Barcelona na
Pierre-Emerick Aubameyang wamefikia makubaliano ya mchezaji huyo kujiunga na
Klabu hiyo baada ya mshambuliaji huyo kusitisha mkataba wake na Arsenal.
Jinamizi la
Pierre-Emerick Aubameyang Arsenal limekamilika, huku mshambuliaji huyo
akijiunga na miamba ya Uhispania Barcelona kwa uhamisho wa bure na kusaini
mkataba wa miezi 18.
Barcelona
wamethibitisha dili hilo Jumatano kwa video iliyoandikwa kuwa 'Ni Wakati wa
Auba'. Walitangaza mkataba huo nje ya dirisha la uhamisho barani Ulaya kufungwa
kwa sababu Aubameyang aliwekwa kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na
Arsenal kukatizwa.
Aubameyang
alivuliwa unahodha wa Arsenal mwezi Desemba na meneja Mikel Arteta, akaamriwa
kufanya mazoezi peke yake na kuondoka nje ya kambi yao huko Dubai na kuchelewa
kurudi kutoka kwa safari iliyoidhinishwa na klabu kwenda Ufaransa.
Mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 32 alipigwa picha akiwa Barcelona siku ya Jumatatu - kwa
mshangao wa Arsenal na timu ya Uhispania - lakini ilimwacha katika nafasi nzuri
ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na kukamilisha uhamisho wake.
Alikuwa na mwaka
mwingine kwenye mkataba wake wa Arsenal, ambao ulikuwa na thamani ya £350,000
kwa wiki na amepunguza masharti hayo kujiunga na Barcelona.
Huko Uhispania,
Aubameyang ataongoza kikosi cha Xavi kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Baada ya mwanzo
mbaya wa msimu, Barcelona wako pointi moja nje ya nne bora na watacheza na
Atletico Madrid walio nafasi ya nne Jumapili katika mchuano mkali.
Kwa sasa,
haijulikani ikiwa Aubameyang atakuwa fiti vya kutosha kucheza mechi yake ya
kwanza wikendi hii. Ingawa amekuwa akifanya mazoezi peke yake wakati wa
uhamisho wake wa Arsenal, hajacheza kwa ushindani tangu alipocheza akitokea
benchi dakika ya 85 katika kipigo cha 2-1 kutoka kwa Everton mnamo Desemba 6.
Katika hatua moja
siku ya Jumatatu, dili hilo lilikatizwa na Arsenal walikuwa wakijiandaa kwa
matarajio ya kurekebisha mambo na kumuunganisha tena Aubameyang.
Mkataba huo
ulionekana kuporomoka kutokana na pande hizo mbili kushindwa kufikia mwafaka
kuhusu jinsi ya kugawanya mishahara ya Aubameyang, huku Barcelona wakihangaika
kutoa kiasi ambacho kiliiridhisha Arsenal na pia kukidhi vikwazo vyao vya
kifedha.
Hata hivyo,
mazungumzo hatimaye yalifufuliwa na kufungwa kwa misingi ya kawaida.
ubameyang alikuwa
Arsenal kwa miaka minne licha ya kuondoka katika hali mbaya,
alifunga mabao 92 katika michezo 163 aliyoichezea klabu hiyo.