana
Samatta tayari ameshatangaza timu ya watu watano ambao ni Mohamed Samatta, Idd
Seleman ‘Nado’, Farid Mussa na Juma Kaseja na msemaji wake ni Haji Manara,
ambaye ni Ofi sa Habari wa klabu ya Simba.
Huku wasanii
wake wawili wa Kings Music, K2ga na mdogo wake Abdu Kiba wakitajwa kuwa sehemu
ya kikosi hicho.
Matokeo
yaliyopita yalikuwa hivi, msimu wa kwanza ambao ulikuwa ni Juni Mosi, 2018,
Team Samatta 3-1 TeamKiba, huku msimu wa pili uliofanyika Juni 11 mwaka jana,
Team Kiba walifungwa 6-3.
Hivyo sasa
wapenzi wa michezo wawe tayali kupata burudani ya kipekee katika siku hiyo
maalumu.
ZUCHU AMKUNA LADY JAYDEE
Msanii wa
Bongo Fleva, Judithi Wambura ‘Lady Jaydee’ amesema kuwa msanii mpya wa Lebo ya
Wasafi Classic, Zuchu atafika mbali kutokana na juhudi zake.
Lady Jaydee
amesema kuwa Zuchu amekuwa na juhudi ya kutaka kukutana na watu waliotangulia
ili kujifunza na hicho ndicho kitamfikisha mbali.
“Zuchu ana
juhudi za kuwa karibu na watu waliomtangulia kwenye gemu, hii itamfanya kufika
mbali zaidi na anajitahidi hata kwenye kazi zake.
Pia amesema
kuwa kama sisi zamani tulikuwa tunawaongelea wanamuziki kama mama yake mzazi
(Malkia Khadija Kopa), hiyo ni nzuri sana,’’. alisema Lady Jaydee.
TAKEOFF
AKABILIWA NA TUHUMA NZITO
Mwanamke mmoja huko Jijini Los Angels nchini Marekani amemshitaki Rapa anaeunda kundi la Migos , Kirshnik Khari Ball ‘Takeoff’ kuwa alimbaka walipokua kwenye Party mjini humo huku akisisitiza kuwa ana ushahidi kutoka Hospitali .
Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ , mwanamke huyo amesema kuwa Takeoff alimlazimisha kuwa karibu nae Chumba cha mtu aliyemualika katika Party hiyo .
Katika
mashitaka hayo Mwanadada huyo anadai kabla ya yote Rapa huyo alimlazimisha
avute Marijuana lakini alikataa na kuamua kukimbilia chumbani kwa mmoja wa marafiki
zake waliomualika ,
lakini ghafla Take Off alimfuata na kumlazimisha
kufanya nae mapenzi .
Mwanamke
huyo anadai alipwe fidia kutokana na kitendo alichomfanyia Rapa huyo ambacho
kwa mujibu wake kimemuathiri kisaikolojia.
JUELZ
SANTANA AACHIWA HURU
American Rapa, LaRon Louis James ‘Juelz Santana’ ameachiwa huru kutoka gerezani mara baada ya kutumikia miezi 17.
Ikumbukwe kwamba mwezi March mwaka 2019, Santana alihukumiwa kifungo cha miezi 27 mara baada ya kukutwa na silaha kwenye begi lake akiwa uwanja wa ndege, ambapo alikimbia na kuliacha mikononi mwa polisi.