FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

NDEGE ZA ISRAEL ZA SHAMBULIWA NA WAPELESTINA WA UPANDE WA GAZA


Ndege za kivita za utawala wa Kizayuni wa Israel zimeshambulia makazi ya Wapalestina wa Gaza usiku wa kuamkia leo na kujeruhi watu kadhaa.
Kwa mujibu wa duru za Hospitali ya Shifa katika Ukanda wa Gaza, mtu mmoja ambaye yuko katika hali mahututi ni miongoni mwa majeruhi watatu wa shambulizi hilo la anga la ndege za kijeshi za Israel.
Utawala huo pandikizi unadai kuwa umetekeleza hujuma hiyo dhidi ya ngome za wanachama wa Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina Hamas, eti kulipiza kisasi cha kufyatuliwa roketi kwenda upande wake kutoka eneo hilo.
Jeshi katili la Israel limefanya shambulizi hilo la anga katika hali ambayo, mwezi uliopita Umoja wa Mataifa ulitahadharisha kuwa, eneo la Ukanda wa Gaza huenda lisifae tena kwa ajili ya maisha ya mwanadamu baada ya miaka karibu 10 ya mzingiro wa pande zote wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
Takwimu za Umoja wa Mataifa pia zinaonesha kuwa, asilimia 95 ya maji ya Ukanda wa Gaza hayafai kwa ajili ya matumizi ya mwanadamu, na huduma ya umeme inatolewa kwa masaa mawili tu kwa siku.
Eneo hilo lenye idadi ya Wapalestina milioni mbili limekuwa chini ya mzingiro wa anga, nchi kavu na baharini wa jeshi la utawala katili wa Israel kwa miaka 10 sasa. Israel imezuia kuingizwa bidhaa zote za dharura kama chakula, dawa na maji katika eneo hilo na wagonjwa wengi wamekuwa wakifariki dunia kila uchao katika Ukanda wa Gaza kutokana na ukosefu wa dawa na huduma za afya.