FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

JUVENTUS YAPOTEZA MATUMAINI KUMSAJILI NYOTA WA CHELSEA

 

                                       Mchezaji wa Chelsea, Antonio Rudiger.  picha na mtandao.


Juventus huenda ikamkosa beki wa Chelsea Antonio Rudiger msimu huu wa joto. Miamba hiyo ya Serie A imekuwa ikihusishwa sana na uhamisho wa Mjerumani huyo, ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.

Kwa mujibu wa Tuttomercatoweb, Barcelona inaaminiwa kuwa mbele ya Juventus katika mbio za kumsajili Antonio Rudiger.

Antonio Rudiger alijiunga na Chelsea kutoka AS Roma mwaka 2017 katika mkataba wenye thamani ya pauni milioni 27. Amechukua mchezo wake kwa kiwango kingine tangu Thomas Tuchel alipochukua mikoba katika klabu hiyo mnamo Januari 2021.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 alikuwa na jukumu muhimu katika ushindi wa Chelsea katika Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita na ushindi wao wa Kombe la Dunia la FIFA msimu huu. Amekuwa katika hali nzuri kwa upande wa Tuchel na anachukuliwa kuwa mmoja wa mabeki bora katika Ligi Kuu ya England. Beki huyo amecheza mechi zaidi ya 190 katika klabu hiyo na amefunga mabao 11.

Antonio Rudiger ameripotiwa kufikia makubaliano na Chelsea kuhusu mkataba mpya na Christian Falk. Hata hivyo, The Blues hawawezi kuongeza mikataba ya wachezaji wao wowote kutokana na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa kwa mmiliki wao wa Urusi Roman Abramovich na serikali ya Uingereza.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani anatarajiwa kuwa mchezaji huru msimu huu wa joto. Barcelona inaripotiwa kumuona kama mbadala wa Ronald Araujo.

Mkataba wa Araujo na klabu hiyo ya La Liga unatarajiwa kumalizika mwaka 2023. Mpaka sasa amekataa fursa ya kuongeza mkataba wake na klabu hiyo. Barcelona inaweza kuchagua kumuuza kijana huyo msimu huu badala ya hatari ya kumpoteza kwa uhamisho wa bure mwaka ujao.

Juventus, kwa upande mwingine, inamuona Rudiger kama mbadala bora wa beki mkongwe Giorgio Chiellini kwa mujibu wa The Sun.

Miamba hiyo ya Italia imekuwa na mpango wa kumsajili Antonio Rudiger. The Blaugranas wanaaminika kuwa tayari wamewasilisha ofa kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29.