FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

AHIFADHI MWILI WA MAMAKE KWA ZAIDI YA MWAKA MMOJA ILI KUPOKEA PENSHENI YAKE

 

 

Mwanamume aliweka maiti ya mama yake ndani ya chumba cha chini kwa zaidi ya mwaka mmoja wakati akiendelea kupokea malipo yake ya pensheni, polisi wa Austria wanasema.

Mwanamke huyo wa miaka 89, ambaye inasemekana alikuwa na ugonjwa wa shida ya akili-dementia anadhaniwa kufa kwa sababu za kawaida mnamo Juni mwaka jana.

Mwanawe, mwenye umri wa miaka 66, anasemekana kuweka mwili wake ndani ya sanduku na kutumia vifurushi vya barafu na bandeji kuzuia harufu hiyo.

Polisi wanaamini anaweza kuwa amepokea malipo kinyume cha sheria ya karibu € 50,000 (£ 42,000).

Ulaghai wake uligunduliwa tu baada ya tarishi mpya aliyekuwa amewasilisha mafao ya mwanamke huyo katika mkoa wa magharibi wa Tyrol kuzuiwa kumwona, polisi ilisema katika taarifa.

Hilo lilisababisha uchunguzi, na kupelekea ugunduzi wa kilichofanyika baadaye .

Polisi wanasema kuwa mtu huyo hakuwa na mapato mengine, na alikuwa amewaambia kuwa malipo yangekoma mara moja ikiwa angetoa habari za kifo cha mamake

Mshukiwa pia alisema alikuwa amemwambia kaka yake kwamba mama yao alikuwa akipatiwa huduma hospitalini, na kwamba haikustahili kumtembelea kwani hali yake ilimaanisha haingewezekana kumtambua, iliripoti ORF.