kocha wa Simba Pablo Franco Martin.
Na kalebo Mussa.
Toka msimu uanze wa ligi kuu ya NBC Premier League Simba Sport Club ambayo imebeba ubigwa kwa takribani misimu minne mfululizo, hali ni tete kutokana na mwenendo wake wa uchezaji na upatikaji matoke.
Timu hiyo ambayo mpaka sasa imecheza mechi 13 katika
mzunguko wa kwanza wa ligi kuu imefunga magoli 8, imepoteza mechi 6 ambapo
mechi 4 imetoka suluhu na 2 imefungwa.
Benchi la ufundi mpaka sasa limekaa kimya juu ya
mwenendo huu wa Simba kitu ambacho kinaleta maswali mengi kwa mashabiki na
wadau mbalimbali wa michezo.
Kocha Pablo Franco Martini akiwa na msaidizi wake Selemani Matola wanaonesha
kuishiwa mbinu madhubuti ya kufunia nyavu za magoli, licha ya wachezaji kupiga
mashuti ya kulenga goli vilevile kufika mara nyingi katika lango la goli na
kushindwa kuweka mpira kimyani mwa maadui zao.
Mitazamo ya mashabiki na wadau wa michezo mbalimbali
imekuwa mingi huku wengi wakilalamikia benchi la ufundi kwa kushindwa kufanya
kazi yake inayopaswa kama ilivyokuwa katika msimu uliopita ambao Simba ilikuwa
na mafanikio makubwa katika mpira.
Idd ki Pazi ‘Father’, kipa wa zamani wa kimataifa wa
Tanzania ambaye pia aliwahi kuwa goli kipa wa Simba kwenye miaka ya 1990 alisema
Yanga na Simba huwa wanapokezana kwahiyo haya ambayo yanatokea kwa Simba ni ya
kawaida ispokuwa uongozi unatakiwa usimame imara kuipigania Simba.
“Ungozi usimame imara kuipigania Simba, mara nyingi
mambo haya yakitokea kuna kuwa na mvutano na migogoro sasa sijajua ndani ya
Simba yenyewe kuna nini labda tuone kama
ni vitu vya kawaida au ndiyo haya nayoyaona ya zamani, zamani kulikuwa kunanza
migogoro ya ndani kwa viongozi wenyewe” alisema Pazi.
Alisema licha ya Simba kuwa na kikosi kipana chenye
wachezaji imara bado inashindwa kupata matokeo, kwa kawaida Simba ilikuwa ikienda
muda wa mapumziko ikiwa tayari imeshinda magoli kadhaa.
Aidha, Pazi alisema washambualiji wa kimataifa kama ,
John Bocco amekuwa akikosa magoli ya wazi jambo ambalo siyo la kwaida kulingana
na kiwango chake cha uchezaji mpira.
Pazi aliongeza kuwa kocha wa Simba Pablo bado
anaonekana kuvurugika katika mbinu zake za kupanga kikosi na cha kuleta
ushindi labda huenda amekuja katika
msimu mbaya.
“Simba bado haijasimama kwa mfano majirani zetu wakipanga
timu inapagika lakini sasa hivi kwa upande wa simba bado timu inamvuruga Palo”
alisema.