Inatarajiwa kuwa msimu wa 2019-20 bado unaweza kumaliza katika mpangilio huo katika majira ya joto kwa kuchezwa ndani ya wiki saba.
Lakini pamoja na michezo hiyo ikitarajiwa kuchezwa mbele ya viwanja visivyo na mashabiki, bado wakubwa wa mpira wa miguu nchini humo wanataka mashabiki wao waweze kutazama kila mchezo wa moja kwa moja huku wakiwa nyumbani kwa kuepuka misongamano itakayowaepusha na maambukizi ya Corona.
Katika mpango huo uliombwa na maboss wa vilabu vya EPL michezo inatarajiwa kuoneshwa na Sky Sports, BT Sports na YouTube.
Lakini mara ya mwisho Ligi Kuu ilionyesha mechi za bure ilikuwa siku ya ufunguzi wa msimu wa 2013-14.
Siku hiyo, Sky Sports ilionyesha mchezo kati ya Manchester United dhidi ya Swansea wakati BT Sport iliruhusu mtanange kati ya Crystal Palace vs Arsenal bure.