Na, Kalebo Mussa, Dar Es salaam.
WAZIRI wa nishati, January Makaba amekanusha taarifa
ya uhaba wa mafuta kwa siku 15 kama ilivyotolewa na mkurugenzi wa TPDC, Dkt.
James Mataragio.
Makamba ametoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twitter
ambapo alisema hakuna uhaba wa mafuta, hakuna haja ya watu kuwa na taharuki.
“Takwimu za mafuta ya taa nilizonazo ni za siku tano
zilizopita, ambapo nchini kulikuwa na lita 3,978,276 zinazotosheleza kwa
mahitaji ya siku 46” alisema Makamba.
Akijibu swali la mdau alieuliza mkanganyiko kati ya
mkurugenzi wa TPDC na kauli yake kujichanganya, Makamba alisema kauli yake ni
ya uhakika ya Serikali.
“Hakuna uhaba
wa mafuta nchini. Hakuna sababu ya kuwa na taharuki. Utaratibu wa kuingiza
mafuta unahakikisha kwamba mahitaji yapo wakati wote. Serikali inaendelea
kuchukua hatua kuongeza uhakika wa upatikanaji na unafuu wa bei”, alisema
Makamba.
Aidha , amemtaka mkurugenzi wa TPDC aende ofisini
kutoa maelezo kabla hajachukuliwa hatua za Zaidi.