Msanii wa Bongo Fleva, Hamis Baba ‘H Baba’ amesema mwaka 2020 ni mwaka wake kwani amepania
kurudi kwa kishindo kwenye game.
H Baba alisema kuwa amekuwa mapumzikoni kwa muda
wa miaka mitano sasa na ameamua kuyarejesha makali yake mapema mwakani ataachia
kazi.
Katika kipindi cha ukimya wake kwenye ‘game’ kuna vitu vingi amejifunza ila anachukizwa
sana na baadhi ya wasanii kuwa na tabia za uongo na kuifanya fani ya muziki
kuwa kichaka cha maovu.
Aidha alifunguka kuwa wasanii wengi wamekuwa
wakitunga nyimbo nyepesi sana tofauti nay eye.
Hivyo amejianda kikamilifu kabisa kuhakikisha
muziki wake unarudi kwa kishindo zaidi ya hata ulivyokuwa zamani.
Amber Rutty akataa kufananishwa na nabii Tito
Amber Rutty
ameeleza hayo baada ya kuwepo na ‘comments’ nyingi zinazosema kwamba
sura yake na rangi yake, imefanana na nabii Tito.
“Kuna watu wanapenda kuongeaongea nifanane na nabii
Tito kwani mume wangu au mpenzi wangu, sioni kama tumefanana hatuna hata
undugu, nitafanana naye kivipi halafu yule ni mtoto wa kiume mimi ni wa kike
wapi na wapi nifanane naye” alisema Amber Rutty.
Aidha Amber Rutty aliongeza kuwa “Tupo tofauti
hatuwezi kufanana nataka nifanane na ‘role model’ wangu Amber Rose au mume
wangu ambaye nipo naye kwa saa 24, na wala sijafanana na Amber Lulu hata kidogo
mimi Rutty yeye ni Lulu” aliongeza.
Kamikaze agonga msumari wa mwisho kwa Vanessa
Mdee
Msanii wa Bongo Fleva Cyrill Kamikaze amegongelea msumari wa mwisho
kwa Vanessa Mdee na kusema, alivyomtolea lugha chafu hadhani kama alimaanisha
ila alikuwa na hasira na mawazo na kwamba hawezi kumjibu chochote.
Kamikaze ameeleza hayo, baada ya kuulizwa
kuwa alichukuliaje kauli ya Vanessa
Mdee, kumwambia hapendi wanaume ambao wana tabia za kike ambapo amejibu.
"Hilo lishapita labda tuweke msumari wa
mwisho, sikuwahi kufanya chochote wala kuongea lolote kitu kilichotokea ni kati
yake na Jux kwenye mapenzi yao, mimi sijawahi kuingilia na kujua chochote kama
aliongea hivyo ni fresh" alisema Cyrill
Kamikaze.
Aidha aliongeza kuwa "Kwa yeye kuongea vile
sijui alikuwa katika hali gani na alimaanisha nini, sijawahi kukaa naye
kumuuliza lakini nina imani hakuongea kile kitu kwa kukimaanisha, unajua kuna
muda unaweza ukaongea kitu kwa kuwa una hasira au mawazo kwa sababu ya vitu
vingi, sijawahi kumhukumu na siwezi kurudisha neno lolote" aliongeza.
Chuchu Hansy akanusha kulindwa na silaha
Msanii wa Bongo Movies Chuchu Hansy, amekanusha madai ya yeye
kulindwa na silaha na mpenzi wake, ambaye pia ni mzazi mwenziye, Vincent Kigosi
‘Ray’
“Siwezi kulindwa kwa sababu mimi sijafikia hatua
ya kulindwa na silaha, mtu akiamua kufanya jambo au kitu chake anafanya tu hata
ulindwe kwa saa 24 atafanya tu ndani ya dakika hata 5 au sekunde".
alisema Chuchu Hansy
Aidha Chuchu Hansy ameongeza kuwa hawezi kumzungumzia
baba watoto wake kuwa anafanya hivyo labda aulizwe mwenyewe.
"Siwezi kumuongelea kwa sababu ana vitu
vyake, vingine ambavyo siwezi kuvizungumzia ni vizuri mkimuona mumuulize hilo
swali, kama anayo au hana atawaonesha, sisi Watanzania hatuna desturi ya
kulindana, hivyo nitaishi maisha ambayo Nchi yangu inaruhusu" aliongeza.
Juice Wrld avunja rekodi hii
Baada kifo chake mwishoni mwa wiki , Rapa Jarad Anthony Higgins ‘Juice Wrld’ kutoka
Marekani, ashika rekodi ya kusikilizwa zaidi mtandaoni kwa muda mfupi.
Imeelezwa kuwa, kazi za rapa huyo zimesilikizwa
mara nyingi zaidi mtandaoni.
Twakimu zinasema rapa huyo amesikilizwa mara
milioni 38.2 (streamed 38.2 million times) baada ya kifo chake kilichotokea
siku ya Jumapili.
Aidha, imeendelea kueleza kuwa, kusikilizwa kwa
kazi zake kulipanda maradufu hadi kufikia 487% na kumfanya kuwa msanii
aliyesikilizwa mara nyingi zaidi kwa muda mfupi.