Na Kalebo Mussa.
Timu
ya Umoja wa Mataifa imetua nchini Msumbiji kusaidia maelfu ya watu ambao
wameadhirika na dhoruba ya Tropical Ana, ambayo ilitokea katika mikoa ya kati
na Kaskazini mwa nchini mapema wikii hii.
Kulingana
na ripoti za vyombo vya habari, upepo mkali na mvua kubwa ndizo zimesababisha
mafuriko hayo ambapo imepelekea vifo vya watu na uharibifu wa vitu vingi.
Nchini
humo dhoruba hiyo ilipiga katika maijimbo ya Nampala, Tete,Nissa, Sofalana na
Manica, zaidi ya nyumba 10,000 zilihalibiwa pamoja na madaraja, nyaya za umeme,
Shule, vituo vya afya, mifumo ya maji na miundombinu mingine ya umma.
Hata
hivyo mamlaka za mtaa zilisema kuwa takribani
vituo vya afya 12 na shule 137 zimeharibiwa vibaya, wanafunzi 27,300 hawana sehemu ya kujifunzia
ambapo wikii ijayo shule zinatajiwa kuanza.
Kutokana
na adhari kubwa hiyo kwa mjibu wa UNICEF
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ilisema kuwa zaidi ya watu
45,000 wakiwemo wanawake na watoto 23,000 huenda wakahitaji msaada wa
kibiandadmu kwa haraka.
UNICEF
imepeleka wafanyakazi na kuandaa vifaa vya matibabu na lishe, maji,vyoo na
vifaa vya usafi vilevile pamoja na kuweka muda wa kujifunzia ili kusaidia
watoto na familia zao, shirika hilo linakadiriwa kuhitaji zaidi ya dola milioni
3.5 kwa ajiri ya msaada huo.
Maria Luisa Fornara, Mwakilishi wa UNICEF nchini Msumbiji alisema kuwa wanafanya kazi pamoja na Serikali na washirika wengine ili kuhakikisha watoto na familia zao wanapata msaada wa kuokoa maisha yao.
“Dhoruba hii imeleta adhari kubwa nchini hasa watoto wameadhirika pakubwa” alisema Fornara.
Msumbiji kwa sasa iko katika msimu wa mvua na Umoja wa Mataifa ilisema kuwa inahofia ikiwa hali nyingine itatokea tena kwani itatasababisha adhari kubwa zaidi.