Habari kubwa
ya kiburudani katika mtandao wa kijamii ni kuhusu lebo kubwa ya burudani nchini
Wasafi (WCB) ambayo iko chini ya C.E.O. Naseeb Abdul kumsaini msanii mpya wa Bongo Fleva wa kike,
Zuchu ambaye mpaka sasa anatamba na wimbo wake uitwao ‘wana’.
Zuchu ameonesha
kufurahishwa sana kwa kuingia mkataba na lebo hiyo ambayo inaaminika pakubwa
kuwa inaubunifu mkubwa katika burudani kitaifa na kimataifa.
Kupitia ukurasa
wake wa Instagram wa msanii huyo amefunguka maneno ambayo dhahili ni furaha
kubwa kwake kwa kuwa sehemu ambayo itampa nguvu za kupanua mbawa zake zaidi ili
kufikia malengo yake zaidi.
“It's a huge honor to finally fulfill my dream,
na pia ni baraka na bahati kubwa sana to be signed under The biggest label in
Africa Wcb Wasafi
“Nikiwa kama
mwanamke ndoto yangu kubwa ni kutumia kipaji changu kuthibitisha ule usemi
"Power's not given to you. you have to take it" yaani "nguvu haiji
kwa kupewa, bali kwa kujitengenezea mwenyewe".
“Na hii ni
ili kufuta imani na dhana potofu kuwa wanawake hawawezi bila ya kuwezeshwa.
“Na muhimu
zaidi pia safari yangu katika muziki iende kuwatia nguvu wanawake wote
kupambana katika kutimiza ndoto zao.
Kwa zaidi ya
miaka minne niliisubiri siku hii.
“Thank you Diamond Platnumz and whole of Wcb Wasafi
Management for believing in my talent expect the absolute best.
To all music
lovers from all Over the world, ninaitegemea sana support yenu.
“Asante
Mwenyezi Mungu kwa kipaji na nafasi hii, Ninakuomba uniongoze katika njia yenye
Mafanikio”. aliandika Zuchu
Achilia mbali
na hilo Diamond Platnumz kupitia ukurasa wake wa Instagram hakusita kutoa neno
ambapo alimtaka msanii huo kuwa kielelezo kwa wanaweke wengine kujiona kuwa
wanaweza ambapo wanapofanya juhudi ya kutimiza ndoto zao.
“kupitia
wewe na sapoti ya wadau na mashabiki, tukabadilishe mtazamo na fikra potofu na ulimwengu
wajue kuwa mwanamke ukimuwezesha anaweza” aliandika Diamond Platnumz.
Hata hivyo
msanii mwenzake wa kike Faustina Charles Mfinanga maarufa kama Nandy alifunguka
ya moyoni kwa kuona kuwa tasnia ya burudani sasa inaenda mbele zaidi kwa kuwa
na ongezeo la wasanii wa kike.
“Hongera
sana Zuchu am proud of you! another queen in Tanzania tusogeze Bongo Fleva mbali zaidi nakuamini” aliandika Nandy
Vilvile nao
mashabiki hawakuwa nyumba kutoa maoni yao juu ya suala hili ambalo wengi wao
wameoneshwa kufurahishwa na kusainiwa kwa msanii mpya katika lable hiyo.
Mapokeo yao
yamekuwa makubwa hasa kupenda wimbo wake mpya ambao unafanya vizuri sasa.
Kwa maana
hiyo sasa Zuchu atakuwa imetimiza idadi ya wasanii sita, Naseeb Abdul, Mbosso,
Lava Lava,Rayvvan, Quuen Darlin, Zuchu.
Zuchu ni mtoto
wa malkia wa taarab nchini Tanzania, Khadija Omary Kopa, mama huyo alimpa
maneno ya busara mwanae ambayo hakika ni furaha kubwa
“Kila hatu
Dua, Allah akuongoze Mwanangu imekuwa ndoto zako kwa miaka mingi sana na leo
umetimiza nusu ya ndoto hizo kilichobaki ni dua na salaa nyingi ili Allah azid
kukusimami, Nimefurahi Sana Sana na Allah awasimamie nyote wewe na Ma boss zako
na wenzio wote unaofanya nao kazi mzidi kuendelea kufanya mazuri na makubwa,
Tulia upo sehemu salama mama, Nakupenda Sana Mwanangu” aliandika Khadija Koppa
katika ukurasa wake wa Instagram.
Khadija Koppa
alifunguka namna mwanaye alivyokuwa na furaha kubwa ya kuwa sehemu ya Wasafi
“Yani
sijalala kwa amani kwa furaha maana kama siamini,tumemfuta sana machozi mpaka
leo kafikia hapa Basi Ashukuriwe M/mungu kwa neema hii” aliandika
kabla ya
kujinga na WCB, amewahi kushiriki shindano ya kusaka vipaji vya muziki barani
Afrika mwaka 2016 liitwalo Tecno Own The Stage ambalo pia Nandy alishiriki na kupata Sh36 milioni baada ya
kuwa mshindi wa pili.
Pia Zuchi
ameshiriki baadhi ya nyimbo ukiwemo ule wa ‘Super Woman’ ambao ulishirikisha
wasanii mbalimbali wa kike wa Bongo Fleva na taarabu.
Hata hivyo
katika kusaka kipaji chake na kufikia ndoto aliwahi kurudia baadhi ya nyimbo za
wasanii madharani wimbo wa Nadekezwa wa msanii Mbosso.
Taarifa zaidi
zinasema kuwa Zuchu alikuwa katika lebo hiyo kwa mda mrefu tangu 2018 ambapo
amekuja kusainiwa rasmi aprili 8, 2020 Mungu amuongoze katika safari yake ya
muziki.
KING KIBA AFUNGUKA UKWELI KUHUSU
MOBETTO
Nyota wa
muziki nchini, Ali Salehe ‘King Kiba’ amefunguka na kueleza uhusiano uliopo
kati yake na mrembo, Hamisa Mobetto na kusema kuwa anamchukulia kama msichana anayemuheshimu na anampenda.
“Mimi na
Hamisa ni kama familia na mheshimu ni mschina ambaye anajiheshimu na nampenda”
alisema Alikiba
Aidha April 8 mwaka huu msanii huyo ametoa wimbo wake mpya uitwao ‘Dodo’ ambapo Hamis ni vixen wa video hiyo.