Hali ngumu
inapotokea yaani (Crisis) mara nyingi
huwa inatoa matokea ya kutengeneza makundi mawili, kundi la kwanza ni watu
ambao wanashindwa (Fail) katika kipindi hiki kigumu watu hawa hupoteza kazi,
mitaji,biashara,fedha, na mambo mengine
yakwao huenda tofauti .
Lakini
katika huu wakati kuna watu wataibuka ambao wanaitwa washindi au watu wanao
pata (gain) kwa maneno mengine hakuna kupoteza kwa ujumla kwa sababu kuna
baadhi watapa na wengine watapoteza.
Kwahiyo
hakuna (Crisis) au mgogoro, jambo fulani gumu linapotokea linalokuwa halina
kitu ndani yake matatizo yanapokuja
kunakuwa na makusudi fulani yanakuwepo ambayo yamejificha ndani ya ule mgogoro
kwahiyo tunapojifunza masuala ya kifedha lazima tufahamu kwamba hali kama hii
inapotokea huwa inakuwa imebeba nini? Kuna kitu fulani kimejificha kwahiyo
tusichukulie tu kama jambo la kawaida ili mbeleni isije kutuathili pakubwa.
kusudi la
kuwepo kwa changamoto kama ya aina hii
Kusudi la
kwanza la hali ngumu inapokuwa imetokea moja wapo ni kudhihilisha udhaifu ambao
upo katika maeneo mbalmbali, udhaifu huu unaweza kuanzia kwenye nchi kwa mfano
mfumo ya nchi, mfumo wa kifamilia ,mfumo ya kitaasi.
Kabla ya
changamoto kubwa kutokea kila mtu huwa anakuwa hodari (stable), maisha ya kila
mtu huwa sawa sawa, kila mtu hujiona kuwa hawezi kuyumba au kuteteleka lakini
inapotokea wakati kama huu ndipo haya mambo yanaanza kujionesha, udhaifu huanza
kuonekana. Eneo la kwanza kabisa ni katika mfumo wa kifedha kabla ya wakati huu
mgumu kila mtu alikuwa anajiona yuko salama mambo yake yako vizuri hawezi
kuteteleka kwa namna moja au nyingine ,
baadhi ya
watu walikuwa wakiona biashara zao ziko vizuri pia vipato vyao lakini jambo
kama hili lilipotokea limedhihilisha kwamba kumbe kuna watu mifumo yao ya
kifedha haiko imara au dhabiti wameshindwa kuingiza tena fedha waliokuwa
wanaishi maisha mazuri baadhi yao maisha yamebadilika pakubwa wameporomoka sana
kutoka juu mpaka chini.
Kwahiyo hii
inadhihilisha na kuchimbua udhaifu tulionao na ni muhimu kuangalia kwasababu
kuna wakati unafikili jambo liko sawa ni mpaka wakati mgumu unapotokea ndipo
unajijua kumbe mimi siko salama kama nilivyokuwa nafikili kwenye eneo la
kifedha.
Eneo la pili
ambalo linadhihilishwa ni thamani yako, kuna watu kutokana na changamoto
zilizotokea sasahivi thamani yao imeshuka sana kwasabau kuna baadhi ya watu
katika soko ujuzi wao hauhitajiki tena isitoshe wao wenyewe thamani yao
imepotea kabisa
hakuna
mahali wanaalikwa,kuuza, kununua, mtu anakuwa (reduced to zero) kwahiyo
inadhihilisha kuwa kumbe hakuwa na thamani kubwa kama vile ambavyo alikuwa
anafikilia na asipokuwa muangalifu pengine huko mbeleni anaweza akapoteza kila
kitu ambacho alikuwa nacho pia.
Eneo la tatu
ambalo linadhihilishwa ni ukomo wa ujuzi wako (Limitation of skills) kuna
wakati unajiona kama vile ni mtu mwenye ujuzi unaohitajika sana kwenye jamii
lakini baadaye inapotokea hali ngumu kama hii ndipo unagundua kumbe ujizi wako
siyo bora kama nilivyokuwa nafikilia.
Hii utaiona
hasa wakati huu ujuzi wako hauwezi kukusaidia kuingiza pesa,kutatua matatizo
yako, kupenya tafsiri yake ni kwamba pengine haukuwa imara kama ulivyokuwa
unajiona. Kwahiyo kiufupi chakwanza kabisa hali ngumu kama hii inapotokea
inakuja kudhhilisha maeneo gani tuko dhaifu.
Kwahiyo
badala ya kulalamika na kunungunika unachotakiwa kufanya ni kujiuliza hivi
jambo hili lililotokea ni maeneo gani yamenidhihilisha kwamba mimi niko dhaifu
ili sasa ujipange.
Kusudi la
pili wakati huu wa hali ngumu huwa inaibua watu wapya, kwenye kila changamoto
siku zote usije ukasahau kuna watu wapya wataibuka kwasababu changamoto
inatabia ya
kurudisha
baadhi ya watu chini na kuimbua watu wengine juu. Kwa baadaye kuna watu wapya
watatokea, kuna vipaji vipya ambavyo hatuvijui vitaimbuka kwasababu changamoto
inasababisha watu waje na ubunifu wa aina fulani.
Lakini kuna
viongozi pengine wataibuka wapya katika eneo mbalimbali na ambao tulikuwa hata
hatuwajui vile vile kuna biashara mpya zitaimbuka ambapo toka zamani
hazikuwepo, kuna majina mapya tutaanza kuyasikia kwahiyo kiufupi ni kwamba hali
ngumu inapotokea kama hii huwa inaibua watu wapya.
Kwahiyo
kikubwa ni kwamba mstari ambao unachorwa kuna watu wanashuka chini taratibu na
kuna baadhi wanapanda juu taratibu .
Kusudi la
tatu katika kipindi hiki kigumu ni kuleta style mpya ya maisha, baada ya
changamoto hii tuliyonayo ukweli ni kwamba aina ya maisha ya watu yaani (life
style) huwezi kuwa sawa sawa kama ilivyokuwa zamani .
style ya maisha
yatabadilika katika maeneo mbalimbali madharani, Afya, matumizi ya technology,
fedha, tabia za kifedha,namna ya watu wanavyouza na kununua.
Nini
unatakiwa ufanye wakati huu mgumu ambao umeathili pakubwa.
Hakuna
changamoto kubwa inapotokea inakuwa na hasara peke yake ndani yake kunakuwa na
kufaidika kwa namna moja au nyingine na wewe unatakiwa uwe sehemu ya watu ambao
hawazulika sana na changamoto hii.
Kukataa kuwa
na fikra za jumla, wakati wote kunapokuwa na ungumu wa maisha kikawaida uwezo
wa watu kufikili huwa unashuka . Uwezo wa kufikili unapokuwa unashuka madhara
yake ni kwamba watu hawatumii muda mrefu kuchakata taarifa chochote kinachokuja
mbele yao kinakuwa halali yao.
Kwahiyo
hawapati muda wa kutafakari, kufikilia na hali ya ubunifu inakuwa imeshuka sana
na hii inasababishwa na mambo mawili
makubwa, jambo la kwanza ni kwa sababu ya hofu (fear) mara nyingi kunapokuwepo
na hali ngumu ya maisha watu wengi sana wanakuwa wanasumbuka sana na hofu
Mara
nyingi hofu huwa inaathili uwezo wa
ubongo kufikilia ,inaathili uwezo wa ubongo kuja na suluhisho, inaathili uwezo
wa ubongo kuwa na alternative za maisha
na njia mbadara. Jambo la pili ni kwasababu ya taarifa zinazofanana, sasa hivi
mambo yamekuwa kama yamesimama kwahiyo mtu akiamuka asubuhi anapata taarifa
zilezile mpaka anakwenda kulala
Kwahiyo hii
inachangia kwamba watu hawana vitu mbadara, hawana mawazo mbadara kwasababu
marighafi ya mtu kufikili ni taarifa ambazo anazokuwa anazipata hivyo kama
hapati taarifa mpya hauthili uwezo wa kufikili upya pia
hofu ikizidi watu wengi unakuta hawawezi kusoma, hawezi kusikiza kitu
cha kumjenga,hawezi kusikiliza kitu ambacho ni chanya.
Amua kuwa
mtu wa tofauti kwa maana kwamba usikubali kuwa na mawazo ya jumla . wewe lazima
utafute taarifa nyingine kwasababu nyakati hizi kuna watu wanaendelea (gain),
wanaendelea kutafuta njia mbadara kwasababu maisha kwa upande mwingine lazima
yataendelea kwa namna moja au nyingine kwahiyo lazima uamue kuwa mtu wa tofauti
uwe na mind ambayo iko taofauti na wengine.
Ukifikili
kama mtu mwingine utapata matokea ambayo watu wengine wanapata pia.
Katika
manunuzi nunua kile kitu ambacho unachokihitaji
siyo ambacho unakitaka ,kipindi hiki sicho cha kununua chochote kile
unachokihitaji nunua kitu ambacho hasa unakihitaji siyo unachokitaka.
Huu siyo
wakati wa kuspend wa kutumia ovyovyo kipindi hiki lazima uwe makini katika
matumizi yako kabla hujatumia ni lazima ujiulize mara mbili mbili ni dhamu yako
ya matumizi lazima iwe juu sana, nidhamu yako ya kifedha lazima iwe juu sana
kabla hujafanya chochote inatakiwa ufikilie kwa kina kwa sababu hatujui
changamoto hii itaendelea kwa muda gani na pia labda uwezo wako wa kujihudumia
utadunu kwa muda gani
Fanya kitu
cha mkakati , fanya kitu ambacho kitakusaidia kukupa matokeo kwa muda mrefu
zaidi baada ya changamoto hii kwasababu kitu moja wapo unatakiwa ukijue ni
kwamba changamoto inayotokea sasa hivi lakini madhara yake tunaweza kuishi nayo
kwa muda mrefu sana na hapa kuna mambo matano unaweza kuyafanya moja unaweza
kujenga ujuzi mpya,unaweza kupata ujuzi kwa wakati huu ambao unamuda mrefu
ukiwa nyumbani umetulia .Tafuta ujuzi mpya unaweza kufanya katika njia ya
mtandao
Jambo la
pili unaweza kupata maarifa maalumu (specific Knowledge) maarifa fulani ambayo
ni ya kipekee yanayoweza wewe kukusaidia kutoka sehemu moja mpaka nyingine
madharani kusoma vitabu na kujifunza mambo mengine.
Jambo la
tatu ni kuonesha uwezo wako kimkakati, kwa maana hiyo sasa ukifanya kitu cha
tofauti ni rahisi sana kuonekana na kujulikana kuliko wengi ambao wanafikilia
katika mtindo mmoja. Hivyo hakikisha unaimalika ule uwezo wako kimkakati katika
maeneo ambayo unaweza kujiimalisha.
Jambo la nne
unaweza ukatengeneza bidhaa au huduma mpya , kipindi hiki ni kizuri sana kwa
kufanya hivyo kwasababu unapata muda wa kufikilia, kuchakata mambo, kuona zaidi
ya kawaida, mara nyingi kitu inachoongeza ubunifu wa kitu ni ile hali ya kupata
utulivu.
Changamoto
hii itakapoisha kuna bidhaa nyingi mpya ambazo hazikuwepo duniani tutaanza
kuziona kwasababu kila changamoto inatoa fursa na inaleta maisha ya tofauti
ambayo pia mwanzoni hayakuwepo. Hivyo sasa ni wakati wako wewe kufikilia kitu
ambacho kipya unaweza kukipeleka sokoni baada ya changamoto hii kupita bidhaa,
au huduma kwa na namna wewe mwenyewe unaona.
Jambo la
tano ni lazima upate muda wa kutafakari na kupanga upya maisha yako, jaribu
kukaa chini pitia malengo yako, uwezo wako wa kifedha, nguvu ya ujuzi wako.
Kwahiyo ni wakati ambapo unaweza kuangalia ni njia gani ambazo zinaweza
kukuongezea kipato,nguvu ya kipaji chako na nguvu ya ujuzi wako.
Aina ya
ujuzi au maarifa ambao unahitaji kuwa nao hasa kwa kipindi hiki kigumu
Uwezo wa
kuchambu uwezo wako , katika hali hi kuna mambo mawili makubwa tunayoyaangali
moja kuangalia ujuzi wako, kuna ujuzi ambao unaibuliwa pia mwingine hupotea .
kwahiyo kaa chini jaribu kutafakari ujuzi ulionao sasa hivi baada ya changamoto
hii kupita utahitajika zaidi au ndiyo utapotea au pengine utahitaji kuboresha
zaidi ili ulete maana
Jambo la
pili ambalo unatakiwa ni kuchambua uwezo wako wewe, ni uzoefu wako pengine
umekuwa mzoefu kwenye jambo fulani ulikuwa ukijivunia huo uzoefu lakini je
baada ya changamoto kupita uzoefu wako utakuwa na maana ?
Sasa
unapofanya tathimini ya uwezo wako,ujuzi,uzoefu
wako kuna kitu kinaitwa (High Income Skills) au ujuzi ambao unaweza kukuongezea
pesa kwa haraka na kwa kiwango cha juu.
Mabadiliko
ya mfumo wa maisha ,uweze kujaribu kutathimini mfumo wa maisha kwa maana tabia
ya maisha, kiafya ,kifedha,kijamii,kikazi kwa namna ya watu wanavyofanya mambo.
Kila wakati changamoto inapotokea huwa inaleta fursa mpya, hali ya watu kupenda
vitu vipya ambavyo zamani watu walikuwa hawavipendi, kudhamini vitu vipya
ambavyo zamani vilikuwa havithaminiwi.
Na changamoto
inapodumu kwa muda mrefu ule mfumo wa maisha unaanza kuwa ni sehemu ya kawaidi
ya maisha ya watu katika eneo lile. Kwahiyo unatakiwa uwe na ujuzi wa kuchambua
sasa madharani unachotakiwa kuangalia ni enao lako ambalo wewe unafanyia kazi
au unapata kipato chako.
Kumbuka
hutakiwi kufanya tathimini hii baada ya changamoto hii kuisha wale wanaofanya
tathimini ya changamoto hii wanakuwa wameshachelewa sana wanaofanikiwa ni wale
ambao wanafanya mapema kabisa kabla ya changamoto haijaisha ili uweze
kujiaanda.
Technology
preference sehemu hiyo siyo lazima sana uwe mtaalamu katika eneo hili,
kunapokuwepo na changamoto ya maisha inasababisha technology ipate nguvu na
nafasi madharani kwa sasa kuna baadhi ya shule ambazo zimelazimika wanafunzi wake kusoma kupitia mitandao ya
kijamii. Hivyo kwa sasa ni wakati ambapo unaweza kufikilia namna ambapo
technology itakunufaisha ili uweze kuwafikia watu wengi.
Maarifa ya
pesa, pesa huwa inabadilisha tabia yake kipindi kama hiki
Sehemu
ambazo pesa hujificha wakati huu mgumu ambao ni changamoto kwa baadhi ya watu
Mawazo ,
kikawaida wanasema kwamba kila mwaka mwanadamu hupata mawazo takribani manne
moja ya mawazo hayo akiamua kulifuatilia kwa umakini linaweza kumpatia kipato
kizuri ambacho kinamuwezesha kuinuka kutoka sehemu moja mpaka kiwango kingine
cha maisha yake.
Sasa wewe
unatakiwa ujaribu kuwaza katika kitu ambacho unachokifanya kuna jambo gani
ambalo unaliweza kulifanya likasaidia kupunguza au kuondoa hofu, ukiweza kupata
jibu la swali hilo tafsiri yake ni kwamba watu watakuwa tayali kutumia pesa zao
hata zile kidogo wanazo ili wapunguze kiwango kikubwa cha hofu ambacho wanacho.
Kwahiyo sasa ni namna ya ewe kuja na wazo ambalo linaweza kuwaondolea hofu
katika kipindi hiki.
Bidhaa, kuna
bidhaa nyingi sana zinaendelea kutengenezwa katika kipindi kigumu kama hiki na
nyingine zitaendelea kutengenezwa kwa sababu ya mabadiliko ya kimfumo na
nyingine pia zitabunia kwasababu ya mabadiliko ya kimaisha. Hivyo sasa wewe ni
kuangalia eneo la ujuzi wako ambayo wewe unaweza kujikita katika kuitengeneza,
hapa siyo lazima utengeneze unaweza pia ukachukua sehemu ambazo zimetengenezwa
ukawauzia wale ambao wanahitaji.
Ujuzi wako,
kwa sasa hivi kuna aina nyingi ya ujuzi ambao utahitajika na siyo lazima mpaka
ukasome shuleni mwingine unaweza kusoma kupitia kwenye mitandao ya kijamii
lakini hakikisha baada ya changamoto hii kuisha unakuwa na ujuzi ambao utakupa
kipato.
Matatizo,
hapa kikubwa unachotaka kuangalia ni matatizo gani ambayo yameletwa na Corona
sasa hapo utajianda kuchangua tatizo gani ambalo unahitaji kulitatua , kadri
utakavyokuwa unatatua tatizo kubwa na ndogo ndipo utakapo kuwa unaongeza mwanya
mkubwa wa kuwa na kipato kikubwa.
Sheria
zinazoongoza matumizi ya pesa katika kipindi cha changamoto kama hichi
Sheria hizi
zimetokana na wataalamu wawili ambao walifanya utafiti mkubwa sana mmoja
anaitwa Gorger clasum ambaye mwaka 1926
aliandika kitabu chake ambapo alieleza kanuni za dhahabu zinazohusiana na mambo
ya fedha mwingine ni Mack
Phelps yeye
mwaka 1977 alichapisha kitabu chake cha sheria za fedha.
Pesa ni
matoke ya kufanya kitu ambacho watu wako tayali kukulipa kwasababu kinawapa
faida fulani kwenye maisha yako, unapopata pesa tafsiri yake ni kwamba umefanya
kitu ambacho watu wamekiona kimewapa faida kwenye maisha yao vile vile ukiona
pesa imeacha kuja kwako hasa kipindi hiki cha changamoto ni kwasabau ya mambo
mawili.
Jambo la
kwanza ni huenda umeacha kufanya kitu kabisa hakuna kitu ambacho unakifanya
kwahiyo matokeo yake ni kwamba hakuna mtu ambaye atakupatia pesa kwasababu
hakuna kitu ambacho unakifanya
Jambo la
pili nikwamba unafanya kitu lakini watu hawako tayali pengine kukulipa pesa
madharani wanakiona hakina thamani au wanaona wanaweza kukifanyia wenyewe pia.
Hivyo pesa
huja kwa mtu siyo jambo la ajabu tu au bahati nasibu ni matokeo ya kitu
unachokifanya cha tofauti ambacho watu wanauhitaji nacho sana.
Fedha
huongezeka kwa mtu ambaye anatafuta njia ya kutumia ili imletee faida zaidi na
siyo suala la kuwa na pesa nyingi kikubwa ni namna mtu anatumia pesa yake .
hivyo sasa fedha huendelea kumfuata mtu ambaye anaitumia kwa namna
ambayo
inampa faida zaidi na kwa mtu ambaye anatapanya pesa fedha huwa na tabia ya
kumkimbia
Sehemu kubwa
na yamuhimu sana ni kuwa na budget na kujali pesa yako.
Pesa
huenda kwa wale wanaoamini kwamba pesa
zipo kwa ajili yao , moja ya athali ya akili ya mtu ni kuamini kwamba kitu
fulani hakiwezekani ukiamini kuwa hakiwezekani kiuhalisi hutokea . kwahiyo
ondoa kitu kinachoitwa (Limiting belvies) hali yakutoamini katika mambo fulani
kwa kufanya hivyo unafanya ubongo wako kutofikili mbele zaidi na ubongo ukiacha
kufikili maana yake umeacha kupata fursa.
Hivyo sasa
pesa huwafuata watu wanaoamini pamoja na changamoto zilizopo pamoja na magumu
yalipo bado anafurusa ya kutengeneza na kupata pesa zaidi
Pesa huwa
inamkimbia mtu ambaye anailazimisha kupata kipato ambacho hakiwezekani au
anafuata ushauri wa walaghai au watu wajanja, katika kipindi hiki watu wengi
wataanza kutapeliwa kwasababu kunawatu ambao wanataka kupata pesa kwa ghafla
baada ya kuwa biashara zao zimeshuka au kipato
Hivyo sasa
mtu ambaye anataka kupata pesa kwa haraka sana kwa namna isiyo ya kawaida ni
kama vile wanajaribu kumlazimisha ng’ombe kumkamua atoe maziwa ambayo hana matokeo yake ataishia kutoa damu.
Usiingize
pesa yako katika mambo ambayo huyajui vizuri wala kuyafahamu kwasababu ya
tamaa, njaa, shida,matatizo unaweza kujikuta hata kile kidogo ulichonacho
unakipoteza pia
Fedha huwa
inazidi kuongezeka na kumganda mtu ambaye anaiwekeza kama ambavyo anashauriwa
na watu wenye hekima kwamba mtu wa aina hii akiwa amepata pesa yake hapeleki tu
mahali popote.
Kwahiyo
usichukue ushauri kwa mtu yeyote zigatia sana ushauri wa watu wanaojua
kuhusiana na hilo.
Baada ya
kujifunza mambo yote hayo jaribu kuyafanyia kazi kuna vitu vingi sana utapata,
ushichelewe kufanya maamuzi kwasababu utapitwa na fursa nyingi, changamoto
kadiri zinaendelea zinaleta dynamics kwa kubadilisha mambo fulani kwahiyo usiwe
mgumu wa kujifunza kama kuna uwekezaji mkubwa ambao unaweza kuufanya kipindi
hiki ni kujifunza
Madharani
kupitia video,vitabu,redio,television,mitandao ya kijamii. Hii itakusaidia
kubaki na ubora wako na kuzidi kufanikiwa wakati wote.