FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

Rais magufuri kukabidhiwa taarifa ya kkamati ya pili ya madini ijumatatu








Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli atapokea taarifa ya Kamati ya Pili ya wachumi na wanasheria iliyofanya uchunguzi wa madini yaliyo katika makontena yenye mchanga yaliyo katika sehemu mbalimbali nchini Jumatatu, Tarehe 12 Juni 2017, jijini Dar es Salaam.

Kamati hiyo inatarajiwa kutoa tathmini ya hasara ambayo Tanzania imeingia kutokana na mikataba ya madini, athari za kiuchumi ambazo Tanzania imezipata kutokana na mikataba ya madini na ushauri wa kisheria wa namna bora ya kuendesha migodi ya madini ambayo badala ya kuneemesha watanzania imekuwa chanzo cha umasikini kwa wananchi.
Hongera Rais kwa uamuzi wa kuwakomboa watanzania. Tukio hilo litarushwa hewani moja kwa moja (Mubashara) na vyombo mbalimbali vya radio na televisheni pamoja na mitandao ya kijamii, ikiwemo Daily News Online, Habarileo Onli