Na Mwandishi wetu.
MUAMKO wa vijana kwenda kupima Virusi vya Ukimwi na kupata ushauri nasaha umekuwa mdogo sana kwani ni idadi chache ya vijana wanaoenda kupata huduma hiyo.
Akizungumza na Nipashe Mshauri kutoka Zahanati ya Kinyerezi Jijini Dar Es salaam, William Michael alisema kuwa watu wengi wanaogopa kwa sababuu ya ugojwa wenyewe jinsi ulivyo.
“Wanaokuja kupima wenyewe kutoka nyumbani ni wachache sana ukilinganisha na wanaopima kutokana na dalili ambazo anaonesha mgonjwa, ambapo wanaokuja wenyewe kwa Julai 1 mpaka 30 mwaka huuwalikuwa 42 na 209 wakiwa ambao wanapimwa kutoka na dalili walizonazo,” alisema Michael.
Alisema vijana wanakitu kinachoitwa hofu ya utambuzi kwamba hufikilia endapo atakutwa na maambukizi itakuwaje, hofu hiyo imekuwa kubwa kwasabau ya aina ya ugonjwa kuwa mkubwa.
Aliendelea kusema kuwa mtindo wa maisha hususani wanaume hujikita katika shughuli za utafutaji ukilinganisha na wanawake hivyo kushindwa kufika katika vituo husika, vilevile wanaume wengi huwa na tabia ya kupuuza masuala ya kucheki Afya zao.
“Wanaokuja kupima sana ni wanawake ukilinganisha na wanaume, ukiona mwanaume amekuja kupima inabidi umpe kipaumbele na atakupa mambo mengi kulingana na vitu vingi alivyopitia,”alisema Michael.
Aidha, Michael alisema kuwa ili uweze kukaa vizuri kama kijana hutakiwi kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mtu ambaye hujui hali yake ya kiafya, kabla haujingia katika mahusinao hakikisha unajua hali ya kiafya ya mwezio pia historia yake.
Kuwa na mtu mmoja katika mahusiano ambaye mnaaminiana, vilivile vijana watumie kinga ili kulinda afya zao dhidi ya maambukizi ya Ukimwi.
Ahamedi Saidi ambaye ni mmoja yawaliofika kituoni hapo kupata ushauri nasaha alisema kuwa yeye kila mwezi huwa anautaratibi wa kwenda kucheki afya ili kujua maendeleo ya afya yake.
“Nakumbuka kipindi nasoma walimu walikuwa wanatufundisha kuwa kucheki afya katika mwili wa binadamu ni muhimu sana ili kujua uko katika hali gani, kadri nilivyokuwa naelewa kila mwisho wa mwezi kwa sasa ni lazima nicheki afya,” alisema Saidi.
Pia aliwashauri vijana wajitokeze kwa wingi kwenda kucheki afya zao ili wajue afya zao kama wanamaaumbukizi ya Ukimwi ni muhimu sana kwa vijana kucheki afya.