MAPYA yameibuka katika tukio la kijana Hamza kushambulia watu 11 kwa risasi na kuua watano katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Ufaransa, Dar es Salaam.
Wakizungumza na Nipashe kwa nyakati tofauti majirani na viongozi wa eneo alilokuwa anaishi kijana huyo, walisema alikuwa mtu wa kawaida hawakuwahi kusikia ubaya wowote kutoka kwake.
“Tunavyojua sisi ni mtu ambaye anahagaika na mambo yake kama wanavyohagaika watu wengine, lakini matukio mengine mabaya sisi hatuyajui kwasababu hatujawahi kuona akifanya vitendo hivyo,”
Kuhusu madai ya kuwa alikuwa gaidi, alisema siyo kweli kutokana na maisha waliyokuwa wakiishi mtaani, kwa kuwa alipenda kuswali katika Msikiti wa Shazilia.
Kwa mujibu wa Mkuu Operesheni wa Jeshi la Polisi Sabasi, alisema hadi sasa wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo ili kujua dhamira yake.
Katika tukio hilo askari watatu waliuwawa, mlinzi wa kampuni binafsi ya …na wengine sita kujeruhiwa ambao wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).