WATU 13 wameuwawa na wengine hawajulikani walipo kwenye jimbo la Maluku
Kaskazini mwa Indonesia baada ya mafuriko makubwa kulikumba eneo la mashariki
mwa visiwa hivyo.
Shirika la
utafutaji na uokoaji la Indonesia Basarnas lilisema kwamba mvua kubwa ilionyesha
tangu jana Jumamosi ilisababisha mafuriko makubwa katika kisiwa cha Ternate na
kwamba kikosi cha uokoaji bado kinaendeleza juhudi za kuwaondoa waathiriwa.
Vyombo vya habari nchini
humo viliripoti kwamba watu 11
wamefariki kufuatia mkasa huo lakini afisa wa shirika la
Basarnas hakuthibitisha idadi hiyo ya vifo.
Itakumbukwa kuwa mnamo
mwezi Mei takriban watu 60 waliuwawa kutokana na mafuriko na maporomoko ya
matope katika mkoa wa Sumatra magharibi mwa Indonesia.
Wizara ya
afya nchini Uganda imethibitisha visa vingine viwili vya virusi vya homa ya
nyani mpox na kuongeza idadi ya walioambukizwa kuwa watu wanne, katika taifa
hilo la Afrika Mashariki.Mkuregenzi
Mkuu wa huduma ya afya nchini humo Henry Mwebesa aliliambia shirika la reuters
kwamba, wagonjwa hao wawili wapya wanasemekana kuambukizwa kirusi cha Clade
b1.
Wagonjwa hao ambaye mmoja ni dereva wa lori kwa sasa wamewekwa
karantini katika hospitali moja iliyoko Entebbe.
Shirika la afya duniani WHO lilitangaza mripuko wa hivi karibuni
wa Mpox kuwa dharura ya afya ya umma baada ya kirusi hicho kipya kinachodaiwa
kuambukiza kirahisi na kwa kasi kugundulika.
Uganda iliripoti kisa cha kwanza Julai 24 wakati vipimo
kutoka kwa maabara, vya wagonjwa wawili katika hospitali moja inayopakana na
Jamhuri ya kidemkrasia ya Kongo kugunduliwa kuambukizwa homa hiyo.
Takriban mtu mmoja ameuawa baada ya Urusi kuzindua wimbi la ndege zisizo na rubani 28 dhidi ya mji mkuu wa Ukraine Kyiv asubuhi ya leo. Vitali Klitschko, meya wa Kyiv, alisema kwenye ujumbe wa Telegraph
"Asubuhi, ndege zisizo na rubani 28 ziliruka kuelekea Kyiv, Shukrani kwa vikosi vyetu vya kijeshi na ulinzi wa anga, magaidi wengi waliokuwa wakiruka walipigwa risasi. Jumla ya milipuko mitano ilisikika huko Kyiv.
Mmoja wao yuko katika jengo la makazi katika wilaya ya Shevchenkiv. Waokoaji wanaendelea kuzima miundo ya jengo hilo na kufanya kazi ya kubomoa vifusi. Hapo awali, wakaazi 18 wa jengo hilo waliokolewa. Wawili walikuwa chini ya kifusi. Mwili wa mwanamke aliyekufa ulipatikana hivi karibuni.
Kulingana na data ya awali, mtu mmoja zaidi yuko chini ya vifusi. Shughuli za utafutaji na uokoaji zinaendelea.Hapo awali Klitschko alisema kuwa watu watatu wamelazwa hospitalini.
Taarifa zaidi zinasema takriban watu watatu wameuawa na wengine watatu wamelazwa hospitalini baada ya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani za Kamikaze katika mji mkuu wa Ukraine wa Kyiv.
Meya Vitali Klitschko alisema mwanamke aliyekufa alipatikana kutoka kwenye vifusi vya nyumba katika wilaya ya Shevchenkiv, ambapo mlipuko umetokea kutokana na shambulio la ndege isiyo na rubani.
Mtu mwingine yuko chini ya vifusi, aliongeza. Shughuli za utafutaji na uokoaji zinaendelea. Afisa mmoja alisema kuwa watu 19 walikuwa wameokolewa. Klitschko alisema kuwa kumekuwa na milipuko mitano baada ya ndege 28 zisizo na rubani kuelekezwa katika jiji hilo.
Waziri Mkuu wa Ukraine, Denys Shmyhal alisema "Leo, Urusi ilishambulia tena vituo vya kiraia na nishati nchini Ukraine. Jengo la ghorofa huko Kyiv ni miongoni mwa malengo ya magaidi. Watu wamejeruhiwa. Mwitikio wa ulimwengu kwa uhalifu huu lazima uwe wazi: msaada zaidi kwa Ukraine na vikwazo zaidi dhidi ya mchokozi.
Mshauri wa rais wa Ukraine Mykhailo Podolyak alisema baada ya wimbi jipya la mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwamba Urusi inapaswa kufukuzwa kutoka kundi la G20.
Iran ilisema tena Jumatatu kwamba haijaipatia Urusi ndege zisizo na rubani za kutumia nchini Ukraine. "Habari zilizochapishwa kuhusu Iran kuipatia Urusi ndege zisizo na rubani zina malengo ya kisiasa na zinasambazwa na vyanzo vya magharibi. Hatujatoa silaha kwa upande wowote wa nchi zilizo kwenye vita," msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Nasser Kanaani alisema.
Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell alisema umoja huo "utatafuta ushahidi madhubuti" kuhusu ushiriki wa Iran katika vita vya Urusi dhidi ya Ukraine.
Kiongozi wa Ukraine aliishutumu Urusi kwa kujaribu kufedhehesha Umoja wa
Mataifa kwa kufyatua makombora katika mji wa Kyiv wakati wa ziara ya Katibu Mkuu
António Guterres, shambulio ambalo lilisambaratisha mpango wa mji mkuu kurejea
katika hali ya kawaida huku mwelekeo wa vita hivyo ukielekea mashariki.
Rais Volodymyr Zelenskyy alisema vikosi vya Ukraine vinazuia majaribio ya
Urusi kuelekea kusini na mashariki, huku juhudi zikiendelea kuwalinda wakaazi
wa Mariupol, ambao kwa kiasi kikubwa wameharibiwa na kuzingirwa kwa muda wa
miezi 2.
Urusi ilishambulia maeneo yote ya Ukraine siku ya Alhamisi, ikiwa ni pamoja
na shambulio dhidi ya Kyiv ambalo lilishambulia eneo la makazi na jengo
jingine.
Meya Vitali Klitschko alisema ijumaa kuwa mwili mmoja ulipatikana kwenye
vifusi vya shambulio hilo. Watu kumi walijeruhiwa, ikiwa ni pamoja na angalau
mmoja ambaye alipoteza mguu, kulingana na huduma za dharura za Ukraine.
Katika kumbukumbu dhahiri ya mgomo huo huo, Wizara ya Ulinzi ya Urusi
ilisema Ijumaa kwamba ilikuwa imeharibu "majengo ya uzalishaji"
katika kiwanda cha ulinzi cha Artem huko Kyiv. Shambulio la kijasiri zaidi la
Urusi katika mji mkuu huo tangu vikosi vya Moscow kurudi nyuma wiki chache
zilizopita zilikuja saa moja baada ya Zelenskyy kufanya mkutano na waandishi wa
habari na Guterres, ambaye alitembelea baadhi ya uharibifu ndani na karibu na
Kyiv na kulaani mashambulizi dhidi ya raia.
"Hii inasema mengi kuhusu mtazamo wa kweli wa Urusi kwa taasisi za
kimataifa, kuhusu majaribio ya mamlaka ya Urusi kufedhehesha Umoja wa Mataifa
na kila kitu ambacho shirika hilo linawakilisha," Zelenskyy alisema katika
hotuba ya video ya usiku mmoja kwa taifa.
"Kwa hivyo, inahitaji majibu
yenye nguvu sawa." Lengo moja la ziara ya Guterres lilikuwa kuokoa watu
kutoka katika mji wa bandari wa Mariupol ulioharibiwa, ulioko kusini mwa mji wa
Mariupol, ikiwa ni pamoja na vyuma vilivyobomoka ambapo walinzi wa Ukraine
wamejificha na mamia ya raia pia wanajihifadhi, Haijulikani ikiwa imezaa
matunda.
"Siwezi kuthibitisha maelezo kamili ya operesheni hiyo ili kuhakikisha
kuwa inafanywa kwa usalama kwa watu wetu na kwa raia waliokwama huko
Mariupol" alisema Saviano Abreu, msemaji wa ofisi ya kibinadamu ya Umoja
wa Mataifa. Ofisi ya Zelenskyy ilisema mazungumzo yanaendelea na upatanishi wa
Umoja wa Mataifa, na haikuondoa kwamba uhamishaji wa mtambo huo unaweza kutokea
Ijumaa.
Afisa huyo alizungumza kwa sharti la kutotajwa jina kwa sababu
hawakuruhusiwa kuzungumza na vyombo vya habari.
Timu
ya Umoja wa Mataifa imetua nchini Msumbiji kusaidia maelfu ya watu ambao
wameadhirika na dhoruba ya Tropical Ana, ambayo ilitokea katika mikoa ya kati
na Kaskazini mwa nchini mapema wikii hii.
Kulingana
na ripoti za vyombo vya habari, upepo mkali na mvua kubwa ndizo zimesababisha
mafuriko hayo ambapo imepelekea vifo vya watu na uharibifu wa vitu vingi.
Nchini
humo dhoruba hiyo ilipiga katika maijimbo ya Nampala, Tete,Nissa, Sofalana na
Manica, zaidi ya nyumba 10,000 zilihalibiwa pamoja na madaraja, nyaya za umeme,
Shule, vituo vya afya, mifumo ya maji na miundombinu mingine ya umma.
Hata
hivyo mamlaka za mtaa zilisema kuwa takribani
vituo vya afya 12 na shule 137 zimeharibiwa vibaya, wanafunzi 27,300 hawana sehemu ya kujifunzia
ambapo wikii ijayo shule zinatajiwa kuanza.
Kutokana
na adhari kubwa hiyo kwa mjibu wa UNICEF
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto ilisema kuwa zaidi ya watu
45,000 wakiwemo wanawake na watoto 23,000 huenda wakahitaji msaada wa
kibiandadmu kwa haraka.
UNICEF
imepeleka wafanyakazi na kuandaa vifaa vya matibabu na lishe, maji,vyoo na
vifaa vya usafi vilevile pamoja na kuweka muda wa kujifunzia ili kusaidia
watoto na familia zao, shirika hilo linakadiriwa kuhitaji zaidi ya dola milioni
3.5 kwa ajiri ya msaada huo.
Maria Luisa Fornara, Mwakilishi wa UNICEF nchini Msumbiji alisema kuwawanafanya kazi pamoja na Serikali na washirika wengine ili kuhakikisha watoto na familia zao wanapata msaada wa kuokoa maisha yao.
“Dhoruba hii imeleta adhari kubwa nchini hasa watoto wameadhirika pakubwa” alisema Fornara.
Msumbiji kwa sasa iko katika msimu wa mvua na Umoja wa Mataifa ilisema kuwa inahofia ikiwa hali nyingine itatokea tena kwani itatasababisha adhari kubwa zaidi.
Tume ya Uchaguzi nchini Kenya
imetangaza kuahirishwa kwa uchaguzi wa marudio katika majimbo manne
magharibi mwa nchi hiyo ambayo ni ngome ya kiongozi wa upinzani Raila
Odinga aliyetoa wito kwa wafuasi wake kususia uchaguzi wa leo.
Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi wakati wa makabiliano kati ya polisi na wafuasi wa upinzani katika maeneo hayo.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amesema tume imechukua hatua hiyo baada ya upigaji kura kutatizwa na ukosefu wa usalama.
Katika
majimbo hayo ya Kisumu, Siaya, Migori na Homa Bay, wafuasi wa upinzani
walifunga barabara za kuelekea katika vituo vya kupigia kura na
kukabiliana na maafisa wa polisi siku yote.
Katika baadhi ya
maeneo, makarani na maafisa wengine wa kupigia kura hawakufika vituoni
kutokana na kile mmoja wa wasimamizi alisema ni kuhofia usalama wao.
Serikali ilikuwa imewatuma maafisa wa polisi katika maeneo mbalimbali kushika doria.
Gavana
wa jimbo la Kisumu Prof Anyang' Nyongo amewatuhumu polisi kwa kutumia
"magenge ya watu" kuwashambulia wafuasi wa upinzani.
Ameambia BBC kwamba watu wawili wamefariki eneo lake na wengine 29 wanauguza majeraha.
Prof Nyong'o amesema hawataruhusu uchaguzi wa marudio ufanyike katika kaunti hiyo.
"Nimetangaza
kama gavana wa hii kaunti wiki moja ya maombolezi ambapo wakati huo
hakutakuwa na sherehe. Kwetu uchaguzi huwa ni sherehe," amesema.
Amesema iwapo tume hiyo itaendelea kusisitiza uchaguzi ufanyike, basi wataenda kortini kutaka uzuiwe.
Wapiga kura wachache kujitokeza
Ni wapiga kura wachache waliojitokeza kupiga kura leo ikilinganishwa na uchaguzi wa kwanza uliofanyika tarehe 8 Agosti.
Rais Kenyatta, ambaye anatarajia kuibuka mshindi, alikuwa amewahimiza wapiga kura kujitokeza kwa wingi.
Mpinzani wake mkuu Bw Odinga hata hivyo alikuwa amesema uchaguzi huo si wa kuaminika na kuwataka wafuasi wake kutoshiriki.
Uchaguzi
wa leo ulitokana na hatua ya Mahakama ya Juu ya kufuta matokeo ya
uchaguzi huo wa Agosti kutokana na kesi iliyowasilishwa na Bw Odinga.
Mahakama hiyo ilisema uchaguzi huo ulijaa kasoro nyingi ambazo kuna uwezekano ziliathiri matokeo.
Usalama kudumishwa
Maelfu
ya maafisa wa polisi, wakisaidiwa na maafisa kutoka idara nyingine za
usalama, walikuwa wametumwa kudumisha usalama katika vituo vya kupigia
kura kote nchini humo pamoja na kutoa ulinzi wa wapiga kura.
Vituo
vya kupigia kura vilifungwa saa kumi na moja jioni, ingawa katika
baadhi ya maeneo ambayo vituo vilichelewa kufunguliwa muda wa kufunga
vituo uliongezwa.
Bw Chebukati alisema ingawa upigaji kura
uliendelea vyema katika baadhi ya maeneo, kuna maeneo yaliyoathiriwa na
hali ya usalama pamoja na mvua kubwa iliyonyesha maeneo mengi na
kutatiza usafiri.
Makundi mengi ya waangalizi wa kimataifa yalikwua yamepunguza idadi ya waangalizi kutokana na wasiwasi wa kiusalama.
Matokeo
ya kutoka vituo vya kupigia kura, yaliyo kwenye fomu zifahamikazo kama
Fomu 34A, yamekuwa yakipakiwa katika mtandao wa tume hiyo.
Matokeo ya jumla ya matokeo ngazi ya maeneo bunge ambayo hutolewa kupitia Fomu 34B yanatarajiwa kutolewa baadaye.
Tume ina hadi siku saba kutangaza matokeo ya jumla ya urais, ambayo hutangazwa kupitia Fomu 34C.
Rais uhuru kenyata akitoka kupiga kura
Kuchoshwa na siasa
Baada ya kupiga kura Gatundu, Bw Kenyatta alisema wakati umefika kwa taifa kusonga mbele.
"Tumechoshwa na kuwa katika kipindi cha uchaguzi. Ni wakati wa kusonga mbele," alisema.
Aliongeza pia kwamba maeneo mengi nchini humo usalama ulidumishwa.