FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

TAMBO ZA HAJI MANARA

 

Awali alipokuwa ndani ya Simba kabla ya kubwaga manyanga aliwahi kuweka wazi kuwa timu hiyo ya Simba ilikuwa ni namba moja kwa kutwaa mataji mengi ila kwa wakati huu anasema kuwa Yanga ni mabingwa mara nyingi.

Manara ameweka wazi kuwa huwezi kusema kuwa Simba amechukua Kombe ubingwa mara sita wakati Yanga amechukua mara tano wakati kuna data nyingine ambazo hazijawekwa.

"Mabingwa wa muda wote ndani ya Tanzania ni Yanga, hizo namba zote ambazo unaziona nilizitengeneza mwenyewe, hivyo haziwezi kunitisha kabla ya kujiondoa.

"Ikiwa utaweka orodha ya mabonanza pamoja na mambo mengine basi Yanga inaweza kuwa na mataji bilioni ambayo tumeyatwaa hivyo hakuna namna kwa fact, (ukweli) sisi tunaongoza kwa kutwaa mataji mengi.

"Achana na porojo za nyuma kwa fact Yanga ina mataji mengi kuliko klabu yote Tanzania, nilifanya makosa ya kudangaya,".