Msanii mkongwe wa Bongo Fleva mwenye sauti ya
kumtoa nyoka pangoni, Rehema Chalamila ‘Ray C’ ambaye pia ni dada wa wasanii wa
muziki nchini, amemtaka msanii mwenzake Naseeb Abdul Diamond Platnumz ambaye
pia ni mdogo wake kwenye sanaa kuishi kwenye maneno aliyowahi kuyazungumza.
Ray C kupitia ukurasa wake wa ‘Instar gram’ ali –‘share’
video hiyo fupi ambayo alikuwa akizungumzia
kuhusu ushikamo wa wasanii ili muziki ukue kimataifa zaidi.
“Hii ni kwako Diamond Platnumz Tusitengenezeane
chuki neno kubwa sana dogo sana hebu ishi kwa hili neno ulilotamka hata Mungu
atafurahi na atazidi kufungua baraka mbele yako acha maneno mengi wewe piga
kazi tu uwanja wako mzee baba
Nakukubali sana sema kuna muda unakera dogo mimi
ndiyo dada ako halafu nilishakwambia ukinimind kimpango wako ila nakukumbali
sana na unajua sana sema una maneno fulani yani yanaudhi sana
siku niliyokutana na wewe tukaongea nilikukubali
sana maana ulinioneshea upendo wa thati kutoka moyoni na kila mtu anayenijiua
anajua kuwa nakukubali ila kuna watu fulani wanaokuzunguka wanakuharibia sana
yaani vijembe hata havikupendezi mdogo wangu na hao wala hawakutakii mema wanakupamba
tu ili mladi uharibu tu
hawana nia njema na wewe unapendwa sana sema
mdomo dogo mdomo hebu tulia tupe tu minyimbo achana na hizi mambo aisee
usitugawe mashabiki pleas!” alaindika Ray C.
msanii mwenzake Rosa Ree alifunguka kwa kumwabia
kuwa ushauri alitoa ni wakinafiki kwani umeegemea upande mmoja.
“Ushauri wa kinafiki tu kwa nini asitoe ushauri
pande zote mbili??? Kwa nini tu Diamond ndo mwenye makosa??” Rosa Ree.
hata hivyo mashabi hawakusita kutoa ya moyoni
baada ya ushauri huo
“Huyo dada hana akili huwezi kushauri sehemu moja
tu saiv Diamond Platnumz wana mshambulia mbona upande wa pili ndo wameanzixha
zari halafu anavunga anamkazia msanii wetu mwambie atuachie msanii wetu”
aliandika mmoja wa mashabiki
‘Asap
Rocky’ anyimwa ruhusa hii
American rapper Rakim Mayers ‘Asap Rocky’ amenyimwa ruhusa ya
kutoa mavazi na kutumbuiza kwa wafungwa wa jela ambayo alifungwa nchini Sweden
mwezi Julai mwaka huu.
Mwezi uliopita Rocky alisema ata-design mavazi
kwa ajili ya wafungwa wa Jela hiyo. Kupitia ‘Twitter’ yake aliandika.
-"Even When I'm denied access to donate or
perform for the inmates in Sweden I still want to raise awareness for the
immigrants and poor people of outside surrounding areas, this has been a
difficult journey, but I feel it's my task to give back to people who supported
me when I was down." aliandika Asap
Rocky.
“Nasikia baba Tiffah unasema eti Fiesta haikujaza”
Nay wa Mitego
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel
Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameutumia ukurasa wake wa ‘Instar gram’ kutupa dongo
kwa Diamond kuhusiana na tamasha la Fiesta liliofanyika wikiendi hii katika
uwanja wa uhuru jijini Dar Es Salaam.
ikumbukwe baada ya Tamasha la Wasafi Festival
kumaliuzika tarehe 9 mwezi wa 11 na kufanikiwa kujaza uwanja kwa asilimia kubwa
ambako lilifanyikia katika viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar Es Salaam
yalianza maneno ya kukejeliana kati ya pande
mbili ambazo zimefanikiwa kufanya matamasha makubwa hapa nchini ambalo ni
Tamasha la Wasafi Festival lililochini ya Wasafi Media na Tamsha la Fiesta
lililochini ya Clouds media.
Maneno yalianza baada ya Tamasha hilo kujaza sana
na watu kuanza kusema kuwa tutaona tamasha la Fiesta kama litajaza hivi lakini
pia katikati kabla ya Tamasha la Fiesta kufanyika Dar Es Salaam yaliibuka
maneno baada ya Diamond kwenda kufanya show nchini Siera lione na kufanikiwa
kujaza uwanja watu walianza kumkejeli kuwa haikuwa show yake, na kupelekea
Diamond kuandika maneno haya:-
Sasa baada ya Fiesta kufanyika wikiendi hii
ambayo ilikuwa tarehe 8 mwezi wa 12 na kufanikiwa kujaza sana tena katika
uwanja mkubwa kuliko uwanja lilikofanyika Tamasha la Wasafi Festival maneno
yameanza mitandaoni tena hadi kupelekea msanii Nay Wa Mitego kutupa dongo kwa
Diamond na kumwambia kuwa
“Nasikia BabaTiffa Unasema Eti Fiesta Haikujaa.?
Nakujua Mwanangu Ukipanic Huwa Unakua Na Tatizo La Kuona, Sasa Relax Chukua
Time Yako Tizama Hii Clip Kwa Dakika 1 Tu, Haija Editiwa ata Kidogo Utapa Jibu
Na Utaendelea Na Kazi Zako Zingine. Pia Nikukumbushe Kitu, Mtoto Ni Mtoto Na
Mama Ni Mama Tu.”alindika Ney
Hata hivyo baadhi ya mashabiki walipongeza Nay
kwa kusema ivyo lakini wengine walmkosoa kwa kusema kuwa hakusitahili kusema
hivyo kwani yeye mi msanii kuna leo na kesho
“Wewe mwenzio anatamasha lake lako liko wapi? ebu
jifikilie nani mwenye tamasha apo kati yawasani wote apo utumwa mwanangu kila
siku upo kwenu kwanza una kolabo gan namsani wanje uyo umuwezi kwa lolote mpaka
kwa watoto mtumwa mkubwa jiongeze mambo ayo wachie wenyewe media zao” aliandika
mmoja wa mashabiki.
Uwoya sintovumilia hili kwa mume wangu
Staa wa BongoMovie, Irene Uwoya, amesema atakuwa
hana noma akimuona mpenzi wake anam 'kiss, mwanamke mwingine au kumuita majina
ya kimahaba, ila kitu atakachokishindwa ni kuona mwenza wake akimsaliti.
Irene Uwoya,alisema hayo baada ya watu kujaji urafiki wa Wema
Sepetu na Aunty Ezekiel, kupeana mabusu hadharani jambo ambalo si la kawaida
kwa wanawake kufanya hivyo.
"Mimi naona ni kawaida tu ni watu ambao wana
urafiki wa muda mrefu, ku-kiss ni vitu vya kawaida tu hakuna kikubwa hapo
haimanishi chochote hata kumwita mtu darling ni sawa tu, hata mimi mtu yeyote
naweza kumuita hivyo" alisema Uwoya.
Aidha akizungumzia kuhusu mpenzi wake, kufanya
kitendo cha kum 'kiss' mwanamke mwingine Irene Uwoya alisema.
"Kwangu mimi mwanaume wangu akimkiss mwanamke
itategemea, unajua kuna kiss zinatofautiana ukifanya hivyo katika hali ya
urafiki inaonekana na ukifanya katika hali ya mapenzi inaonekana pia, mimi
nitachukulia kitu cha kawaida cha urafiki hakuna tatizo ila akinisaliti siwezi kuvumilia" aliongeza
.