Msanii wa
vichekesho nchini, Peter Mollel ‘Pierre
Liquid’ ameeleza namna ambavyo alivyopona ungonjwa wa Covid 19,awataka
Watanzania kutokuwa na hofu dhidi ya ungonjwa huu
Akizungumza kwa
nyakati tofauti Pierre alisema kuwa kwa kiasi kikubwa mazoezi yalimsaidia
kupata unafuu kwa uharaka sana.
“Niliwekwa karantini
Amana nikawa natumia dawa nikawa nameza pia kingine nikawa nafanya mazoezi ya
viungo, kwakeli yamenisaidia sana kwasababu nilikuwa siwezi kupumua vizuri
lakini baada ya kuwa nafanya yale mazoezi niakajikuta mapafu yanapanuka vizuri.
kwahiyo kuanzia hapo nikawa natoa pumuzi
vizuri tofauti na mwanzo nikasema basi kumbe mazoezi yanasaidia toka hapo
maumivu ya kichwa nayo yakawa yameondoka kifua tena kikawa hakiumi tena mbavu
zilikuwa zinanibana sana nazo zimeacha kubana mpaka sasa hivi niko vizuri
namshukuru Mungu.
Mungu
atusaidie kabisa na atuepushie na huyu mdudu ambaye anatusakama katika nchi
yetu.” Alisema Pierre
Aidha aliongeza
kwa kuwataka Watanzania wasiwe na hofu bali wawe na ujasiri wa kwenda kupima
endapo wanapokuwa wamejihisi kuwa na dalili zinazofanana na ungonjwa huo.
“Nachosema kwamba
kwa Watanzania wenzangu wasihofu kwenda Hospitalini wanapopata zile dalili waende mara moja
kwasababu unapoenda kule mapema ndipo unapoweza kupata nafuu vizuri kama mimi nilivyoweza
kupata nafuu haraka sana kwababu
nilipogundulika na huo ungonjwa nikaenda na kama hivi nimetoka, inamaana
inawezekana ukapona kama nilivyo vizuri . nilikuwa nakula machungwa,maji ya
limao,tangawizi ni hivo tu basi” aliongeza.
Beyonce
kuunga mkono sekta ya afya
Msanii kutoka
nchini Marekani, Beyoncé Giselle Knowles ‘Beyonce’ akiwa na mama yake mzazi, Bi.
Tina Knowles wameamua kuchangia Sekta ya Afya kwa kujitolea vifaa vya kupima virusi
vya Corona pamoja na vifaa vingine muhimu kwa watu kujikinga.
Beyonce na
Mama yake kupitia tovuti yake ameanzisha kampeni iitwayo ‘IDidMyPart’ ambayo
inawahamasisha jamii ya watu weusi kuweka kipaumbele suala la afya zao kwenye
janga hili la Corona.
Aidha lengo
la kampeni yao ni kwa watu maarufu kuchangia kupitia tovuti hiyo , mpaka sasa Tyler
Perry tayari ameonesha nia ya kutoa vifaa
vya upimaji wa Corona mjini Atlanta Georgia.
Ikumbukwe kwamba
kabla ya kuja na kampeni hii Beyonce ameshawahi kuchangia kiasi cha ($6 million) sawa na Bilioni 13.8 za
Kitanzania kwa asasi za huduma za kijamii kwa ajili ya kuchangia vifaa tiba
mjini New York, Houston, Detroit.
Wema alamba
dili nono
Msanii wa
Bongo Movie ambaye pia kwa sasa amejikita kwenye mapishi kupitia kipindi chake
cha ‘CookwithWemaSepetu’ ,Wemu Abrahamu ametangazwa rasmi kuwa balozi wa sosi
ya nyanya (Tomato Sauce) kutoka kampuni ya RedGold.
Akiongea na
Waandishi wa Habari jana Wema alibainisha kuwa RedGold ni bidhaa zinazotengenezwa
na Darsh Industries Tanzania ambapo wana
bidhaa nyingine nyingi zikiwemo Tomato Sauce, Chilli Sauce, Jams, Juice na
Ketchup.
Aidha aliongeza kuwa Kampuni hiyo ya RedGold
ndio wadhamini wa kwanza kwenye kipindi chake cha Mapishi kinachoruka kupitia kwenye
Application yake iitwayo WemaApp.
Hata hivyo
kupitia ukurasa wake wa Instagram alionesha furaha yake namna ambavyo
anafurahia kuwa mwanafamilia wa RedGold.
“Ninayo
furaha kutangaza Rasmi kuwa Mimi ni Brand Ambassador wa RedGold na pia RedGold
ndo Sponsor wetu wa kwanza kabisa kwenye kipindi chetu pendwa cha Cook with
Wema Sepetu kinachoruka kupitia Application yangu... .”aliandika Wema.