Na, Kalebo Mussa,Dar Es Salaam.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dk. Hussein Ali Mwinyi amewataka viongozi na watendaji wa Wizara na idara za
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutekeleza wajibu wao katika kusimamia mifumo
ya ukusanyaji na matumizi ya fedha za Serikali.
Akizungumza Ikulu jana visiwani Zanzibar katika kikako
cha kupokea ripoti ya mthibiti na mkaguzi mkuu wa serikali (CAG) Dkt. Othamani
Abass Ali, alisema kuwa hategemei ripoti ijayo ya mwezi June, 2022 kuwepo lundo
la dosari.
Alisema lazima hali hii ilekebishwe mara moja kila mtu
atimize wajibu wake kwani taasisi nyingi za serikali hazijatimiza wajibu wake
ipasavyo katika ukusanyaji wa mapato.
“Baada ya
kupokea ripoti hii nadhani kila mmoja wetu aone wajibu wake katika kurekebisha
hali, leo ni sisi tunaozungumza fedha za OS hazitoshi, fedha za miradi ya maendeleo
hazipatikani”, alisema Mwinyi.
Dkt. Mwinyi alisema ripoti hii inaonesha kuna sehemu nyingi tungetakiwa tupate fedha
kama serikali lakini hazipatikani kutokana na kutokuwa makini katika kukusanya
mapato.
Aidha, Dkt. Mwinyi aliwakumbusha mawaziri kutembelea
katika taasisi zao ili wazijue vizuri ili kuhakikisha taasisi hizo zinafanya
wajibu wake ikiwemo ukusanyaji wa mapato ya serikali ili kuondoa dosari ambazo
zinajitokeza.
Awali, mdhibiti na mkaguzi mkuu wa serikali (CAGD)
Dkt. Othamn Abass Ali alisema katika kukamilisha
ripoti hiyo kuna taarifa ambazo waliziomba wakazikosa.
Alisema wakati
wa ukaguzi alibaini agizo la kuhamisha fedha ya mapato yanayotokana na kodi
ikiwemo mapato ya ZDRB yaliyokusanywa kupitia hesabu yake iliyopo PPZ kwenda
BOT mpaka kukamilisha ukaguzi huo, ukaguzi haukupatiwa agizo hilo.
“Mapato ya TRA yalikuwa yakihaulishwa kutoka hesabu
yake iliyopo PPZ kwenda BOT mara tatu kwa wiki, lakini huku kwetu sisi ZDRB, PPZ,
BOT hatukupata haya maagizo na kilichobaini ni kuwa hii fedha ina kaa sana
pale, hali hii ni kuikosesha serikali kufanya matumizi ya fedha hiyo kwa
wakati”, alisema Ali.
Hata hivyo, alisema
katika ukakuzi huo ulibaini kuwa taasisi ya utafiti wa kilimo Zanzabari
haina mfumo mzuri wa utayarishwaji wa bajeti katika vyazo vyake vya mapato.
Alisema hali
hiyo imetokana na kuwepo na mabadiliko ya mwaka ya makadirio ya mapato
yanayotokana na uuzwaji wa miche, mazao, pamoja na mapato ya ukondishwaji
mashaba ambayo hupanda na kushuka bila kuwepo na sababu za msingi.