Msanii wa
Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ amemuandika ujumbe mzito msanii mwezake
Rich Mavoko, adai kuwa anafahamu machungu anayopitia kwa sasa hadi kupelekea
ukimya wake, ahoji wanaofurahia kupotea kwake wananufaika na kipi hasa.
Harmonize
ameandika ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo pia umeibua hisa
kali kwa baadhi ya watu
“Familia
ngapi zipo nyuma ya Rich Mavoko ? na zinamtegemea yeye kwakila jambo hasa hili
la kupata mkate wa kilasiku vip kuhusu ndoto za familia hizo na zinaishije
katika wakati huu?
Ndoto ngapi
za wasani ambao wanategemea kuzifikia hizo ndoto kupitia Mavoco ? na nyuma ya
hao wasanii kuna familia nyengine pia.
Je? maumivu
malalamiko ya wazazi wake hasa mama mzazi ambae ndio kama roho yake!
ushajiuliza ni kauli ngapi za uchungu anazitoa ambazo zinaweza kumpata kila
anaefurahishwa na hili kwa makusudi ?
Maana mzazi
wa mwenzio ni wako pia laana yake haishindwi kukupata ! la mwisho kabisa
mgeukie mwenzio anaefurahia na kuifanya hii kuwa ni habari njema kwake ya
kumfanya atembee kifua mbele na hata kuandika mtandaoni kwa furaha Mavoco
kapotea muulize anafaidika na nini ?.
Mungu
anasababu na maana yake bro Richi Mavoco kama mdogoako nakuombea najua ukimya
wako unamaana kubwa sanaa ndani yako ninachojua ni kujiweka sawa na kutuletea
kazi zingine tunakupenda na tunakuombea mungu akufanyie wepesi.! Let’s go bro
mdogoako rafiki yako nipo hapa muda wowote! Ramadan Kareem.” Aliandika
Harmonize
Ikumbukwe
kwamba toka Desemba 31, 2019, Mavoko hajaposti chochote kile kwenye kurasa zake
za mitandao ya kijamii wala kutoa wimbo mpya au kushirikishwa na msanii
mwingine.
HUSSEIN
MACHOZI AWEKA WAZI JAMBO HILI
Msanii wa
Bongo Fleva, Hussein Rashid
‘Hussein Machozi’ ambaye amekita makazi yake nchini Italia kwa muda kwasababu
ya covid 19 ameweka wazi hali ya sasa nchini humo.
Hussein
alisema kuwa kwa sasa mashariti ya kukaa ndani yamelegezwa hivyo watu wanatoka
nje licha ya kuwekewa mipaka.
“Kwa sasa
tunaweza kutoka nje tukazunguka lakini pia kuna mipaka tumewekewa kwa mfano
huwezi kutoka Morogoro ukaenda Dar Es salaam yaani umetoka nje ya nyumba yako
unaweza kwenda Kipunguni, Kariakoo hauruhusiwi kuvuka mkoa kwa mkoa
Lakini jambo
ambalo tunafurahi kwanza vifo vimepungua siyo kama vilivyokuwa mwanzo na kitu
ambacho kimesababisha vifo kupungua ni kukaa ndani na kusikiliza maelekezo
asikwambie mtu uzima uko ndani” alisema Hussein Machozi.
Aidha aliongeza
kuwa “baadhi ya vitu vimefunguliwa ikiwemo wajenzi wanaojenga, tunaomba tu
Mungu hali izidi kupungua ili watu tufanye kazi zetu kama kawaida kwasababu ni
kweli huu ugonjwa umekata hesabau nyingi sana kwa hivyo tuombeane kote
Ulimwenguni kwasababu huu ungonjwa siyo wa Italia au China pekee yake”.
R.KELLY MBIONI KUTOKA GEREZANI
Msanii wa
muziki nchini Marekani, Robert Sylvester Kelly ‘R Kelly’ huwenda akaanza
kuonekana akiwa huru kwa muda fulani, hii ni baada ya kugundulika anaugua
kisukari (diabetes) kwa muda mrefu huku juhudi za kutoka kwake zikifanywa na
wakili wake, Steven Greenberg.
Sasa maombi
haya ni ya muda mrefu kwa wakili huyo juu ya jaji wa kesi zinazo muandama
mkongwe huyo na ikimchukua muda mrefu kushughulikia kesi hiyo kutokana na
makosa ya jinai yanayo muandama mteja wake.
Hofu kubwa
ni kuwa kinga yake ya mwili imepungua hivyo itamfanya kushambuliwa na
maambukizi ya Corona hasa akiwa gerezani kwani hakuna njia sahihi ya kujikinga
ukizingatia kuna msongamano wa wafungwa.
Itakumbukwa,
R.kelly anashikiliwa kwa makosa ya unyanyasaji wa kijinsia (Ubakaji), pia
kufunga ndoa na mwanamuziki Aaliya huku akiwa na umri chini ya miaka 18.
DIAMOND
PLATNUMZ AANZA KUTEKELEZA AHADI YAKE
Msanii wa
Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametoa msaada wa kodi ya pango kwa
watu 57 ambao ni wajane, walemavu pamoja na wasiojiweza.
Msaada huo
ni waawamu ya kwanza katika ile dhamira yake ya kusaidia kodi ya pango kwa kaya
500 nchini zilizoathirika kiuchumi na janga la mlipuko wa virusi vya Corona.
Kufuatia
jambo hilo, familia zilizobakia kwenye orodha ya kaya 500 ni 443 ambapo
mchakato unaendelea kwa ajili ya kuzipata kaya za wajane, walemavu na
wasiojeweza.