Wasanii waaswa kutumia mwezi mtukufu wa Ramadhani kuombana msamaha
msanii wa filamu nchini Tanzania, Steve Mengele ‘Steve Nyerere’ amewataka wasanii wa filamu nchini kutumia mwezi mtukufu wa Ramadhan kuombana msamaha pale walipokoseana na kusameana.
Akiongea na mtandao wa hivisasa katika mahojiano maalum, Steve amesema haoni haja ya wasanii kuendelea kulumbana hasa katika mwezi huu mtukufu wa toba kwani haileti picha nzuri kwa jamii inayotuzunguka na kutufatilia kuona kila siku tunakoseana.
“Nawaomba wasanii wenzangu kwa ujumla pamoja na mashabiki zetu tusameane kwakuwa tunajenga nyumba moja hivyo hatupaswi kugombea fito,” amesema.
Kauli hiyo imekuja baada ya Steve Nyerere kupishana na wasanii wenzake hivi karibuni wakati wa maandamano ya kupinga filamu za nje kuingizwa nchini na kama zitaingiizwa zifate utaratibu wa kulipa kodi ili waende sawa na wao.
Mwezi mtukufu wa Ramadhan ni mwezi unaotumiwa na watu wengi katika jamii kuombana msamaha.