Wayne Rooney.
Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney amekiri kuwa na kiburi mara baada ya Sir Alex Ferguson alipojaribu kumsajili, meneja huyo wa Derby County alifichua kuwa Red Devils walijaribu kumsajili alipokuwa na umri wa miaka 14 pekee.
Rooney alikataa ofa hiyo ili abaki
na timu yake ya utotoni Everton, alisema Sir Alex Ferguson alijaribu kumsajili
alipokuwa na umri wa miaka 14. Alex aliongea na wazazi wake Rooney kwenye simu
na kumpa taarifa ya kuwa mwanao kuhitajika Manchester lakini Rooney hakuwa
tayari kwa muda huo.
Kauli ya Rooney alisema kwamba yeye anahitaji kubaki Everton. “Alex alizungumza kwenye
simu na mama na baba yangu. Alex alisema,
Manchester United wanataka kukusajili.’
Nikasema, ‘Mwambie aondoke. Nataka kuichezea Everton,
Kisha, kadiri muda ulivyosonga, nilijua kwamba nilipaswa kumchezea Alex
Ferguson, sababu ya mimi kusajiliwa na United ilikuwa Alex Ferguson.” Alisema Rooney.