Pancho mwamba aja na mwarobaini wa kuurudisha muziki wa Dans
wanamuziki wa Bendi ya Fm Academia Pancho Mwamba
Msanii wa muziki wa bendi toka kundi la Fm Academia wazee wa Ngwasuma Pancho Mwamba amewapa somo wasanii wanaotumia kiki na skendo sasa ili kuinua muziki wa dansi.
Akiongea na kituo kimoja cha runinga ,Pancho amesema haoni haja ya kutafuta kiki na skendo ili kuinua soko la muziki wa dansi kwani jitihada pamoja na ubora wa kazi ndio njia pekee ya kurudisha mashabiki.
“Sioni haja ya wasanii wa bendi kutafuta kiki na skendo wakizani ndio njia pekee ya kurudisha heshima ya muziki wa dansi nchiini “Alisema Pancho.
Hali hiyo inajitokeza kwa sasa kutokana na muziki wa dansi kukosa mashabiki wengi katika shoo hali ambayo inawapa hofu wasanii.
“Nawaomba mashabiki zangu wote wazidi kutupa maoni na ushauri pia nasi wasanii tuzidi kubadilisha mfumo wa kazi tuliokuwa tunatumia zamani ili kurudi katika soko”, alisema Pancho.