Rais Magufuli amteua Profesa Florens Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu
Rais Dk John Magufuli amteua Profesa Florens Luoga kuwa Gavana wa Benki Kuu Tanzania. Amtaka Gavana wa sasa Beno Ndulu kuanza utaratibu wa kukabidhi ofisi haraka.
Rais Magufuli alifanya uteuzi huo wakati wa kutunuku vyeti vya pongezi maalum wajumbe wote waliohusika kuchunguza kiwango, aina na thamani ya madini katika makinikia.
Kabla ya uteuzi huo, Profesa Luoga alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA). Akihutubia Taifa baada ya kuwatunuku wajumbe hao, Rais Magufuli amewaonya watu wanaopotosha takwimu rasmi za serikali na kutoa za uongo.
Kutokana na tabia hiyo ya baadhi ya watu, Rais amemwagiza Waziri wa Katiba pamoja na vyombo vya dola kuwachukulia hatua watu wanaopotosha takwimu wakati ukweli wanaujua.
"Vita ya kupigania rasilimali za nchi ni ngumu sana, ninapata shida kubwa kutokana na kuongoza vita hii, inaniumiza sana lakini nimetumwa na Watanzania kuifanya kazi hii kwa moyo wangu wote" Rais Dk John Magufuli Rais Magufuli amewashutumu watu wanaopinga juhudi za serikali za kutetea rasilimali za nchi akisema wanapigania matumbo yao "Wanaopinga juhudi za serikali za kupigania rasilimali za nchi wanatetea pesa walizoahidiwa na wezi wa rasilimali zetu" Rais Dk John Magufuli, Ikulu, Dar es Salaam.
Rais Magufuli ashukuru vyama vya upinzani kwa kuruhusu wanachama wao kuwepo katika kamati za madini kwa sababu maendeleo hayana vyama. Asema fedha zikiongezeka hata ruzuku za vyama zitaongezeka