HALMASHAURI za Wilaya za Mikoa ya Kanda ya Mashariki inayoundwa na Tanga, Pwani, Dar es Salaam na Morogoro ambazo hushiriki maonesho ya kilimo, mifugo na uvuvi (Nanenane), zimeshauriwa kuanzisha ngazi ya kata na wilaya.
Hii ni kuiwezesha elimu
inayotolewa na wataalamu kwa wakulima na wafugaji kuhusu teknolojia ya kilimo,
ufugaji, mbegu bora na matumizi ya pembejeo za kisasa iwafikie wakulima wengi
zaidi waliopo vijijini.
Katibu Tawala wa Mkoa wa
Morogoro, Clifford Tandari alibanisha hayo juzi wakati akizungumza na waandishi
wa habari pamoja na wataalamu wa sekta za kilimo, mifugo na uvuvi kwenye Uwanja
wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Katibu Tawala wa mkoa huyo
pia alishauri mikoa ya kanda hiyo baada ya kumalizika kwa maonesho hayo ni
vyema kufanyika katika onesho la Kilimo kwa kushindanishwa mkoa kwa mkoa ili
kupata wakulima na wafugaji mahiri ambao wanaweza kuingia kushindana.