Msanii wa
Bongo Fleva, Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ ameweka wazi suala la kuoa na kwa sasa yupo
kwenye maandalizi na panapo maajaliwa ataweza kufunga ndoa hivi Karibuni.
Ommy ameweka
wazi jambo hilo alipokuwa mbashara katika ukurasa wake wa Instagram ambapo
alisema kuwa kwasasa ameanza maandalizi madogo madogo ikiwemo kufuga ndevu ili hata
akienda kuposa aonekane ni kijana anaejielewa.
Aidha aliongeza
kuwa alitaka kuoa kipindi hiki cha Ramadhan lakini akaogopa asije kuuziwa mbuzi
kwenye gunia.
Msanii wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ amezua gumzo kubwa, ampigia
simu Jacqueline Wolper,Sarah
amtaka mpenzi wake aende nyumbani kwa Nicole.
Harmonize alipokuwa
live na Jacqueline Wolper katika ukurasa wake wa Instagram mashabiki wengi wali-comment
kutaka warudiane pia wengine walishangazwa na tukio hilo la Harmonize
kuwasiliana na EX wake hadharani.
Gumzo kubwa lilikuja ambapo,Harmonize alipokuwa live
kwenye Instagram akiongea na video vixen, Nicole katika wimbo wake wa "Bedroom" ambapo mke wake, Sarah
aliandika commet kuwa "Baby nenda salimia Nicole nyumbani".
Comment hiyo
ililetea sura tofauti kwa Nicole kisha kumwambia, Sarah kuwa yeye hawako kwenye
mahusiano ya kimapenzi na Harmonize kama ambavyo imekuwa ikienezwa mtandaoni.
“Wengine
wanaongea maneno mabaya, unaona comment, Baby nenda salimia Nicole nyumbani,
Why!, why!, why!, Sarah i don’t live with Harmonize in my home,” alisema Nicole
kisha na kuondoka katika line.
HABARI NJEMA
KWA MEEK MILL
Msanii kutoka
nchini Marekani, Robert Rihmeek Williams ‘Meek Mill’ na mpenzi wake, Milan
Harris wamefanikiwa kupata mtoto wa kiume.
Meek Mill
ameweka jambo hilo wazi Mei 6,2020 katika ukurasa wake wa ‘Twitter’ ambapo siku hiyo pia alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa.
Meek Mill
ameiita hii ni zawadi yake bora kabisa kwake na huyu anakuwa mtoto wake wa
tatu, tayari ana watoto wawili wa kiume Murad Williams na Rihmeek Williams.
Msanii wa Bongo
Fleva na mwanamitindo , Hamisa Mobetto jana ametambulishwa rasmi kuwa
mwanafamilia wa taasisi ya Smart Generation.
Taasisi hiyo
inajikita kuchukua watu ambao wanaushawishi mkubwa katika jamii ili kuweza
kuwahamasisha vijana katika nyanja mbalimbali
Mwanamitindo
huyo ambaye anaushawishi mkubwa hasa katika mitandao ya kijami aliweka wazi
namana ambavyo atajikita kuwashawishi vijana kuwa makini katika suala la uzazi
wa mpango
“Tukiwa kwenye
taifa lenye uwazi na ukweli ni vizuri kwa kila kijana ambaye ametimiza umri wa
kuwa kwenye mahusinao kuchukua hatua ambazo zinafaa wakati wanaanza mahusiano
ili kuepuka mimba ambazo hawajatalajia na hii inaenda kwa pande zote mbili kwa
maana ya wanaume na wanawake”. alisema Mobetto.
“Tukiwa kama
taifa ningependa kushauri kwa kila kijana wakati wakuanza mahusiano ni wakati pia
sahihi wakujipanga katika maisha yako usilete kitu chochote kikwaze wewe kutimiza
malengo ama ndoto zako katika maisha, vituo vya afya tunavyo vingi nchi nzima
ni vizuri kila mtu aende kwenye vituo hivyo akapate ushauri na kuna njia tu za
kujizuia kupata ujauzito kama hauko tayari kwa kutumia uzazi wa mpango kuna
mipira na njia nyingi”.aliongeza
Aidha C.E.O
wa SMART GENERATION, Siza akiwa na Msanii wa Bongo Fleva Nikki Wa Pill alisema kuwa lengo kubwa ambalo wanalitizamia
ni kuwawezesha vijana wa Kitanzania kuweza kutumia vipaji vyao ili kufika
mbali.