FIGHT FOR FREEDOM

FIGHT FOR FREEDOM

MATUMIZI YA MIHADARATI BADO NI MTAMBUKA


Utumiaji wa mihadarati  bado ni mtambuka licha ya serikali katika mataifa mbalimbali kuchukua hatu madhubuti ya kutokomeza utumiaji huo ambao kwa asilimia kubwa umesababisha athali kubwa kwa baadhi watu hususani kwa vijana ambao ndio waathilika wakubwa.

Vyazo mbalimbali vya habari ikiwemo tafiti ambazo zimefanyika hivi karibuni zimeweza kufafanua jambo hili ambalo bado linaendelea kushika kasi katika sehemu mbalimbali dunia  

Kwa mujibu wa shirika la Routers  dawa aina ya heloini imeongezeka kwenye pwani ya Kenya katika miaka ya hivi karibuni ikisemekana kuwa dawa hizo zinatoka mara nyingi   Afghanistan zikipitishwa Mombasa kuelekea mataifa ya Magharibi hii ni  kulingana na ripoti iliyotolewa hivi karibuni na umoja wa Ulaya.

Miji ya Mobasa,Malindi na Ramu imeonekana kuathilika zaidi hata hivyo mihadarati hiyo inapenya zaidi hadi kwenye miji mikuu kama  Nairobi hii ni kutokana na wingi wa matumizi pia uwezo wa kifedha wa wanaoishi hapo.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa baadhi ya watumiaji wa mihadarati wametengwa na jamii zao,mjini Mombasa baadhi ya washukiwa wa matumizi ya dawa za kulevya wameshambuliwa hata kufika hatu ya kuchomwa vilevile kuawa na haraiki ya watu ,

Hata hivyo imeleta picha mbaya sana kwa kuathili shunguli za kitalii nchini Kenya. Utafiti zaidi uiliweka wazi kuwa sababu kubwa ambayo inapelekea utumiaji wa dawa hizo ni ukosefu wa ajira kwa miongoni mwa vijana waishio eneo hilo.

Hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwemo mijadara kwenye Bunge, uhamasisho wa kijamii pamoja na ukamataji wa ulanguzi na kuchomwa kwa dawa  zinazopatikana ingawa hali inaonekana kuzolota licha ya juhudi zote hizo.

Kwamujibu wa mtandao wa Tai unaeleza kuwa nchini Tanzania matumizi ya dawa ya kulevya yameshuhudiwa miongoni mwa vijana ingawa hatua madhubuti zimechukuliwa kwenye  vita dhidi ya tatizo hilo,Tume yakudhibiti  mihadarati mijini Dar Es Salaam 2011 ilitoa lipoti kuwa idadi ya watumiaji ilikuwa 1050 lakini hadi miaka ya hivi karibuni imepanda zaidi ya nusu milioni.

Baadhi ya madhara yanayosemekana ni uharifu, magonjwa ya zinaa ajali za barabarani na mauji kutokana na matumizi ya dawa za kulevya.Mihadarati ambayo inatumika sana nchini Tanzania ni kama vile bangi,cats, heroini na kokeini. Hata hivyo katika siku za hivi karibuni idadi ya watumiaji inasemekana kupungua nchini Tanzania ikilinganishwa na Kenya.

Fayazani Mohamed ni moja ya aliyekuwa mtumiaji wa dawa hizo hapa anaeleza namna ilivyokuwa ngumu kwake kuacha pia alivyonza kutumia
“Nikijisemeye mimi mwenyewe ni hatua ngumu sana ya kusema nimechoka lakini niliweza kushauliwa, kuambiwa na dungu jamaa kwamba nisitumie kulingana nilikuwa nimechoka sana kiafya”.  Fayazani Mohamed alisema.  

Namna ambavyo alianza kutumia Fayazani alisema kuwa kulingana na uwezo wa fedha aliokuwa nao pia marafiki wabaya ndio ilikuwa chanzo cha kutumia matumizi ya dawa hizo, katika hatua ya kwanza mtu anajisikia raha sana ambapo inasababisha matumizi kuongezeka kwa kila siku .

Pia Ally Masito ni moja ya aliyekuwa mtumiaji wa dawa ambapo mpaka sasa ana miaka sita akiwa hatumii anasemakuwa yeye kwa upande wake kilichosababisha kutumia dawa hizo ni mahusino ya kimapenzi ambapo alimpenda binti kwa baadaye wazazi wa msichana huyo walikataa uhusiano huo na hapo akawa ni mtu wa mawazo mengi na ndipo akaona furaha kubwa ni kutumia dawa hizo ingawa bado iliendelea kumtesa kwasababu alijikuta akianza tabia ya wizi na unyanganyi  kitendo ambazo kilizidi kumtesa sana .

Taibu Abdul Rahmani ni mwanaharakari na mwanasaikologia pia mshauri akiwa pwani ya Kenya anasema kuwa tatizo hili ni kubwa sana ukiangalia hasa katika mwambao wa pwani tumeadhiliki pa kubwa sana na hili ni jambo ambalo lilitokea katika familia yetu na niliweza kupoteza mkubwa wangu katika janga la dawa za kulevya na ndiyo ikwa ni msukumo  kuingia na kusaidia wengine katika hali ambayo wanawezo kurudi kuwa sawa.

Kitu ambacho kinapelekea mtu kutumia dawa hizo zinakuja kwa njia nyingi sana ukiangalia suala la heroini ambao ndio unga utumiaji wake unahitaji kwa mara tatu kwa mtuamiaji sungu kwahivyo lazima uwe na ile chanzo cha wewe kuanza kutumia katika pwani Kenya   ukiangalia Mombasa mpaka Ramu elimu hakuna.

Kwahiyo katika jamii ya watu wanapokulia kuna muda fulani ambao tunakosea katika maisha kitu ambacho kinasababisha kuzama katika mambo kama haya pia matumizi ya dawa mengine ni kama vile bangi, mirungi,pombe ni baadhi ya vitu vinavyomsukumu mtu kuingia katika uraibu wa unga,

Athali zake ni kubwa sana moja wapo ni yakisaikolojia mtu anaathilika kwasababu kila siku anataka kutumia ili aishi vilevile afya yake inazolota kwasababu muda wote hufikilia kupata dawa kila siku.
Hata hivyo Agata Mbale alitoa mtazamo wake huku akipinga tabia ya watu kujihusisha katika tabia hiyo ambayo ni hatal “napinga sana kitu kiitwacho  mihadarati kwasababu husababisha vijina wengi kutoka na kuingia kwenya mambo mabaya ambayo ni maovu kutokana na kutumia mihadarati.

Mihadarati inakuwa mitaani watu wanaitumia wanaapotoka hasa hasa kwa vijana wengi wanashindwa kufanya kazi kwa kuendekeza mambo siyo ya msingi halafu mwisho wa siku wanakuja wanasema wanajuta.

Kwahiyo napenda kuwambia vijana wenzangu utumiaji wa mihadarati ni mbaya sana inatakiwa tuikwepe ili tufanye kazi kwa bidii kwa sababu vijana ni nguvu ya Taifa”; .Agata Mbale  kutoka Mrongoro Tanzainia.
Katika hali ambayo siyo ya kawaida baadhi ya watumiaji ambao wanashindwa kupanda dawa hizo wanatumia dawa ya panya, mafuta ya petrol na vingine vingi kwa ajili ya kujiridhisha.

Hivyo serikali katika mataifa mbalimbali bado inahitaji kuongeza juhudi katika kupambana na kutokomeza tatizo hili ambalo bado ni mtambuka.