Walisema walombi penye miti hapana wajenzi, ila pia wakapiga soga wakaongezea jungu kuu halikosi ukoko. Kwanini niseme penye miti hapana wajenzi? Rich Mavoko ni miongoni mwa mastaa ambao wamekua wakiiwakilisha Tanzania vyema kwa mda ila Watanzania mbona tunamuchukulia poa? Kama kijana mwengine yule wakitanzania amekua akihaha angalau kupitia kipaji chake kujikimu kimaisha pia kuiwakilisha Tanzania kimataifa.
Ari hii ilimfanya pia wakati flani akakimbilia nchini Kenya nakutafuta nafasi chini ya mwavuli wa kaka Empire wakati akianza muziki, kabla ya msanii mwenza na mwenye kupenda maendeleo Diamond Platnumz kuamua kumpa nafasi na akamsajali chini ya lebo yake ya WCB.
Ila kama tujuavyo, mtoto akikua lazima atoke na aende kujenga nyumba yake mbali na wazazi wake, je niharamu kijana aliebalekhe kuanza maisha mbali na wazazi wake? Mbona majirani wamuchukie, wamusute na kumudhihaki. Watanzania hii si hulka yetu, tokea enzi za Mwalimu Nyerere hadi sasa Anko Magu. Sitaki kuongolea sana mambo ya WCB maana kila mja aliyepo Tanzania anaelewa mazuri yaliyotokea pale. Mengi yamefichika kuhusu kuondoka kwa Rich Mavoko pale, ila kwanini tufukue makaburi ya wafu?
Kilichopo ni kwamba Rich Mavoko baada ya kutoka WCB, aliamua kuanzisha lebo yake kwajina BillioneaKid. Katika kuchunguza kwetu, Mavoko wakati wote watanzania walipokua wanamuona yupo kimya, alikua mbioni kutengeneza lebo yake na uvumbuzi wetu ni kwamba fedha ambazo ametumia kuwekeza Mavoko kwa mradi huu niza kiasi cha haja.
Sababu kuu nikuhakikisha anafungua nafasi za kazi si kwak pekee, ila pia kwa vijana wenza. Kuna kampuni kadhaa za nchini Kenya zilitaka kumsajili, lakini kwasababu ya uzalendo na kuipenda Tanzania, Mavoko alikataa na kuamua kulinda hadhi yake kama Mtanzania.
Hii ni kwasababu yaupendo alionao kwa Watanzania wanzake. Watanzania japo wasanii wapo wengi, ila Rich Mavoko ni mfano wakuigwa, kwanini nasema hivi? Lebo yake ipo kwaajili ya Watanzania, inafaa Watanzania wafurahie kwani nafasi za kazi si kwa wasanii bali hadi kwa wadau mbalimbali wenye vipaji tofauti Tanzania.
J?e ni nani ambae alikua anafikiria hili? Ninani ambae anachukia maendeleo hapa Tanzania? Kwanini basi tusifurahie kama Lebo ya muziki ya BillioneaKid ikifunguliwa na kubuni nafasi za kazi kwa Watanzania?
Watanzania wanasifika kwa ukarimu, amani , upendo na umoja. Hizi ni nguzo muhimu, zinafaa zifatiliwe, na mtu kama Rich Mavoko akiwekeza kwenye biashara ya muziki na kuunda nafasi za kazi kwa vijana wenza ikiwemo wapiga picha, wanamitindo, watayarishaji wa muziki, waongozaji wa video na wengi wengineo kwanini Watanzania tusimushike mkono kama kijana mwenzetu na kumpa nafasi ya pili ili awezekuendeleza juhudi za kuitangaza Tanzania ulimwenguni kupitia kipaji chake cha muziki?
Watanzania si wanafiki, Watanzania wanaheshimika kwa kupenda na kuenzi vilivyo vya kwao. Basi kwanini Watanzania kwa sauti moja tusiikubali BillioneaKid na kazi zake? Tukumbuke wasanii wote wakali Tanzania wanahitaji malezi kutoka kwa Watanzania, tunapo wanyima nafasi hii, majirani siri na muibia wanafurahia. Maana panzi wakipigana faida kwa kunguru.
Rich Mavoko ni Mtanzania, anahitaji msukumo wa Watanzania wote, japo hakosi mashabiki kote Africa. Watanzania tufungue macho, kijana kama Rich Mavoko anapotamba kupitia muziki kwasababu ya musukumo wako wewe kama Mtanzania, ujue malipo yake ni Tanzania kuongeza nafasi za kazi si kwa wasanii pekee bali kwa Watanzania tabaka mbalimbali.
Wasanii ni wajasiriamali kama vile wakina na Mo Diweji, tuwape nafasi watuwakilishe na japo inaruhusiwa kumfuata msanii umpendae Rich Mavoko amerudi kuwakilisha Tanzania kama mzalendo mwengine. Watanzania kongole kwa umoja, upendo, na amani. Tumpe nafasi, tumusukume, na kumuenzi Mtanzania mwenzetu.