Jini Kabula akanusha kuiba mume wa mtu.
Msanii wa Filamu nchini, Jini Kabula aliyetamba na tamthilia ya ‘Jumba la Dhahabu’ amekanusha vikali kuhusika na tuhuma za kuiba mume wa mtu.
Kabula amesema hayo alipokuwa akipiga stori na mtandao wa hivisasa na kudai kuwa hajaishiwa wanaume hadi kwenda kuchukua mume wa mtu.
,Kwani anachokiamini yeye ni kuwa mpenzi aliyenaye si mume wa mtu.
“Siitaji maneno na chokochoko maana naona nafatiliwa kila kukicha kuwa naiba mume wa mtu, kitu ambacho hakina ukweli ndani yake. Ninachoamini ni kuwa mpenzi niliyenaye sio mume wa mtu,” amesema.
Aidha, amewataka mashabiki wake kuzidi kumuunga mkono katika kazi zake na kuachana na uvumi huo.