FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

MESEJI ZA KUMUOMBA MPENZI WAKO MSAMAHA

 


Kugombana katika mahusiano ya kimapenzi ni sehemu ya mahusiano hivyo inapotokea kwamba mmegombana, basi unatukaiwa kumtumia meseji zifutazo ili aweze kukusamehe:


1. Hivi kweli haya ndiyo mapenzi ama naota njozi? Nimefanya kila naloweza kuliimarisha letu penzi lakini naishia kuambulia majonzi, nimekuwa mtu wa kububujikwa na machozi kwa sababu ya lako penzi, kama nimekukosea tafadhali niwie radhi mpenzi, nakupenda na amini wewe pekee ndiye uliyetimiza ndoto yangu ya mapenzi.

2. Hivi ni kosa gani nilililokutendea ambalo sipaswi kusamehewa? Ni kweli nilikosea nahitaji kusamehewa mpenzi, plz naomba nielewe kwani sina mwingine zaidi yako wewe. Luv u

3. Nakiri kweli nimekukosea naomba wako msamaha kwa yote yaliyotokea hakika nimekukwaza.

4. Lakini kwa hakika hii ni mara yangu ya kwanza naamini,naamini utanisamehe laaziz na kunipa nafasi ya kulienzi lako penzi.

5. Unajua nakupenda ila tu umeamua kunitenda rudisha moyo nyuma kisha twende sambamba mapenzi yanavyokwenda.

6. Mapenzi ni usanii ukiigiza utashindwa,mapenzi yanatoka moyoni wengi walioigiza walishatengana,mpenzi wangu usiniache.

7. Penzi la kweli siku zote hudumu,penzi la kitapeli haliishi ugomvi,mpenzi wangu leo nimegundua nakukosea na naahidi kubadilika na kuwa mpenzi mpya na bora,nisamehe .

8. Mpenzi nashukuru nikikuacha nitakuwa ninakufuru mi ndiyo mpenzio na hauna mwenzako mpenzi kuwa huru.

9. Japo umeniuzi sina budi kukupa hizi pongezi, sijui umejifunza wapi mapenzi, hakika kwako mi ni mfungwa wa mapenzi! Nakupenza mpenzi nitunziye langu penzi!

10. Hakika sikutaraji kulikosa lako penzi, wataka kuniacha kuniacha ningali nakuhitaji, mpenzi tambua nahitaji yako hifadhi na niko radhi kukupeleka hadi kwa wangu wazazi, amini kwenda kwa mwingine sihitaji. Nakupenda.

11.Siamini kilichotokea, hakika nimekukosea, lakini naapa katu sitorudia, upuuzi niliokufanyia, najua jinsi gani waumia ndiyo maana umeninunia, nisamehe mpenzi nafsi yangu ipate kutulia kwani bila wewe sina thamani katika hii dunia!

12. Kina ninapokukumbuka machozi yanidondoka, hivi leo mwana wa mwenzio ninaumbuka kwa kuparamia mapenzi kwa pupa, ukweli nakupa, hivi sasa najuta! Nisamehe mpenzi.

13. Ni kweli nakiri ndani ya nafsi yangu kwamba nilikukosea mpenzi wangu, naomba unisamehe na unipe nafasi nyingine katika moyo wako mpenzi wangu. Nakupenda sana, pokea busu mwanana....mwaaaaaaaa...