FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

Namna viazi vitamu vilivyo mkombozi wa wakulima Gairo




VIAZI vitamu ni moja kati ya mazao makuu ya mizizi nchini Tanzania kwa ajili ya chakula. Ni zao linalotajwa kuvumilia ukame. Asili yake ni Amerika ya Kati na ya Kusini na kwa hapa Tanzania, zao hili hulimwa zaidi katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Dodoma, Kagera, Arusha, Ruvuma na Morogoro.
Viazi vitamu hutumika kama chakula kwa kutayarishwa katika njia mbalimbali. Unga wa viazi vitamu hutumika kutengeneza keki, maandazi, kalimati na tambi. Majani ya viazi huliwa kama mboga pia hutumika katika kutayarisha mboji.
Kuna aina nyingi za viazi vitamu zinazolimwa ulimwenguni na kwamba hapa nchini Tanzania aina zinazolimwa zaidi ni Ukerewe, Simama, Kakamega, Karoti C, Mwananjemu, Ali mtumwa mayai, Mavuno, Pananzala, Kibakuli, Sinia,Vumilia na Polista.
Wilaya ya Gairo iliyopo mkoani Morogoro pia ni miongoni mwa maeneo yanayozalisha zao hili. Linatajwa kuwa ni la pili kwa kuzalishwa na wananchi wake likitanguliwa na zao la mahindi na limekuwa ni la biashara zaidi katika kukuza pato lao kiuchumi kwa waishio mijini na vijijini.
Uzalishaji huu kwa wingi katika wilaya ya Gairo ni kutokana na hali ya hewa na upatikanaji wa mvua si za kutosha na kuvumilia ukame tofauti na mazao mengine. Wananchi wa wilaya ya Gairo ambao asilimia kubwa ni Wakaguru amelipa jina la kikabila la zao hilo kuwa ni ‘Mandoro’ ambapo wamekuwa wakizalisha aina tofauti ya viazi vitamu na kusafirisha nje ya wilaya na kuuzwa sehemu mbalimbali ndani ya wilaya hii.
Mkuu wa wilaya ya Gairo, Seriel Mchembe anaonesha takwimu za malengo na utekelezaji wa kilimo mwaka 2015/ 2016 kwa mazao aina sita likiongozwa na la mahindi na kufuatiwa na viazi vitamu.
Wilaya hii ni kati ya wilaya saba za mkoa wa Morogoro na ina jumla ya kilometa za mraba 1,851.34. Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, inaonesha wilaya ina wakazi 193,011, kati yao wanaume ni 93,206 na wanawake ni 99,802.
Kulingana na matokeo ya idadi ya watu yaliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu, kuwa mwaka 2016 Wilaya inakadiriwa kuwa na wakazi 213,802 kati ya hao wanaume 103,246 na wanawake 110,556.
Hivyo kutokana ongezeko la idadi ya watu na kukosekana kwa zao kuu la biashara, wananchi wa wilaya hii licha ya kuzalisha mahindi, maharage, alizeti, mbaazi na miwa kwa kiwango kidogo, nguvu kubwa wamezielekeza kwenye kilimo cha zao la viazi vitamu.
“Tumeendelea kuhamasisha kilimo cha mazao mbalimbali kwa kufuata kaulimbiu ya mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe kwa kila kaya ilime heka mbili zao la chakula na heka moja mazao ya biashara wengi wamejikita kweye zao hili la viazi vitamu,” anasema Mchembe.
Anasema, vile vile hamashauri ya wilaya ya Gairo imewezesha kuhamasisha wakulima juu ya matumizi ya mbegu bora na kutumia zana bora za kilimo. “Mvua zinazoendelea kunyesha zimewawezesha wakulima kupanda mazao mbalimbali hususani mahindi, mtama, mihogo ulezi, mbogamboga na viazi vitamu,” anasema Mchembe.
Anasema malengo ya uzalishaji yamekuwa yakitimia na hata kuvuka. Kwa mfano, lengo la msimu wa mwaka 2015/2016 ilikuwa ni kulima heta 8,756 za viazi na mavuno yalitarajiwa kuwa tani 21, 044.
Katika mwaka wa 2016/2017 malengo la uzalishaji wa zao hili ilikuwa ni hekta sawa na msimu uliotanguliwa lakini matarajio ya mavuno ni tani 30,024. Zao hili la viazi vitamu limepewa umuhimu katika kukuza uchumi wa wilaya na kuinua pato la wananchi.
Uongozi wa wilaya umelipa kipaumbe kwa kuwahamasisha wakulima waongeze kasi ya uzalishaji wake ili liwanusuru kimaisha. Mchembe anasema, wananchi wa wilaya ya Gairo kwa sasa wanajituma kuongeza uzalishaji mali katika kilimo, ufugaji na biashara.
Baadhi ya wakulima wa viazi wilayani hapa, wanakiri kunufaika na kilimo cha zao hili wakisema ni mkombozi kwao. Mkazi wa Gairo, Muhando Peter anasema kuwa kabla ya kushamiri kwa kilimo hicho wakulima wengi walikuwa wakitegemea mahindi pekee.
Anasema kuwa hivi sasa plastiki kubwa ya viazi vitamu linauzwa kati ya Sh 4,000 na 5,000, wakati gunia aina ya kiroba linauzwa wastani wa Sh 60,000. Anasema kuwa, zao hilo ndiyo tegemeo kubwa katika familia kwa chakula na biashara hivyo wananchi wamelipa kipaumbele cha kwanza sambamba na mahindi.
Anatoa mfano wa kipindi hiki cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani akisema, zao hili lina walaji wengi jambo ambalo ni faida kwa wakulima